Uchaguzi 2020 Mgombea Urais mmoja leo kalalamika eti kuna watu wamejitokeza kumpinga kwa kugombea

Uchaguzi 2020 Mgombea Urais mmoja leo kalalamika eti kuna watu wamejitokeza kumpinga kwa kugombea

Joyce joyce

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2020
Posts
457
Reaction score
1,973
Wakuu, kuna Mgombea Urais mmoja leo amelalamika sana akituhumu watu wa vyama vingine kujitokeza kugombea nafasi ya urais, akisema kuwa mbona Mkapa, Kikwete na Mwinyi wao walipewa miaka kumi? Anahoji kwani yeye ana makosa gani? Nimeshindwa kuelewa wakuu kwani hao aliowataja walipita bila kupingwa? Kwenye kumbukumbu zangu nakumbuka wote hao waligombea na wapinzani waliweka wagombea urais, sasa huyu wa leo kusema maneno hayo nimeshindwa kabisa kumwelewa.

Lakini kuna kitu nimekigundua kuwa huyu mtu hapendi kupingwa, kumbe ndio maana hata kushauriwa au kukosolewa alikataa katakata nimejaribu kugmfuatilia hata huko nyuma kumbe kwenye ubunge Siku zote alikuwa anapita bila kupingwa alikuwa anafanya vigisu vigisu hadi wenzake wanaondolewa, ni tabia yake.

Pia nimejiuliza kwani anapolalamika kuwa wenzake walipewa miaka kumi inamaana ameishajua kuwa Watanzania wamemkataaa? Swali langu amejuaje kuwa hatapita? Amejuaje kuwa mwisho wake ni miaka mitano? OK tunashukuru kajua kuwa watanzania wameishasema no.

Niwakbushe kitu ambacho hamkijui "MANENO YANAUMBA"

Kumbe hata hiii ya kuua democracy huyu mzee ni kitu kilicho kwenye damu, na maneno hayo aliyoyasema kayasema mara kwa mara na si Dalili Nzuri Mtumishi Kama huyu kupewa nchi nihatariiiii kuliko mnavyofikiri mtu kama huyu anaweza kukugeuka mtu yoyote uwe CCM Au upinzani, uwe ndugu au usiwe ndugu, watu wa aina hiii hawapaswi kuwaachwa wakapita wakuuu chukueni tahadhali mtu kama huyu anaumiza kote kote na watu kama hawa hawaondokagi madarakani mtakuja kujuta huko mbeleni, leo utamuunga mkono kesho atakugeuka itakula kwako unaemuunga mkono kisa uko nae kwa sasa.

Hivi mwanamume anaemtongoza mwanamke anaenda Kwa kigezo kuwa mbona Fulani ulimkubalia kipindi kile? Kwan nini Mimi unaninyima? Tobaaa

Mnasema mtapita Kwa asilimia tisini, mnaimba nyimbo kila kukicha kuwa mtapita Kwa kishindo huku mnatenda ukatiri wa kiwango cha juuu ili mpate viti maaalum, sasa kila kitu chenu mnatumia vitu vyoote vya serikali sasa mnaogopa nini kuruhusu kuingia uwanjani? Kama mnajiweza mnakaa na kuimba imba kuwa mtapata kura nyingi, huku mnafanyia ukatiri mwanamke Yule wa mlimba mnamuogopa mwanamke? Halafu mnaimba mapambio kuwa mtashinda Kwa kishindo? Utwmshindaje? Mnashindana na Nani?

Mama wa mlimba amewasilisha risti anewakabidhi Kwa Picha na video, Mkurugenzi amepokea mkononi risiti video inaonekana akishukuru kupewa, anamwiita Afisa wake anamkabidhi Kwa mkono video inaonekana hadharani anaagiza waandikie kwenye kitabu huku anakenua Meno video yoooote inamuonesha had mkono wa kupokea Halafu mnamwambia kuwa weka pingamizi kuwa hakuleta risiti, Loooh hata mshiba wa aibu Hamna? Huku mnatamba kuwa mnapendwa huku mnatenda ukatiri, ole wenu hiii haikutokea tarime tungewashikisha adhabu, tungewaambia wanaume kuwa hamkutendewa nyie tumetendewa sisi ngoja tuwanyoooshe wenyewe, mnabahati nyie sio huku tarime

Mijitu Kama hiii ikishtakiwa wa wababe wenzao inaaaza kusema mara ooh mabeberu. Msipomrudisha mtakuja kutajana tunawwambia
 
Pia waambieni watu kuwa Magufuli atashinda kwa jinsi Tanzania ilivyo, wafunzeni kweli hii, ili kuepusha mishtuko ya kukata tamaa, au tumesahau wale waliofukiwa kifusi siku za kutosha pale kahama mpaka uchaguzi ukaisha na matokeo yakatangazwa Magufuli kashinda huku wao walitegemea Lowasa angeshinda, matokeo yake, waliuguza moyo badala ya adha za shimoni!

