Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mchambuzi
Nakubali kwamba Membe bado yupo katika nafasi nzuri kuelekea 2015. Lakini kama alitaka kujipima, basi matokeo haya ya kuwa wa mtu wa 6 kati ya 10 inaonyesha yupo "vulnerable" mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu, japokuwa ameweza kupenya na kupata ushindi. Ukizingatia hao 6 wa mbele yake hawatajwi kuwa na nia ya kugombea Urais, nilitegemea Membe angepata kura zaidi kwavile anatajwa-tajwa sana kwamba anakubalika.
Nasema Lissu hana temperament ya kura Rais kwa vile amejijengea image mbele ya wapira kura wengi ya kuwa too volatile na too combative. Its the same Dr Slaa syndrome. Naamini mwisho wa siku Watanzania wengi wanataka Rais ambaye kwa personality ni muungwana, ambaye kijamii sio mchonganishi bali ni mlezi wa umma (tazama hasa Nyerere na Mwinyi, hata Mkapa na JK wanazo sifa hizi kwa kiasi fulani). Kwa maoni yangu Lissu's "abrasiveness" is good in opposition politics but he would have to moderate it in order to be a viable presidential material for the whole electorate.
Naamini humo CCM kuna watu ambao wana-qualify kuiongoza nchi hii, lakini sio January. Is this supposed to be a joke!
Mpaka hapa sikutaka kuendelea kusoma walaka wako ila CCM wakithubutu kumsimamisha Membe ili ashindane na Dr Slaa,Lissu basi wajue ndo mwanzo wa wao kuwa wapinzani!!pili wewe kwa mtazamo wako unajua EL atakuwa amelala tu anasubili wajumbe wa NEC wachague majina hayo mawili tu??wakati yeye kaisha wekeza!!Na kwambia kama tupo kati ya ulio wataja hapati hata mtu mmoja na kama ndo wanaambiwa wanaambiwa ili wasiongeze makundi ndani ya chama ila Mwenyekiti yeye anajua ninani atamsimamisha 2015!!
Mpaka hapa sikutaka kuendelea kusoma walaka wako ila CCM wakithubutu kumsimamisha Membe ili ashindane na Dr Slaa,Lissu basi wajue ndo mwanzo wa wao kuwa wapinzani!!pili wewe kwa mtazamo wako unajua EL atakuwa amelala tu anasubili wajumbe wa NEC wachague majina hayo mawili tu??wakati yeye kaisha wekeza!!Na kwambia kama tupo kati ya ulio wataja hapati hata mtu mmoja na kama ndo wanaambiwa wanaambiwa ili wasiongeze makundi ndani ya chama ila Mwenyekiti yeye anajua ninani atamsimamisha 2015!!
Je, ni vigezo gani hutumiwa na CCM kumpata mgombea Urais? Najua wengi katika mjadala huu wataleta hoja khanga, kofia, n.k, kwani ukweli ulio wazi ni kwamba Chama kimechafuka; Lakini tukiweka hili pembeni kwa sasa, Vigezo vinavyotumika kuteua jina la mtu kuwa mgombea Urais (CCM) vipo vingi, na vingine ni very arbitrary na pia mchakato wake sio democratic; Lakini huo ni mjadala mwingine, na kwa sasa ningependa kujadili vigezo vifuatavyo:
- Awe na Sifa za Kuwa Mbunge Kufikia Kipindi husika
- Awe Mjumbe wa NEC Kufikia Kipindi Husika
- Jina lake liwe familiar miongoni mwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa
- Asiwe amethibitika kwamba ni mla rushwa (tetesi hazitoshi)/Awe na Sifa Za Kukemea Rushwa
- Na Awe na Umri utakaovutia Wapiga Kura Vijana
Mada ni safi na quite objetive. Hapo nilipoweka red ni viongozi wangapi wa CCM waliothibitika kuwa ni wala rushwa na hawafai kuwa Rais wa nchi na wamechukuliwa hatua gani? Ingekuwa vizuri ukafafanua hil,i ili hiyo dhamira ya kumaliza rushwa kupitia chama tawala na serikali yake ifahamike kwa wananchi walioumizwa mno mno na mwenendo huu. Aidha itarudisha imani ya wananchi kwa CCM ambao wataendelea kukipa ridhaa ya kuendelea kutawala.
