sheria zinazolalamikiwa kimsingi zinagusa madereva wote.
ila kama kawaida nchi yetu focus kubwa inamulikwa kwa trucks na mabasi.
mimi nakubaliana na wewe yote isipokua kumkinga dereva.
madereva wengi kanuni hawazingatii ,
jambo tv hapa clip hii wamehoji madereva wawili, wasikilize alafu tuangalie wao kama madereva wanafahamu taratibu za kazi yao.
dereva anasema mwenye mamlaka ya kufunga leseni ni mahakama tu, huyu kasoma wapi sheria ya barabarani, hajafundishwa kuna mazingira afisa polisi kuanzia ngazi ya ASP kwenda juu anaweza mfungia leseni
View: https://www.youtube.com/watch?v=R2dF9nnawNI
mjadala huu sio mwepesi namna hiyo na unakua mzito zaidi kwa dereva kwakua yeye muda wote anatakiwa kufuata sheria iliyowekwa