Ninasikitishwa na kadhia ya mgomo wa madereva wa mabasi wanaoshinikiza eti wasikatwe pointi kwenye leseni zao wanapofanya makosa.
Pamoja na hayo kuna mmoja nimemsikia akisema eti wanatozwa faini hata mara tatu ya kosa la kuzidisha mwendo na kwa hiyo anaona alistahili kuipa mara moja hata kama amerudia kosa hilo baada ya kulipishwa faini.
Huu ni upuuzi mkubwa kwani sheria hizi zimelenga kupunguza ajali kwa kuwafanya madereva wawe makini wanapokuwa barabarani.
Mamlaka hazipaswi kuwachekea hawa watu kwani wengi wao hawajali usalama wa abiria wao,bali wanachojali ni ushindani wa spidi na sifa za kijinga tu barabarani.
Wanaonesha dharau sana kwamba hadi aende waziri mkuu au makamu ndipo wasikilize.Huu ni uhalifu kama uhalifu mwingine.Wote wanaochochea wakamatwe na kuchukuliwa hatua kali sana.