Mgomo wa wafanya biashara ni wa kipuuzi kuwahi kutokea! Wao inawahusu nini mlaji akipandishiwa bei bidhaa? Wao ni wapeleka kodi tu anayelipa ni mlaji

Huna biashara unafanya

unalelewa na shemejio anayefanyakazi za umbea hapo Lumumba alafu unakuja hapa kubwa waja upuuzi
 
Sasa Ulipelekwa Shule kwa Kodi Zetu halafu hukuelimika kweli?

VAT inatakiwa iwe na Baseline!

Malalamiko ya Wafanyabiashara wa Kariakoo ni kwamba sehemu ya Importation ya Bidhaa haitozwi kodi ipasavyo kule Bandarini..

Unaingiza mzigo Mkubwa lakini unalipia VAT kidogo!

Kuna gap...

Na dhamira ya Wafanyabiashara ni kulipa Kodi Serikalini na siyo kama ulivyoelewa wewe!


Sasa huku kwenye kuuza uta-Claim vipi ile deposit yako?

Halafu Mlaji ni Lazima awe na Uwiano wa Bei na Masoko ya Jirani,Dunia kwa sasa ni Kijiji kwa hivo ni Lazima utizame kwenye angle hizo!

Pata Elimu kwanza!
 
Kenya wanachofanya unawaunga mkono jinsi wanavyopora maduka ya watu na Hadi vyakula vya mama nitilie
Biashara zimefungwa na Bado wanavunja milango ya maduka na kupora
Kwanini serikali ilisubiri mpaka wananchi wachukue hatua hiyo Ili kujitetea na sera mbovu za serikali?

Njia hiyo (ya watu kuingia barabarani) kudai haki zao mbalimbali siku zote sio salama wala njema. Njia hii huambatana na uharibifu wa mali na mara nyingi umwagaji wa damu. Watu wenye hasira hawezi kuwa na ustaarabu unafikiri wewe!

Hupaswi kuwalaumu wananchi. Ni serikali za kidunia ndizo zinapaswa kulaumiwa kwa kuendekeza sera mbaya zisizoungwa mkono na wananchi

Mfano hapa kwetu Tanzania ni skendo ya ufisadi kwenye ishu ya Sukari inayowahusu baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali kuisha kwa namna ile huku wananchi tukidanganywa waziwazi mchana kweupe kana kwamba sisi ni wajinga fulani hivi

Kwa hiyo, ukitaka kuepuka njia hiyo, uwajibikaji wa kutenda haki ndilo Jibu lako!!
 
Kwa muandiko huu naona kama uko ulaya vile
Haujui kabisa kodi na mashine uchwara hizo
Ukitoa receipt kwa kila mteja mwisho wa siku watakuambia ulipe mamilioni huo ni wizi

18% kwa Bara na 15% visiwani ni nyingi mno
 
Kauze njegele za Bibi yako huna unalojua.
 
Si kweli ungea kikodi zaidi.mlaji wa mwisho ndio anayebeba mzigo wa kodi na mfanyabiashara ni wakala tu wa hizo kodi sasa inakuwaje kwamba inapunguza uwezo wa mfanyabiashara kununua?hiyo ni principle gani ya kodi?
Jamaa kaongea vizuri sana na mimi nimemuelewa sana
Mfano siyo kila bidhaa iliyopo kkoo inatoka china mimi nanunua rasta kiwandani ambapo kiwanda kinanichukulia mimi kama mlaji kwa hiyo kitanibebesha huo mzigo wa kodi anaosema mtoa hoja
Kkoo mimi pia nawauzia wafanyabishara wanaoenda klkuuza kwa walaji wengine kwa hiyo mimi siyo mlaji wa mwisho
Kwa mnyororo huo mtoa hoja anamuongelea nani wa kubebeshwa huo mzigo
 
Unapakatwa ww
 
Mauzo yakishuka maana yake kuna mtu hataweza kula, kuvaa, kujenga na kushindwa kabisa kujikimu kimaisha, na hapo ndipo kutakapotokea hasira za wananchi kudai haki zao

Wao wafanyabishara inawahusu nini maumivu ya walaji?


..mfanyabiashara wa bidhaa A, ni mlaji wa bidhaa B,C,D, etc etc.

..lakini hata hiyo bidhaa A anayoiuza huenda na yeye pia ni mlaji. Kwa mfano mtu akiwa mfanyabiashara wa simu janja, iko siku na yeye atalazimika kununua kwa mahitaji yake, au ya wanaomtegemea.

..
 
Inaelekea wewe hujawahi kuuza kitu chochote, kwa muuzaji makini bei ya kumuuzia mnunuzi inamhusu. Bei uliyopanga ni muhimu kwa kuwa ndio itakayoamua utauza vitu vingapi ( vingi au kidogo). Ukiuza vingi utapata faida kubwa . Ukiuza kidogo faida nayo itakuwa ndogo. Vile vile huwezi kupandisha bei kama unavyotaka - utakosa wanunuzi. Kila mwezi lazima uuze ili ulipie kodi ya jengo, mishahara ya wafanyakazi , na Kodi uliyokadiriwa na TRA wakati unakata leseni ya biashara. Biashara ni ngumu- waache watafute muafaka na TRA.
 
Mkuu upo sahihi tu wala hujakosea! Mimi nataka maisha hayo magumu yawapige sana walala hoi, wasipokula na hao wafanyabiashara wasipouza, ndio joto sasa la mgomo nchi nzima linafuata na heshima inakuja
 
Mawazo ya kipumbavu sana. Wafanyabiashara wao hawali, hawavai...? Jinga sana wewe.
 
Mawazo ya kipumbavu sana. Wafanyabiashara wao hawali, hawavai...? Jinga sana wewe.
Tehe tehe!

Punguza jaziba mkuu, kwa akili yako unadhani hao wafanyabishara wanakusaidia wewe uliyejificha nyuma ya keebodi huku ukidhani wewe isipoandamana mambo yatabadirika

Chukua hatua acha ujinga
 
Tehe tehe!

Punguza jaziba mkuu, kwa akili yako unadhani hao wafanyabishara wanakusaidia wewe uliyejificha nyuma ya keebodi huku ukidhani wewe isipoandamana mambo yatabadirika

Chukua hatua acha ujinga
Jaziba, yatabadirika. Duh, jifunze kuandika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…