Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Yustas Rwamugira, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, 2025, akisisitiza kuwa uchaguzi upo kwa mujibu wa Katiba ya nchi na kwamba kila Mtanzania ana wajibu wa kushiriki katika mchakato huo muhimu wa kidemokrasia
Rwamugira ametoa wito huo leo Jumatatu, Oktoba 27, 2025, wakati akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Marangu Mashariki, Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro, ambapo amewataka wananchi kupuuza maneno ya mtandaoni na kila mmoja ajitokeze kupiga kura
“Nendeni mpige kura, mmalize muende nyumbani. Najua kumekuwa na maneno kwenye mitandao ya kijamii wakidai hakuna uchaguzi, hayo ni maneno yasiyo na kichwa wala miguu. Uchaguzi upo na unafanyika kwa mujibu wa Katiba,” amesema Rwamugira
Amefafanua kuwa muda wa uongozi wa Serikali iliyopo madarakani umeisha kikatiba, hivyo ni haki ya wananchi kuchagua viongozi wapya
Ameeleza kuwa mfumo wa vyama vingi upo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo wananchi wasirubuniwe na taarifa za upotoshaji
Soma pia GE2025 - Mgombea urais TLP: Uchaguzi upo, yeyote anayesema hakuna Uchaguzi Mitandaoni atachukuliwa hatua
Chanzo: Mwananchi_official