Naweza kusema kwamba, tunahatua kubwa sana kujifunza kutoka kwa majirani zetu Kenya! Kodi na ama ongezeko lolote la kikodi litokanazo na bidhaa, humlenga moja kwa moja mlaji na siyo mfanya biashara!
Kwa upande mwingine, maandamano ya majirani zetu, ni sahihi na siyo haya ya wafanyabiashara wa Kariakoo!
Kwa kawaida, mfanyabiashara huwa halipi kodi! Kwa sababu, asipouza hawezi kudaiwa kodi
Anapouza ndio hulazimika kulipa kodi, maana yake, anayekuja kununua ndiye anayelipa kodi zote, na mfanyabiashara kazi yake ni kupeleka kodi iliyotokana na njaa ya mlaji, kazi ya mfanyabishara, hufanya hesabu kabla ya kuanza kuuza bidhaa zake ili apate ya kodi ya pango, TRA, na gharama zoote ili abakiwe na faida yake
Nadhani hesabu zinawavuruga hawa wafanyabiashara, badala ya kukaa, kisha kuona ni kwanamna ipi itawalazimu kuongeza bei kwenye kila bidhaa ili wao wabaki na faida zao na maumivu ya kodi hizo anabaki nazo mlaji wao wanaweka mgomo, huo mgomo hauwahusu hata chembe
Huo mgomo iliwapasa watumia bidhaa (Walaji) ndiyo waandamane na ama kugomaa kula ili iwe sawa siyo kwa mfanyabishara kugoma, huo ni upuuzi na kuchelewesha wajinga kupata akili, wananchi wakionja joto ya jiwe ndo wataamua wao kugoma na ama wavumilie maumivu ya sera mbovu za viongozi wao!
Nikimuuliza mfanya biashara anachogomea ni kipi, hana jibu kulingana na kwamba, yeye ni wakili tu wa serikali kuwasilisha kodi kwauaminifu kutoka kwa watumiaji bidhaa
Fungueni maduka na mpandishe bidhaa ili kama yupo wa kuandamana, aandamane mwananchi mtumiaji bidhaa
Uko sahihi sana ndugu
Nsanzagee, kwamba walichopaswa kufanya wafanyabiashara ni kuongeza tu bei ya bidhaa na huduma zao Ili mlaji wa mwisho (mwananchi) ndiye aumie kisawasawa ili kama akitambua kuwa anaumia ndiyo sasa achukue hatua dhidi ya watunga sera na serikali yao kwa kuansamana na kugoma kama wanavyofanya Kenya sasa.
Lakini Mimi nadhani hawa wafanyabiashara wana kitu kingine zaidi ya hiki unachofikiri wewe (kuwa ni wajinga tu). Hapana si wajinga. Wako sahihi na wanajua wakifanyacho.
Aidha, ukumbuke kuwa nao ni wananchi.
Ukiachilia mbali kazi yao ya biashara, lakini pia wanahitaji huduma zingine muhimu kama elimu, barabara, huduma bora na nafuu za afya, usafiri na usafirishaji, mawasiliano, maji safi na salama, mazingira bora na salama ya kuishi, amani na usalama nk
Kugoma kwao si tu kwamba kunahusu biashara zao. Kunatuhusu hata sisi wateja wao, walaji wa mwisho wa huduma zao wanazotupa
Wewe unafikiri wafanyabiashara wanajisikiaje iwapo wanalipa kodi, ushuru na tozo nyingi ambazo wanaona kabisa kuwa zinaenda kwenye mifuko ya viongozi wa umma wachache na kutajirika pasipo kutoa jasho na wakati huo huo huduma za kijamii kama nilivyozitaja hapo zikiwa duni na za hovyo?
Unadhani hao wafanyabiashara hawahitaji maji? Umeme wa uhakika? Elimu bora kwa ajili ya watoto wao? Barabara bora kwa ajili kupita na magari yao?
Wewe unadhani wanajisikiaje kuwaona watu tuliowaamini kama viongozi waadilifu kugeuka kuwa wezi na mafisadi waliokubuhu kwa fedha za umma zinazolipwa kama kodi, tozo na ushuru mbalimbali Ili kutoa huduma bora kwa watu wote?
Mfano ni hili skendo la ufisadi wa sukari ambalo viongozi wetu wachache wakiongizwa na waziri wa sekta ya Kilimo (Hussein Mohamed Bashe), yule wa fedha (Mwigulu Lameck Nchemba) na Bodi ya Sukari Tanzania kushirikiana na baadhi ya kampuni za wafanyabiashara wachache mafisadi na wezi kuiba au kuihujumu mapato ya nchi zaidi ya TZS 700bn huku wabunge (wawakilishi wa wananchi) nao wakihongwa Ili kufunika wizi na ufisadi huo.
Wewe unafikiri wanajisikiaje hawa wafanyabiashara? Yaani wao wabanwe kulipa Kodi kubwakubwa huku wenzao wachache wajanja wajanja wakipewa misamaha kinyume kabisa cha sheria na utaratibu?
Kwa hiyo: HAPANA wala sio wajinga na wala sio wapumbavu kwa kuchukua maamuzi ya kugoma. Wameanza wao na sisi wananchi tunatakiwa kuwaunga mkono badala ya kuwatukana na kuwataja wapandishe bei ya bidhaa na huduma zao.
Shida iko kwako wewe
Nsanzagee na wananchi wenzako!!