YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 52,001
Kuna maajabu yanayovunja katiba za vyama kwenye uchaguzi huu mkuu.
Tumeona Lisu Makamu mwenyekiti taifa wa CHADEMA na mgombea uraisi kupitia Chadema akitoa tamko kuwa anamuunga mkono Mgombea uraisi wa Zanzibar Maalim Seif wa Act wazalendo.
Pia tumeona Maalim SEIF Mwenyekiti wwa ACT wazalendo taifa akimuunga mkono Tundu Lissu.
Sina shida na kuungana mikono hata kuungana miguu ruksa.
Ninachohoji kwa mujibu wa katiba za vyama vyao hayo maamuzi yalitakiwa kufanywa na kamati kuu na mikutano mikuu yao sio wao kujiamulia kwenye majukwaa!
Ninaomba ufafanuzi kuhusu hili kutoka kwa wataalamu wa sheria na katiba liko sahihi? kama haliko sahihi nini kinatakiwa kufanyika?
Kwa mfano Membe ni Mgombea uraisi wa ACT wazalendo aliyepitishwa na vikao halali kuanzia kamati kuu hadi mkutano mkuu. Na kapoteza pesa zake za kuchukua fomu na gharama za kuzunguka nchi nzima kutafuta wadhamini na akaanza kugharimia kampeni zake leo mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Maalim Seif anasema hamtambui anamtambua Lissu.
Pia upande wa Zanzibar kuna mgombea uraisi kupitia Chadema Vikao vya chama vya kamati kuu na mkutano mkuu walimptisha Said Issa Mohamed kuwa mgombea uraisi wa Zanzibar kaingia gharama za kuchukua fomu na kuzunguka nchi nzima ya zanzibar kutafuta wadhamini leo Makamu mwenyekiti wa Chadema Taifa Tundu LIsu anasema hamtambui anamtambua Maalim Seif wa ACT wazalendo kinyume cha katiba ya chadema na maamuzi ya kamati kuu na mkutano mkuu wa Chadema.