Mgomo wa Daladala wamalizika Arusha, usafiri warejea kama kawaida

Mgomo wa Daladala wamalizika Arusha, usafiri warejea kama kawaida

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Baada ya mvutano wa siku mbili hatimaye usafiri wa Daladala Mkoani Arusha umerejea kama kawaida leo Jumatano Agosti 16, 2023.

Afisa Mfawidhi wa LATRA, Joseph Michael amesema “Kilichozingatiwa ni Sera, tumewapangia vituo vipya watu wa Bajaj, tunawaondoa mjini kuwapeleka pembeni na wamekubali hilo.”

Naye, Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Bajaji Arusha, Shafii Ramadhani amesema “Baaada ya kikao cha Agosti 15, 2023 kati ya Viongozi wa Umoja wa Bajaji, LATRA na Jeshi la Polisi tumefikia uamuzi mzuri.

“Kamati imeafikiana juu ya upangwaji wa vituo, tumefanya zoezi la kugawa Bajaji ambazo zinatakiwa kukaa kwenye vituo husika, tunashirikiana na Jeshi la Polisi na LATRA, kilichobaki kwa sasa ni nguvu kubwa kuelekezwa kwenye utekelezaji, kilichobaki ni Serikali kutoa maelekezo rasmi ya mgawanyo ndani ya wiki moja kutoka sasa.

“Pia Bajaji ambazo itapata mgawanyo wa vituo ni zile ambazo zimekidhi vigezo vya Leseni na zipo hai.”

2d066635-9537-4f53-a1cb-95f1544e8834.jpg

Hali ilivyokuwa wakati wa mgomo Agosti 14, 2023

Pia Soma: Arusha: Daladala zagoma tena Arusha, leo Agosti 14, 2023
 
Wana bahati sio Mimi ninaetoa mamlaka maana hata nisingetoa tamko lolote. Hoja yao haina mashiko kabisa, Wana uselfish Sana. Wangebanana wote kila sehemu kila mmoja apate riziki yake.
 
Bajaji walitakiwa wawe na vituo vyao maalum,wakae tofaoti na mabasi

Ova
 
Back
Top Bottom