Uchaguzi 2020 Mgombea Urais kupitia ACT-Wazalendo, Bernard Membe achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC

Uchaguzi 2020 Mgombea Urais kupitia ACT-Wazalendo, Bernard Membe achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC

Mgombea Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo pamoja na mgombea mwenza Profesa Omar Hamad leo Agosti 7, 2020, tayari wamekwishachukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za NEC Jijini Dodoma.


Mbona azam TV walisema Mpaka kesho coz Leo haikuwa zamu Yao,

Wao ni kesho na chadema na chama kingine
 
Anaenda kumtoa ikulu bwana yule...sjui kwanini anaogopaga kumtaja jina!!
Amtaje jina?

Kila kitu alichonancho Membe maishani kwake from Kazi yake,mali zake,kazi nzuri za watoto/ndg zake kazipata kupitia/chini ya CCM sasa aje ajaribu kumtaja taja huyo Magufuli aone kama hajarudishwa kwny enzi za ujima.

Nyalandu nae alianza kuleta zile kampeni za kistaarabu kujifanya anaogopa kumtaja taja Magu naona Chadema wakaona usituchezee wewe kaa pembeni kwanza na siasa zako za busara busara.

Membe kampeni zake zitakua za kufurahisha sana maana atajifanya kuleta busara nyingi jukwaani huku watu wakitaka kusikia vitu konki/vitu org/vitu vigumu.
 
Mtu yeyote anayeamini kuwa Membe ni mpinzani basi huyo ana ukichaa ambao hata Mirembe hawawezi kuutibu
Hii ndio hofu yangu, kama kweli angekuwa mpinzani angemuunga mkono Tundu Lissu, the guy he is in opposition wing for a special mission like Lowasa.
Tundu Lissu na Chadema wakae vizuri, waelewe kuwa kura za ACT zishagawanywa
 
Sasa mbona wanatuchanganya siamuachie TL au wote wautaka Urais? Mwaka huu kazi ipo.
 
Mgombea urais wa JMT mh Membe wa ACT wazalendo leo amechukua fomu za kugombea katika ofisi za tume ya uchaguzi jijini Dodoma.

Kila la kheri.

Source Eatv
Maendeleo hayana vyama!
Huyo ndio JASUSI Mbobezi , Huku NIYEYE huku JASUSI wakimpa za Uso JIWE.
 
Ana miss zile shirt za kijani .sio hizi batiki za zambarau

SUBIRI KIDOGO
 
Hivi Membe kabisa yupo serious ?Hope mbeleni atamwachia Lissu. To be honest Ukijumlisha kura za zote upinzani mwaka 2015 ,upinzani walimshinda Magufuli tatizo ushindi wao waliugawana.
Hii ni hofu kwangu, baadae inawezekana vipi kama form kashachukua NEC? Inanijilia kwa ugumu flani kuamini kama jamaa ni mpinzani wa kweli.
 
Hivi Membe kabisa yupo serious ?Hope mbeleni atamwachia Lissu. To be honest Ukijumlisha kura za zote upinzani mwaka 2015 ,upinzani walimshinda Magufuli tatizo ushindi wao waliugawana.
Hata sasa wapinzani wamegawanyika kwa kuwa kila mmoja anafikiri anatosha kuingia Ikulu.
 
Back
Top Bottom