Tetesi: Mgomo mkubwa wa madereva wanukia, wasafiri jiandaeni

Wakigoma Mkuu wa Mkoa wa dar ataenda kuongea nao na watarudi barabarani....mmesahau mara hii?
 
Naona wangegoma kwa sababu za msingi kama kupewa mikataba ya kazi ambayo itawasaidia kupata bima za afya, pension, kuweza kukopa kama wafanyakazi wengine nk
 
Nimemisskusikia habari za migomo.
na wagome tu.
 
Yaani nisimame kwenye zebra bila ya kuwa na mtu, tunafanyana machizi?
Na hiyo itakuwa ni kinyume cha sheria,
Sheria inataka usimame pale unaposimamishwa(na ma traffic, au kizuizi au zuio), au pale mtu anapovuka kivuko hicho au kama kuna mtu pembeni mwa kivuko anataka kuvuka. Na si vinginevyo.
 
Wagome tu hii barabara ya shinyanga mwanza, mwanza musoma yaani ni tabu tupu haya mayutong ya mchina yanagonga utafikiri yamekata sentaboliti
 
Mbona sababu za kijinga sana.

Sheria inasemaje?

Sababu za kijinga? Mtu akisimama ambapo hakuna mtu anayevuka au anaetaka kuvuka apigwe faini na anaepita watu wamesimama pembeni apigwe faini? sijui tukuulize wewe Nyakuanyakua ndio sheria gani?
 




Kusema ukweli hiki chombo cha usalama barabarani kimekuwa kero na sasa hakijulikani kinafanya kazi gani, kuna mengi ya kujiuliza je haya matamko yanalenga kuwachanganya madereva ili askari wapate kuchukua rushwa kwa wingi zaidi au wanalenga kulinda usalama wa watumiaji wa barabara na vyombo vya moto.

Ukitazama kwa makini, utagundua wengi wa askari wa kikosi hicho wapo kifedha zaidi na siyo kazi, nitatoa mfano mmoja kati ya mingi inayoonekana wazi ambayo vyombo vya uchunguzi vinaweza kufanyia kazi na kuja na majibu.

Ukiwa kwenye bus linaloanza safari kwenye terminal, (mathalani UBT) anakuja askari anatangaza kufunga mikanda, bus linaondoka na abiria waliokaa kwenye viti tu, bus likifika nje linaongeza abiria kama kumi wanakaa kwenye mfuniko wa injini na wengine kusimama mlangoni, bus hilo litakwenda mpaka karibu na mpaka wa Dar na Pwani kabla ya Maili Moja, dereva wa bus atatoa fedha na kumpa kijana (wakala) atangulize kwa askari Maili Moja ili asibughudhiwe kwenye ukaguzi, na kama siku hiyo kuna askari mtata basi abiria hao wanahamishiwa kwenye taxi au bus jingine dogo wanatangulizwa mbele ambako bus litawakuta na kuwapakia tena, bus hilo likifika Ruvu JKT pub kuna askari pale wanapewa chao kisha linaendelea na safari, bus likifika Ruvu darajani abiria wanapakiwa kwenye pikipiki watangulie baada ya mizani ili kukwepa uzito wa bus kusomeka umezidi kwenye mizani, bus litawachukua abiria hao baada ya kuvuka mizani ya vugwaza ambapo hapo napo kuna askari wa kikosi hicho, nadhani napo pale askari na madereva wanajuana kwa vilemba vyao, bus litaendelea na safari mpaka njiapanda ya JK Msolwa, napo askari wanajifanya wanakagua lakini kwa kupita upande wa dereva na kupenda mikono kisha bus linaendelea na safari.

Tunaona waziwazi yanayofanywa na askari wa kikosi hicho na kujiuliza maswali mengi;
Wanafanya kwa maslahi ya kwao binafsi?
Wanatumwa na kiongozi wao kukusanya pesa kwa maslahi ya viongozi?
Au wanacheza igizo kumridhisha Rais kuwa wapo kazini kumbe wana agenda yao?

Binafsi naona askari wengi kwenye hizo check points wapo kibiashara zaidi, naomba Mkuu wa kikosi hicho ajitokeze hadharani aonyeshe mikanda ya usalama wanayojifunga wale abiria wanaokaa juu ya mfuniko wa injini na kusimama mlangoni kwenye mabasi huku askari wake wakiyatazama yanapita wakati askari hao ndiyo waliotangaza kila abiria afunge mikanda ya usalama.
 
Madereva hawajaenda shule?
Hawajui sheria zinasema nini kwenye zebra au alama za barabara?

Waache ujinga,
 
Barabarani hakuna amani aisee ni kero si kwa madereva wa mabasi tu kuendesha gari imekua kama jinai... Askari wametapakaa pote tena wanasubiria
 
Daah mgomo usikieni tu
Niliwahi kusafiri saa tisa mchana huku presha ya je gari nililokata tiketi ntapata
 
hii point sana ama kwa hakika unasafiri mara kwa mara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…