Mgomo Kariakoo: Wafanyabiashara wakutana Mnazi Mmoja

Mgomo Kariakoo: Wafanyabiashara wakutana Mnazi Mmoja

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
70,791
Reaction score
98,334
Baada ya kutangaza kugoma kufungua maduka yao wiki iliyopita, hatimaye Kariakoo ikasimama.

Mkuu wa Mkoa akaenda, akashindwa wafanyabiashara wakamtaka Rais, Ripoti ikatoka kutoka Dodoma kuwa Mkutano utafanyika Dodoma siku ya Alhamis, chini ya Waziri Mkuu, wafanyabiashara wakagoma.

Likatoka tamko kuwa Jumatano watakutana Ofisi ya Waziri Mkuu, wakagoma Waziri Mkuu akaenda Kariakoo, akaongea nao ila hawakuelewana. Jumanne mgomo ukaendelea kama kawaida.

Polisi wakapewa majina ya watu kuwa ndo wanaoshinikiza, watu hao wakaitwa Msimbazi kutoa maelezo.

Leo mkutano ukawa ufanyika kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara na Serikali Anatouglu, wafanyabiashara wakaugomea kwamba hawaamini viongozi wao wanataka wao wenyewe watoe maoni yao.

Pametokea mvutano ila mwisho Serikali imekubali kupeleka Kikao cha Wazi Mnazi Mmoja. Wafanyabiashara wameonesha umoja na wameweza.

Kamwe msikubali maoni yenu yapelekwe kifichoni na watu wachache.
 
Hadi sasa Serikali bado haijafika eneo husika
 
Huyo mwenyekiti kama alichaguliwa na wafanyabishara basi hawezi kuchaguliwa tena
Amesababisha jana watu wakaitwa Msimbazi na Polisi walisema yeye ndo kawataja kuwa wanasababisha wenzao wasifungue maduka
 
Mkutano unaanza uko Live TBC
 
Anaongea Chalamila

Wafanyakazi wengine angalieni na kamwe msiendeshwe na story
 
Amesababisha jana watu wakaitwa Msimbazi na Polisi walisema yeye ndo kawataja kuwa wanasababisha wenzao wasifungue maduka
Mpuuzi sana huyo jamaa yani ni bonge la Yuda
 
Back
Top Bottom