Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mgombea Urais wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Yustas Rwamugira amesema chama hicho hakiungi mkono vyama ambavyo vinanadi uchaguzi usifanyike,na badala yake kuwataka wananchi wajitokeze kupiga kura kwa wingi Oktoba 29.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadahara uliofanyika viwanja vya Mabanda ya Papa Mkoani Tanga, Jumamosi Septemba 27,2025 amesema watanzania wajitokeze kupiga kura na kuchagua viongozi ambao wataweza kusaidia kutatua yale ambayo yanawakabili kwenye maeneo yao.
Amesema ameona kwenye mitandao ya kijamii kuna makundi yanahamasisha wananchi wasipige kura,jambo ambalo ni kosa kisheria ila chama chake hawaungi mkono mambo hayo na kuwataka wananchi wajitokeze kwa wingi Oktoba 29 kuchagua viongozi wao.
Ameeleza kuwa kama TLP wao uchaguzi upo na unakwenda kufanyika na wote ambao wanahamasisha watu wasijitokeze kwenda kupiga kura vyombo vya dola vipo ma watakwenda kuchukuliwa hatua za kisheria.
Amewataka wananchi wasishawishiwe kutoa kadi zao za kupiga kura kwa mtu yeyote yule na badala yake wazitunze ili wakati ukifika wakapige kura,kwani hiyo ni haki yao ya msingi na wanatakiwa kuitekeleza.