Asante kwa mchango wako kiongozi; Nia yangu katika hatua ya mwanzo ilikuwa sio kuelezea sifa za hawa wawili bali sababu kwanini nadhani matukio ya sasa yatapelekea kuwa top three kwenye kinyang'anyiro hicho; Lissu nimemtaja kwa makusudi kama njia ya kuchokoza mada, hasa kuonyesha kwamba jina lako kupita CCM haitakuwa automatic kushinda Urais, hasa iwapo Chadema watafanyia kazi mambo kadhaa niliyojadili hapa na kwingineko; Vinginevyo nchi yetu inahitaji rais ambae:
1. Ana msimamo unaoeleweka juu ya muungano, hasa wenye kuweka maslahi ya Tanganyika na Tanzania kwa pamoja, na hafichi msimamo wake kwa kuogopa kuangamia kisiasa kwa kudai Tanganyika ndani ya Tanzania;
2. Ambae atakuwa ana heshimu utawala wa sheria;
3. Ambae atakuwa mkali juu ya ufisadi/rushwa;
4. Ambae ataendana na demographics zilizipo sasa katika population i.e. taifa kuwa ni la vijana;
5. Ambae anaonyesha uwezo wa kujenga hoja kuhusiana na maslahi ya taifa nje na ndani ya bunge;
6. Mwenye elimu, uelewa na pia upeo juu ya masuala la kisiasa, kijamii, kiuchumi, na kisheria, ndani na nje ya nchi;
7. ETC
Lissu anatosha katika mengi kama sio yote juu ya haya, na ni vizuri wagombea wa CCM muda ukifika nao wao tuwapime kwa haya na mengineo;