ukweli ni kwamba tunachukua boom hapa auxiliary police kwa sasa. Chenginewe ni swala la walipewa suspension ambapo mi kwa mtazamo wangu ni bora hao watu wakaandika kuomba kurudishwa badala ya kufanya vurugu zisizokuwa na msingi. Ninachoamini kwa matamshi ya JK siku ya Uhuru pale Ikulu kwamba hawatafanya maamuzi kwa shinikizo ni wazi kwamba tutaishia kwenda home kwa nauli tunazopewa na boom la pili ila tukirudi ni njaa mtindo mmoja. Hao kina kijicho wanatudanganya wakati walipiga magoti kuomba msahamaha mbele ya displinary committee na dada nilimhusudu kama mpambanaji yeye kabisa alikana hakuhusika na mapambano yale na kudhiriki kuapia kwamba hata video clips zinazomwonesha yeye kuwa siye yeye kwa hapo alitusaliti. Hivyo ni vyema tuwashauri kupitia DARUSO hata kama hawaitaki wajaribu kujipanga upya ama la chuo kifungwe mpaka watakaporudi ila kwa tahadhari tu ni kwamba suspension ni study days ndiyo zinahesabiwa na siyo likizo.