Mchambuzi, nakubaliana na wewe kwamba katika wajumbe 10 waliogombea NEC, Membe anaweza kufikiriwa kuwa mgombea wa CCM. Ingawa amepata nafasi ya sita kiuchaguzi, haimanishi hakubaliki sana kwa wajumbe, bali imetokana na vita vya kisiasa ambavyo vilielekezwa kwake kwa vile anajulikana ana malengo ya uraisi, hivyo alifanyiwa kampeni za kinyume kumzuia, hivyo kitendo cha kupata nafasi ya sita ni sifa tosha ya kuwa mpiganaji na kuvutia makundi ambayo hayakupenda kampeni chafu na maneno ambayo yalilenga kumboa na kumharibia sifa ili akose nafasi ya NEC.
Hata hivyo, naamini CCM bado wanaweza kumleta mtu mwingine nje ya wajumbe wa NEC au watu wengine wenye mvuto ambao ni wajumbe wa NEC kupitia wilaya. Kama walivyofanya kumleta Mangula , nafasi ya m/mwenyekiti.
Kwa jinsi ambavyo siasa za makundi zilivyoitesa CCM, si ajabu wakatumia ule mkakati wao maarufu wote wakose na wakaja na mtu mpya.
Swali ni kwamba , je kuna watu ambao wanaweza kuthubutu kuingia kinyang'anyiro cha kuwa mgombea wa CCM, bila kuhofia madhara yanayoweza kukupata endapo, utaonyesha dhamira ya kugombea halafu ukakosa. Hapo ndipo , wengi hukimbilia bora kujiunga na kambi fulani za wagombea, lakini mwisho wa siku ni kupata madhara yale yale endapo kambi uliyoiunga mkono haifanikiwi.
Hatima basi ni nini? Kwa vile mchakato wa CCM una matatizo mengi ya kumpata mgombea, kwani CCM itakuwa imejeruhiwa sana kumpata mgombea, basi upinzani una nafasi nzuri ya kutoa mgombea. Lakini kumbuka, CCM hawataacha mgombea mzuri apatikane kutoka kwa wapinzani. Mkakati wa mapandikizi ndani ya vyama vya upinzani umepata mashiko sana kwa watu wengine.
Mapandikizi ni pamoja na wagombea wenye kauli au msimamo ndumi la kuwili, pandikizi la udini na ukabila, haya yote yatafanya kazi kinyume cha kupata mzuri hasa CDM au atakapopatikana mgombea mzuri.