Mgombea Urais Hiram avunja ushirikiano na FDC/CFD, asema Biya hajashinda Uchaguzi wa Cameroon 2025

Mgombea Urais Hiram avunja ushirikiano na FDC/CFD, asema Biya hajashinda Uchaguzi wa Cameroon 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Raia wa Cameroon walipiga kura Jumapili, Oktoba 12, 2025, katika uchaguzi unaotarajiwa kumrejesha madarakani Rais Paul Biya, mwenye miaka 92, ambaye ameiongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miongo minne. Uchaguzi huo, uliofuatiliwa kwa karibu na wachambuzi wa ndani na wa kimataifa, umeibua mjadala mkubwa kuhusu uwazi, uhuru wa vyombo vya habari, na ushiriki wa upinzani.

Wakati Tume ya Uchaguzi ikiwa bado haijatangaza matokeo rasmi, baadhi ya wanasiasa na viongozi wa vyama wameanza kutoa kauli kuhusu mwelekeo wa matokeo hayo. Miongoni mwao ni Denis Émilien Atangana, Mwenyekiti wa Chama cha FDC/CFD Taifa, ambaye ametangaza kumtambua Rais Biya kama mshindi wa uchaguzi huo, hatua iliyozua mgongano na baadhi ya viongozi wa upinzani.

1760428115045.png
Kwa upande wa Mgombea wa urais Hiram Samuel Iyodi kupitia chama chake mwenyewe, cha MP3 (Mouvement Patriotique pour la Prospérité du Peuple), aliyeungwa mkono awali na FDC/CFD, kabla ya tarehe 13 Oktoba 2025, kuandika barua rasmi ya kusitisha ushirikiano wake na chama hicho, amesema wazi kwamba serikali haikushinda uchaguzi huo, akijibu moja kwa moja taarifa ya Denis Émilien Atangana aliyetoa kauli ya kumtangaza Rais Biya "Mshindi."

1760428201010.png
Katika tamko rasmi, la Kohtem Princewill Sambit, Mratibu wa Timu ya Kampeni za Hiram 2025 na Mtendaji Mkuu wa Chama cha siasa cha MP3, naye ametangaza kujitenga kabisa na kauli iliyotolewa na Atangana aliyedaiwa kuwa na uhusiano na serikali na Rais wa Kitaifa wa FDC/CFD, chama kilichomwidhinisha kugombea kwa Hiram, kuhusu ushindi wa rais aliyeko madarakani.”

Kohtem Princewill Sambit, amesisitiza kuwa imani yao iko katika mapambano ya pamoja kwa ajili ya mabadiliko, utu, na urejesho kamili wa mamlaka ya watu.

Hiram25.jpg
Soma
 
Cameroon ni nchi ya hovyo kama Tanganyika tu
 
Back
Top Bottom