Mgomo wa Daladala Arusha, Dereva Daladala wailalamikia LATRA, wadai haiwatendei haki

Mgomo wa Daladala Arusha, Dereva Daladala wailalamikia LATRA, wadai haiwatendei haki

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polis (ACP)Zauda Mohamed, amewaomba wamiliki na madereva wa vyombo vya moto vinavyotoa huduma za usafirishaji maarufu kama “daladala” mkoani humo kukaa pamoja na mamlaka husika, ikiwemo Jeshi la Polisi, ili kutafuta suluhisho la mgomo huo na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Hatua hiyo imekuja baada ya watoa huduma hao Jijini Arusha mapema leo kugoma kutoa huduma, wakidai kutokupewa taarifa za faini wanazotozwa na LATRA, mamlaka inayosimamia udhibiti wa usafiri wa ardhini.

Kwa upande wake, kiongozi kutoka LATRA amewaomba viongozi wa madereva hao kukaa pamoja na mamlaka hiyo ili kujadili changamoto zao walizonazo ili kwa pamoja kutafuta suluhisho la kudumu kwa changamoto hizo.
 
Wanawapiga, yaani Kwa hizi daladala Kila wakipita Kila siku lazima waache buku, Piga hesabu daladala ngapi zinapita, hao ni Trafki Tu bado hao mamlaka nyingine.
 
Hivi Hawa mbunge wao yupo wapi?
Bado yupo na filamu ya rio?
 
Safi acha latra wafanye hyo kazi ya kubeba abiria sasa
Komaeni hivyo hivyo mpaka kieleweke

Ova
 
Back
Top Bottom