Elections 2015 Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli


Pasco wewe si ulikuwa kambi ya mzee wa mafuriko?
 
Pasco wewe si ulikuwa kambi ya mzee wa mafuriko?
Sijawahi kuwemo kwenye kambi ya mgombea yoyote, ila kwenye CCM nilikuwa namkubali sana EL na kumsupport humu jf!, ila kiukweli JPM ni jembe kuliko hata EL!.

Tena nawaombeni msije kunifananisha na Petro aliyemkana Yesu mara tatu kabla jogoo hajawika, mimi sijawahi kuwepo kwenye kambi ya mtu yoyote na sijawahi kupokea senti tano ya mgombea yoyote!.

Pasco
 
Tanzania hapa tulipofika tunamhitaji tulikuwa tunahitaji benevolent dictator, Mungu katupatia a real dictaor!, Tanzania ili tubadilike, na ili tuende, tunahitaji mtu kama Magufuli!, atatawala kwa an iron hand ni heshima na adabu!.

Pasco
 
Mpaka huu uchaguzi uishe Mamvii atakanwa sana, namhurumia sana.
 
Tanzania hapa tulipofika tunamhitaji tulikuwa tunahitaji benevolent dictator, Mungu katupatia a real dictaor!, Tanzania ili tubadilike, na ili tuende, tunahitaji mtu kama Magufuli!, atatawala kwa an iron hand ni heshima na adabu!.

Pasco
Maamuzi ya kukurupuka ndiyo unayaita ya kidikteta?
Mwambie alipie kwanza ile hasara ya bil 40 za samaki aliyotusababishia Watanzania.
 


You can say that again
 
Kidogo nilipata madokezo kama hayo

 
The Boss, wewe mtazamo wako ni upi kwenye mambo yanavyokwenda? Naamini tunamuhitaji mtu atakayebadilisha approach yetu kwenye mambo ya msingi. We need a person like JPM


Mimi naamini hafai
but wengine hawafai zaidi
in the end amekuwa kama 'malaika' mbele ya 'mashetani'

So bora nusu shari tu for now,tusubiri tuone
but aki fail sitashangaa
 
Mimi naamini hafai
but wengine hawafai zaidi
in the end amekuwa kama 'malaika' mbele ya 'mashetani'

So bora nusu shari tu for now,tusubiri tuone
but aki fail sitashangaa

Indeed...katika wale watano, hakukuwa na namna...ni heri nusu shari. Sijui vigezo gani vinatumika, ila ndio hivyo tena.
 
Hahahahaha lol!!!! Sijui siye Watanzania tulimkosea nini Mungu mpaka tupate watu wa ajabu ajabu ambao hawana hata sifa moja ya uongozi kuliongoza Taifa letu.

SABABU NI UVAMIZI WA zANZIBAR NA KUIINGIZA TANGANYIKA CHINI YA MWAVULI WA MUUNGANO FEKI
 
..Magufuli ni mropokaji.

..hana kabisa breki ya mdomo.

..pia inaonekana hajatulia kimawazo, na Uraisi hauhitaji mtu wa namna hiyo.

Mkuu joka kuu, nimetafakari sana capabilities za Magufuli kwenye Urais hasa kwenye kipengele cha mahusiano na majirani zetu.
Magufuli ni kama 'ndugu' wa Raila Odinga ambapo pia Kenya haijatulia 'kivile'. Uganda nayo kuna chokochoko za chini chini, Burundi na Rwanda hali tete, Malawi na sisi bado shughuli ni mbichi, Somalia, Sudan bado wanaweza kuisumbua EA.
Uzoefu unaonyesha Tanzania huwa ni mpatanishi. Ilikuwa hivyo kwa Mwinyi, Ben na sasa Kikwete.
Hawa viongozi watatu walikuwa wana Diplomatic Capabilities. Magufuli kwa historia hana hizo.
Ametoka kufundisha, kagombea ubunge, kapewa uwaziri na sasa anataka kuwa rais. Akiwa rais atakuwa na uwezo wa ku-manage haya mambo?
Mkandara
Pasco
Mag3
Somoche
 
Last edited by a moderator:
Usishangae Mzito Kabwela, CCM inazama na ninavyojua mfa maji hutapatapa na hata majani atajaribu kuyang'ang'ania katika jitihada za kujaribu kujiokoa. Hiyo ndiyo sababu kubwa kwa nini wanamng'ang'ania Magufuli, completely a non starter...heri hata Ben alianza on a clean slate (so we were told), huyu jamaa anaanza na gunia la kashfa, next to nothing diplomacy na hata kuongea tu hajui. Lakini linalosikitisha zaidi ni kwamba huyo aliye msafi CCM hii tunayoijua imtoe wapi?
 
Last edited by a moderator:
Kwa harakaharaka Mh JPM anaonekana ni mtu asiye shaurika kirahisi, na pia asiyeweza kukontrol hasira zake. Hii ni hatari kwa mtu wa namna hii kupewa madaraka ya juu kabisa nchini.
 
Mara nyingi rais huwa na washauri wake wa mambo mbali mbali lakini huchukua maamuzi sahihi baada ya kushauriwa. Hivyo usitegemee kwamba Mwinyi, Mkapa na Kikwete walikuwa wakifanya maamuzi yao wenyewe, zaidi ya hapo Upatanishi ni kipaji kinachotokana na hekima na Busara sio wadhifa ama Elimu .. Na uwezo wa mtu kaitka hili inategema anaheshimika vipi..
 

..hilo la kuwa mpatanishi sidhani kama analiweza.

..lakini kuna suala kubwa zaidi, nalo ni nafasi na maslahi ya Tz ktk EAC.

..raisi wa Tz ajaye lazima awe makini kwamba hachukui maamuzi ambayo yatawaumiza wa-Tz ktk EAC.

..hii jumuiya imekaa kiujanja-ujanja, ambapo kila mwanachama anavutia kwake. sasa Raisi ajaye ni lazima aelewe kinachoendela ktk jumuiya.

cc Geza Ulole, Mkandara, Mag3
 
Magufuli pamoja na utendaji wake kawekwa pale kulinda maslahi ya waliopita! Hilo pekee linaanza kumletea shida na kama fununu tunazozisikia juu ya EL zikiwa kweli, mpambano huu utakuwa mtamuu ile mbaya tatizo CUF wana nia ya kuharibu hizi mbio tena wako radhi kucheza kadi za udini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…