Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,559
- 11,180
Iwapo vetting ya viongozi ingefanywa na JF asingepita mtu labda aje malaika!
Maneno mazuri sana haya japokuwa yalitoka siku nyingi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Iwapo vetting ya viongozi ingefanywa na JF asingepita mtu labda aje malaika!
..ukisikiliza hotuba za Magufuli anazotoa mbele ya "laisi" Dr.Jakaya "Mlisho" Kikwete ndiyo utachoka kabisa.
Duh! JF kuna mambo. Kwahiyo itabidi aende "tuition" ya kiswahili kwanza!
Wanabodi,
Leo nimekutana na rafiki yangu wa siku nyingi, ambaye ni mtu wa kuaminika na ni kada wa Chama cha Mapinduzi-CCM, akanieleza seriously habari za kushtusha kidogo ambazo mimi pia zimenihuzunisha, kunisikitisha na kunisononesha!, kuwa eti imeishaamuliwa mgombea wa urais wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi-CCM ni Mhe. John Pombe Magufuli!.
Kilichonistua, kunihuzunisha, kunisikitisha na kunisononesha, ni the reasons behind alizonitajia ambazo ndizo zimepelekea CCM kuamua why ni lazima awe Magufuli tuu, and no one else!.
Kwa vile sababu hizo alizonitajia, baadhi ni justifiable na nyingine sio tuu ni unjustifiable!, bali hazikubaliki kabisa katika Tanzania ya leo!. Naomba kwa sasa nisizitaje kwanza, kwa sababu habari zenyewe nimezisikia from a single source, nahitaji kwanza kufanya collaborative verification na kupata attribution ili nijiridhishe kuwa ni za kweli na kuthibitisha kuwa hivyo ndivyo CCM inavyoweza kufikia maamuzi based on hayo niliyoyasikia!, then nitaziweka hadharani hizo sababu za CCM on Why ni Magufuli!.
Kwa kawaida sisi waandishi, ukipata taarifa kama hii, huwa inaitwa "news tip", haukimbilii kuiandika mbio mbio mpaka kwanza uifanyie verification kuthibitisha ukweli wa taarifa yenyewe, lakini kwa vile sasa tunaishi kwenye "the world of information age", nimeamua kuileta hii "news tip" humu jf, hivi hivi ikiwa kwenye hatua ya "tip" kabla hata ya verification, ili wewe kama mwana JF, uipate ile advantage ya JF, "be the first to know!", hivyo nawaombeni tuu sasa mkae mkijua, "Mgombea wa CCM 2015 ni John Pombe Magufuli!"
Nikiisha "confirm" neno "tetesi" litaondolewa na kuwa replaced na neno "confirmed!", na nitaziweka hizo sababu ila sasa ndio zijadiliwe!, na nawahakikishia wale wote wenye mapenzi mema na taifa hili, mkizisikia hizo sababu za CCM!, na nyinyi pia zitawashtua, kuwahuzunisha, kuwasikitisha na kuwasononesha!. Naomba nisiwatajie jina la huyo source wangu chini ya kinga ya kihabari inayoitwa "The Confidentiality of the source".
NB. Sio kila thread ni lazima ichangiwe, saa nyingine itoshe kujisomea tuu na kujipitia bila kuchangia chochote!. Hii ni just a news tip, kwa vile nimewaahidi naifanyia verification kuithibitisha, nawaombeni msiniulize swali lolote at this stage, kwa sababu sitajibu chochote!, and if possible nawashauri na nyingi msome FYE only na sio lazime mchangie kwa sasa na badala yake mvute subira kusubiria verification.
Sababu ya kuiwahisha humu JF kabla ya verification ni ili tuu wewe kama mwana JF to be the first to know!. Information is power!, if you are the first to know, then you'll have the powers to make good things happen or not to happen if they are bad things!.
Asante.
Pasco.
Naona CCM wamefanyia kazi maoni yangu na wengine waliokuwa wanawaza kama mimi nilivyokuwa na waza.Tumeisha waona wapole na wasikivu...wanavyoendesha nchi...tumejua faida zao na hasara zao...sasa tunataka tuwaone ambao ni wakali na si wasikivu linapokuja suala la kufuata sheria....kama hizo sheria wanazijua wao tu watafsri sheria (judiciary) na raia wengine zinawatatiza basi mfumo wa judiciary una matatizo makubwa...unahitaji kufumuliwa ili uweze kutuletea sheria upitia miswada ya sheria inyoeleweka kwa watu wote...maana sheria ni kwa ajili ya watu wote siyo wanasheria tu.
Apite Maghufuli.
Update 12/07/2015
Leo hili limetimia ni kweli aliyepita ni Magufuli, nimezitafakari sababu nilizotajiwa ile siku napewa tetesi hii, na kuzipima na hiki kilichotokea, nimejikuta nimelazimika kutoziamini kuwa zile nilizosikia ndizo sababu zenyewe halisi.
Kwa sisi waandishi tuna kanuni, ukilisikia jambo, kama huliamini, then usiliseme wala kuliandika, hivyo hizo sababu nilisopewa siku hiyo, why Magufuli, siziamini, naomba nisiziseme hivyo chukulie kupitishwa kwa Magufuli kumetokea tuu natural, bila any pre meditated moves, na hili bandiko lichukuliwa tuu kama just a coincidence, nilisema ni Magufuli na akawa coincidentally.
Kwa mtakaonielewa asanteni, kwa msio nielewa samahanini sana!.
Hongera Magufuli!.
Pasco
Mkuu Pasco unaweza kuwa karibu na ukweli halisi hasa ukizingatia harakati za Bwana Pombe mara kaja na daraja la Kigamboni kashalitembelea na kulikagua mara tatu,akaja na swaga nyingine bandari ya nchi kavu Ruvu nikajisemea tangu lini kawa waziri wa uchukuzi kabla hali ya hewa haijakaa sawa katembelea vivuko sijui vya wapi vile nikajisemea huyu si bure nikadhani sasa atatulia kumbe wapi kaja na barabara za juu sijui zinaitwa flyover kazitolea ufafanuzi kwamba foleni Dar itakuwa historia duh.
Mpaka hapo ndugu mwanaJF mwenzangu uhitaji kuambiwa na Pasco huyu ndio mgombea wa CCM hapana tumia akili yako kiduchu utagundua Pombe safari hii kaamua haswa haogopi magazeti ya Rostitamu wala mifedha ya Laigwanani wa Monduli jogoo awike asiwike lazima kutakucha tu.Nafasi ya Pombe safari hii ni wazi kwasababu pia Vasco Dagama asingependa Rais ajae atoke nje ya baraza lake la mawaziri ukitamza baraza lake sasa hakuna waziri anayemkaribia Pombe kwa vituko nasema vituko si kwa bahati mbaya la hasha Bwana Pombe ni waziri wa kukariri barabara na kilometa,ni waziri mropokaji kuliko mawaziri wote wa Vasco labda unaweza kumlinganisha na aliyekuwa katibu mkuu wa CCM Bwana Makamba hana akili hajui aseme nini wapi na wakati gani kwa hakika Tanzania itakuwa na Rais wa hovyo kuliko marais wate tangu tupate uhuru.