Mgomo Kariakoo: Wafanyabiashara wakutana Mnazi Mmoja

Mgomo Kariakoo: Wafanyabiashara wakutana Mnazi Mmoja

Wafanyabiashara wa kkoo ndio Tanzania yenyewe safi sana mmeonyesha kuwa hilo ndio Jiji na linakaliwa na Watu...
 
Nimempenda mama bonge muuza vipodozi hadi waziri mkuu amecheka naona kampa namba,

Yule alosema Gulio la China lisiwepo sababu Soko la Kariakoo litakufa na watoto wao kukosa biashara miaka ijayo, mwambieni Biashara ushindani
 
Huyo mwenyekiti kama alichaguliwa na wafanyabishara basi hawezi kuchaguliwa tena
Bwana Massawe kawauza wenzake kwa bei nafuu
a570437d316740d980c291732bd59265.jpg
 
Maana serikali Ina vitu vitatu.
Polisi
Mahakama
Magereza.
Ukivikumbuka hivi vitu vitatu, mwenyewe unarudi kwenye mstari.
Bogazi kama nyie ndio mnafanya nchii hii iliwe na watu wachache
 
Baada ya kutangaza kugoma kufungua maduka yao wiki iliyopita, hatimaye Kariakoo ikasimama.

Mkuu wa Mkoa akaenda, akashindwa wafanyabiashara wakamtaka Rais, Ripoti ikatoka kutoka Dodoma kuwa Mkutano utafanyika Dodoma siku ya Alhamis, chini ya Waziri Mkuu, wafanyabiashara wakagoma.

Likatoka tamko kuwa Jumatano watakutana Ofisi ya Waziri Mkuu, wakagoma Waziri Mkuu akaenda Kariakoo, akaongea nao ila hawakuelewana. Jumanne mgomo ukaendelea kama kawaida.

Polisi wakapewa majina ya watu kuwa ndo wanaoshinikiza, watu hao wakaitwa Msimbazi kutoa maelezo.

Leo mkutano ukawa ufanyika kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara na Serikali Anatouglu, wafanyabiashara wakaugomea kwamba hawaamini viongozi wao wanataka wao wenyewe watoe maoni yao.

Pametokea mvutano ila mwisho Serikali imekubali kupeleka Kikao cha Wazi Mnazi Mmoja. Wafanyabiashara wameonesha umoja na wameweza.

Kamwe msikubali maoni yenu yapelekwe kifichoni na watu wachache.
Kunaweza kukawa na kiongozi ambaye ana-engineer kisirisiri mgomo huu kwa ajili ya kumkomoa Mama. Haya mambo siku hizi nayaelewa sana kuliko zamani
 
Pongezi kubwa sana kwa wafanyabiashara kariakoo kwa kumkataa waziri wa fedha hadharani..
 
Ewaaaah mambo yote hadharani, sio mara oooh viongozi wenu watawawakilisha… wakalambishwe asali.
 
Mgomo unaashiria KUWEPO ajenda lakini nyuma ya ajenda hiyo pia ipo ajenda, tusubiri tutaona ninini hiyo ajenda iliyo nyuma ya ajenda ya mgomo ni suala la wakati tu. Na mgomo huo si bure bali ni ghali na gharama yake lazima ilipwe. Na wakuilipa gharama kwa vyovyote lazima apatikane na alipe.
 
Back
Top Bottom