Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,434
- Thread starter
- #141
Nguruvi3,
Asante sana kwa mchango wako; Migiro binafsi namuweka kwenye top 5 lakini sioni akipita kwani kufikia 2015, nchi itakuwa imeyumba sana na yenye kuhitaji utatuzi wa masuala mengine mengi ya msingi na muhimu kuliko suala la gender equity; Urais wa mwanamke unaendana na perception ya udhaifu, na sidhani kama watanzania wapo tayari kutoka kwenye hali ya sasa na kuingia katika hali nyingine ambayo itafanania na hii ya sasa, kama sio kuizidi; Kutakuwa na agenda kuu tano kuelekea 2015:
Migiro atasukumwa sukumwa weee, na hatimaye kukutana na Meghji's Syndrome kwani kwa hoja hiyo hiyo ya gender n.k. Meghji inasemekana ndiye aliyekuwa chaguo la mwenyekiti kama mgombea mwenza mpaka dakika ya mwisho; To put it in a better perspective, hakuna mgombea atakayepita kwa kubebwa na mwenyekiti kwa asilimia 100; Atakayepita ni yule atakayejisaidia mwenyewe, na baadae kupigiwa krosi, assuming chama kitabakia intact mpaka uchaguzi 2015;
All in all, i still believe kwa hoja nilizojenga kwamba agenda kuu itakayotawala ni aidha Ufisadi au Kura za Vijana; Vinginevyo suala la kuwa na mgombea wa kuvunja makundi litakuja kwa kuchechemea sana kwani ili mtu huyu afanikiwe, atahitaji kuungwa mkono kwa fedha na kundi fulani...; Hata 1995, licha ya makundi kuvunjwa, watu fulani fulani bado walihitajika kifedha kusaidia kampeni na ndio maana mpaka leo wana nguvu; kwahiyo tatizo la makundi litajirudia tu hata ateuliwe nani kwani kwenye maamuzi muhimu ya Chama, watawala wa CCM hawapishani kihoja au itikadi bali maslahi; Vita hivi vitakuwa very interesting, tuombee uzima tuvishuhudie;
Pia kwa mtazamo wako, jukumu kubwa la Mangula na Kinana litakuwa ni nini hasa katika yote haya;

- Ufisadi - membe akiwa mgombea
- Vijana - January akiwa mgombea
- Kuokoa Muungano, zamu yetu wazanzibari - Karume
- Jinsia - Migiro
- Mtu asiye na makundi - hatumjui bado ingawa tayari jina lake sio geni masikioni mwetu; Migiro katika hili la tano hatoshi kwani inajulikana wazi kwamba karibikia katika kipindi chote chaa wamu ya nne, nafasi zake za uongozi mara nyingi hazijawa za kupigiwa kura bali kuteuliwa;