Huo ndio Ukweli,

Tanzania Bado kwa misingi ya Elimu, au so nyie mliwahi pendekeza bila kuwa na elimu ya angalau form four mtu asiruhusiwe kupiga kura?
 
Pia waambieni watu kuwa Magufuli atashinda kwa jinsi Tanzania ilivyo, wafunzeni kweli hii, ili kuepusha mishtuko ya kukata tamaa, au tumesahau wale waliofukiwa kifusi siku za kutosha pale kahama mpaka uchaguzi ukaisha na matokeo yakatangazwa Magufuli kashinda huku wao walitegemea Lowasa angeshinda, matokeo yake, waliuguza moyo badala ya adha za shimoni!...
Wewe unaleta hoja tofauti na bango langu, utakuwa una utindio wa ubongo, kinachoulizwa Hapa nikuwa Kwa nini anasema kuwa watanzania wanataka kumpa miaka mitano Wakati wenzake walipewa miaka kumi?

Yeye mwenyewe anahoji hivyo kwenye mkutano wake, sasa tunauliza Kwa nini anaona kuwa watanzania wamemkataaa? Inamaanaa ameshtuka na Kwa nini anatumia kigezo cha waliopita kuwa mbona wao walipewa kumi? Ina maaana ukimtongoza mwanamke unatumia kigezo cha mwenzio kuwa mbona yeye alikubaliwa?
 
Wakuu, kuna mgombea urais mmoja leo amelalamika sana akituhumu watu wa vyama vingne kujitokeza kugombea nafasi ya urais, akisema kuwa mbona Mkapa, Kikwete na Mwinyi wao walipewa miaka kumi? Anahoji kwani yeye ana makosa gani? Nimeshindwa kuelewa wakuu kwani hao aliowataja walipita bila kupingwa? Kwenye kumbukumbu zangu nakumbuka wote hao waligombea na wapinzani waliweka wagombea urais, sasa huyu wa leo kusema maneno hayo nimeshindwa kabisa kumwelewa...
Jiti ambalo hata historia halijui sijui liliwezaje kupewa urais
 
Wakuu, kuna mgombea urais mmoja leo amelalamika sana akituhumu watu wa vyama vingne kujitokeza kugombea nafasi ya urais, akisema kuwa mbona Mkapa, Kikwete na Mwinyi wao walipewa miaka kumi? Anahoji kwani yeye ana makosa gani? Nimeshindwa kuelewa wakuu kwani hao aliowataja walipita bila kupingwa? Kwenye kumbukumbu zangu nakumbuka wote hao waligombea na wapinzani waliweka wagombea urais, sasa huyu wa leo kusema maneno hayo nimeshindwa kabisa kumwelewa...
Labda interijensia itakuwa inaonyesha kuwa kura zinazidi kupwaya ......!!
 
Wewe unaleta hoja tofauti na bango langu, utakuwa una utindio wa ubongo, kinachoulizwa Hapa nikuwa Kwa nini anasema kuwa watanzania wanataka kumpa miaka mitano Wakati wenzake walipewa miaka kumi? Yeye mwenyewe anahoji hivyo kwenye mkutano wake, sasa tunauliza Kwa nini anaona kuwa watanzania wamemkataaa? Inamaanaa ameshtuka na Kwa nini anatumia kigezo cha waliopita kuwa mbona wao walipewa kumi? Ina maaana ukimtongoza mwanamke unatumia kigezo cha mwenzio kuwa mbona yeye alikubaliwa?
Unaposema Ina maana ...... unajijibu kwa hisi zako, wewe hujui huu ni wakati wa kampeni, wakati wa kuamua. Mtindio wa ubongo hauhusiki, usidhani wenye utindio hawana upeo, nakazia jipange kihisia za matokeo, tumaini la mwelekeo unaowazia halipo.
 
Back
Top Bottom