Mgomo wa Madereva na Wafanyakazi wa mabasi wafanya mgomo Morogoro na Dar

Mgomo wa Madereva na Wafanyakazi wa mabasi wafanya mgomo Morogoro na Dar

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Hali ilivyo Mbezi, Dar Es Salaam kwenye Stendi Kuu ya Mabus ambapo inaripotiwa kwa taarifa za awali kuwa kuna mgomo wa Madereva wa Mabus wakigomea kukatwa alama kwenye Leseni zao hivyo wamegoma kuanza safari hii leo.

Hapa ni stendi ya Nane Nane, Dodoma, hali ilivyo asubuhi ya leo baada ya mgomo wa mabasi.




Hali ya mgomo wa madereva na wafanyakazi wa mabasi imeendelea kushuhudiwa katika Kituo cha Mabasi Msamvu mkoani Morogoro, huku ITV ikikuta mabasi yaliyopangwa kuanza safari saa 12:00 kwenda mikoa mbalimbali yakiwa hayapakii abiria.

Mabasi yanayoonekana kuondoka kituoni ni yale yaliyowasili kutoka safari za masafa marefu na yanayomaliza safari katika kituo hicho.

Soma pia: Madereva Mwanza watishia kusitisha huduma kuanzia Septemba 29, 2026

Baadhi ya madereva na wafanyakazi waliokutwa kituoni wamekataa kuzungumza, huku waliozungumza kwa masharti ya kutorekodiwa wakisema wamelazimika kuwaruhusu abiria waliokuwa wanatarajia kuanza safari Msamvu kurejea nyumbani, kwa hofu ya magari yao kushambuliwa endapo wangeendelea na safari.

Wanasema wao ndio wenye dhamana ya magari hayo na usalama wao pamoja na mali walizokabidhiwa.

Madai makubwa ya madereva yanahusu faini wanazodai kutozwa na askari wa Usalama Barabarani, ambazo kwa baadhi ya makosa zinaweza kufikia hadi shilingi milioni moja kwa dereva, pamoja na hatua za kusimamishwa leseni kwa muda, kupunguziwa pointi na hatimaye kupokonywa leseni.

Madereva hao wanasema baada ya kurejeshewa leseni, baadhi yao hutakiwa kurejea shuleni kabla ya kuruhusiwa kuendelea kuendesha, hali wanayodai kuwaathiri kiuchumi kwa kuwa bila leseni hawawezi kutambulika kazini na wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa familia.

Madereva hao pia wanadai kuwa hata wale wanaoendesha mabasi ya masafa marefu wamekuwa wakisafiri kwa tahadhari, wakizingatia usalama wao, abiria na magari. Wamesema endapo hakuna uhakika wa usalama, wako tayari kusimamisha magari na kusubiri maamuzi ya uongozi wao baada ya kukutana na mamlaka husika katika vikao vinavyotarajiwa kujadili changamoto hizo.

Pia soma: Jeshi la Polisi limetoa onyo kali kwa mtu yeyote au kikundi kinachojihusisha na vitendo vya kuzuia mabasi na malori kuendelea na safari zao
 
Huu mgomo ulipaswa kuwashirikisha hata madereva binafsi

Hata ukiwa unaendesha private car, bado utakatwa alama kwenye leseni yako ukikutwa na kosa

Ni kama njia ya kulazimisha rushwa kwa askari, maana Kila ukikutwa na kosa unakatwa alama kwenye leseni yako 🙌
 
Back
Top Bottom