Umesema tetesi za rushwa hazina mashiko katika context ya hoja uliyoleta, sawa lakini hiki ni kitendawili!! Wala rushwa watathibitikaje ilihali hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa na vyombo husika? CCM imshukuru Mungu sana kwa umbumbu wa wananchi waliokosa elimu hasa wa vijijini na kuendelea kuridhika na CCM kwa kukosa uwezo wa kuelewa na kupambanua mateso waliyonayo kutokana na utawala mbovu wa miaka mingi chini ya chama hiki.
Kwa hotuba JK aliyoitoa,anaonekana amechoka na makundi na majina ya watu wanaotaka nafasi ya uraisi.
Japo,JK huwa hatabiriki katika kauli zake,nahisi sasa yupo tayari kuwatosa wote wanaotaka Urais(waliojitangaza au kuhisiwa kuitaka nafasi hiyo).
MEMBE:
Kwani kwa Nyakati tofauti,Membe naye amediriki kusema anawajua maadui zake(hii inaonesha yupo katika mchakato wa kuitaka nafasi hii ya urais!!!!).
Mkuu wa nchi atakuwa anajua nia ya Membe,japo hasemi na hataki kuonyesha kuwa yupo kundi lipi,lakini kwa nyakati tofauti,Vijana wa mkoa wa pwani waliwahi kusema rais hata toka kaskakazini,kauli ambayo mpaka leo hamna aliyejitokeza kuikanusha.!!!Kwa sasa sio lazima tena Rais achaguliwe kwa vigezo vya kuwa na sifa ya kujua itifaki,kuwa waziri wa nchi za nje.kwani bado vigezo hivi havisaidii kwani JK amekuwa anasafiri mara kwa mara na wananchi hawataki tena kuwa na mtu anasafiri huku mambo ya nchi hayaendi vizuri.Wananchi hawezi kushawishiwa na sifa za mtu anayetoka katika wizara aliyotoka mtangulizi wake.
Kwa vile tayari naye ni sehemu ya watu wenye makundi ndani ya chama,nahisi sasa hivi Chama kinweza kuondokana na makundi kwa kuteua Mgombea ambaye hatajwi wala hana makundi ili kulinda CCM isiendelee kugawanyika.!!
Kwa mantiki hii hata Membe hatapitishwa kugombea Urais 2015.!!!!
JANUARI MAKAMBA:
Jamii kwa sasa haitapenda ugombea Urais kwa kubebwa na hasa majina ambayo ni watoto wa waliokuwa wanasiasa,kama huyu Januari Makamba.!!.Huyu labda anajiimarisha kwa ajili ya hapo baadae awe imara kisiasa kwani awamu hii imembeba,ndio alipoibukia katika siasa.Ujue kuna watanzania wengi wenye vipaji,lakini njia ya kufikia nafasi kama hizi inakuwa ngumu ndani ya CCM,kwa vile hawana fedha.Januari,nahisi hawezi kuchaguliwa kugombea nafasi ya urais ,kwa vile jamii itakuwa nataswira ya WATOTO WA VIGOGO kubebwa,tena kurithishana madaraka ndani ya CCM,nafasi inatoka kwa baba kwenda kwa mtoto(Wazee wengi,kila mtu anataka mtoto wake awe na nafasi katika chama).
una maana EL angegombea kupitia kapu la taifa angeangukia pua?ndivyo unavyoamini?labda sijakuelewa vizuri!
Hujamuweka Lowassa??? Unatafuta ugomvi na Pasco and Co.