Uchaguzi 2020 Mgombea Urais kupitia ACT-Wazalendo, Bernard Membe achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC

Uchaguzi 2020 Mgombea Urais kupitia ACT-Wazalendo, Bernard Membe achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC

Hivi Membe kabisa yupo serious ?Hope mbeleni atamwachia Lissu. To be honest Ukijumlisha kura za zote upinzani mwaka 2015 ,upinzani walimshinda Magufuli tatizo ushindi wao waliugawana.
Bado mnamwamini zitto??

Kwanini upinzani nchii hii hatujifunzii tu
 
Hisia zangu zinanituma kuwa Membe huenda yupo ACT kimkakati! Atagawa kura za Tundu Lissu na kumpa gap kubwa la kiuongozi Mzee baba.

Kama Membe atapata kura basi hizo kura hazitakuwa za yeyote yule in the first place bali ni zake. Usiwafanye wananchi kuwa hawajui wa kumchagua
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Chama cha upinzani Tanzania ni kimoja tu nacho ni CHADEMA na Mgombea wake ni Tundu Lissu. Vyama vingine vyote ni matawi ya CCM.

Kwa maana hiyo CCM ina wagombea wengi ambao watazigawa kura za CCM, na upinzani una mgombea mmoja tu Tundu Lissu ambae atapigiwa kura zote za upinzani. Sijui hofu yako kwa Membe kugawanya kura za upinzani inatoka wapi? Wewe shangilia tu CCM inagawanya kura zake hivyo kumpa uhakika wa ushindi Mgombea wetu wa upinzani Tundu Lissu.
Hapa nimekuelewa
 
Mgombea Urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo pamoja na mgombea mwenza Profesa Omar Hamad leo Agosti 7, 2020, wamechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za NEC Jijini Dodoma.

View attachment 1529783
View attachment 1529827
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mh. Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akikabidhi fomu za kugombea kiti cha Rais kwa Mgombea wa Chama cha ACT-Wazalendo, Bernard Membe katika Ofisi za NEC Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 7,2020, kushoto ni Mgombea Mwenza, Prof. Omar Faki Hamad . Chama hicho kinakuwa cha nane kuchukua fomu.

View attachment 1529828

====
TAARIFA KWA UMMA

MEMBE ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Mgombea Urais wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ndugu Bernard Kamilius Membe leo tarehe 7, Agosti 2020 amechukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Membe amekabidhiwa fomu hiyo ya uteuzi na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage Jijini Dodoma.

Katika uchukuaji huo wa fomu, Membe aliambatana na Mgombea mwenza wake, Profesa Omary Fakih Hamad.

Aidha msafara huo wa Membe uliongozwa na Mwenyekiti wa Chama, Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu, Ndugu Ado Shaibu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Ndugu Mhonga Said Ruhwanya, Katibu wa Mambo ya Nje Ndugu Bonifasia Mapunda, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma, Ndugu Janeth Rithe, Katibu wa Ngome ya Vijana Ndugu Mwanaisha Mndeme na viongozi wengine waandamizi wa Chama.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa fomu hizo, Ndugu Bernard Membe amesema kuwa amejiandaa kufanya kampeni kabambe kila Kona ya nchi ili kuipatia ACT Wazalendo ushindi mnono na kuhakikisha ifikapo tarehe 28 Oktoba 2020, utawala wa Rais Magufuli unafikia tamati.

Imetolewa na:
Janeth Joel Rithe
Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma.

Imetolewa leo tarehe 07 Agosti 2020.
Asante upinzani hii ni tactic pia ya kijasusi.

Thanks tumeelewa.
 
Huyu kachero ni mharibifu tu maana nna uhakika baada ya uchaguzi ataombara radhi na kurejea ccm....

Tunakwenda na Tundu Lissu
Huyu Membe ni mpinzani wa Magufuli sio CCM
 
CCM lazima wadate sababu hawajui wa deal na nani? Lissu ama Membe!! Huku kuna Zitto huku kuna Mbowe...Huku Kuna Maalim Self huku kuna kina Mdee; Lema; Msigwa, Sugu!!

Kweli uchaguzi huu unakwenda kuandika historia mpya kwa taifa letu.


Kweli safari hii aibu inakwenda kumwangukia mtu.
ukishiba maharage tembea na toilet paper sio unakunya tu kila sehem
 
Membe tunamsoma tu. Kama hamuungi mkono Lissu hata huo Uwaziri Mkuu ambao angeupata baada ya Lissu kuwa Raisi atausikia kwenye bomba.

Anatakiwa aamke kama anataka kweli kuleta mabadiriko Tanzania. Ila kama nae ametumwa kama walivyotumwa wengine basi tunamwambia tu nae ataingia kwenye historia ya aibu mwaka huu. Ataenda kunyang’anyana iyo asilimia 30 atakayopata Magufuli maana TUNDU ANTIPAS LISSU anaenda kubeba asilimia 70 ya kura zote hapo October 2020
70%Hiii ni kiwango tosha cha kuua Corona virus na sio urais kwa Tundu
 
Hivi Membe kabisa yupo serious ?Hope mbeleni atamwachia Lissu. To be honest Ukijumlisha kura za zote upinzani mwaka 2015 ,upinzani walimshinda Magufuli tatizo ushindi wao waliugawana.
Ebu tupe kwa tarakimu tuone kama walimshinda. Maneno ya kutunga hayana uhakika - hata iweje.
 
CDM acheni ubinafisi na uchoyo wa fisi kila mmoja ashinde mechi zake bila kumtegemea mwenzake. Mwaka 2015 wenzenu CUF na NCRR waliwaunga mkono mkajiona mnakubalika, sasa ni zamu yenu kuwaunga mkono wenzenu.
 
Back
Top Bottom