Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024
Wafanyabiashara hawakatai kulipa kodi
Changamoto ni utitiri wa kodi kwenye biashara, Makadirio ya kodi yasio na uhalisia naweza kuuza laki moja ila faida ni 1000/=
 
Kama uko timamu, hutakiwi kua serious ati ujibu kwa hoja kwenye huu uzi wa kijana wa buku mbili.
 
1. Mnataka kufanya biashara bila kulipa kodi? Uliona wapi?

2. Viongozi wa mgomo wakamatwe na kufikishwa mahakamani Kwa kosa la uhujumu uchumi.

Cc: Mama Sinyarah kimamnbo
Kwani ni kina nani wamefunga biashara kisa hawataki kulipa kodi? Hivi ukiitwa wewe ni mpumbavu utakataa?
 
Kodi si ombi. Kama umechoka biashara achia wengine wafanye hizo biashara. Mazingira Ni wezeshi hapo kariakoo. Acheni kusumbua Viongozi

Tatizo ni TRA rushwa kila mahali. Hivi ni kwanini kuna makadirio ya kodi ya vitu kutoka nje badala ya kuweka kodi elekezi . Ukadiriaji wa kodi ndiyo tatizo
 
Nauunga mkono, ni kweli,
Hao wachuuzi na viduka vyao, wanaingiza sana mizigo kimagumashi, bila kodi, mzigo unakuja kama wa Zambia, sababu nashangaa, siku hizi kumekuwa na mizigo mingi ya magari makubwa kwenda Zambia kwenye malori yangu.
halafu ukifika kule unarudishwa nusunusu, wakati zamani kwenda Zambia malori ilikuwa ni malori ya mafuta.
 
Unawazuia wageni wasifanye biashara ili iweje?
Napata sana shaka na uelewa wako wa mambo,hivi wewe unaposikia biashara ndogo ndogo akilini mwako inakujia picha gani?

Mchina akiwa amekodi ground floor ya ghorofa fulani hapo mjini au amekodi warehouse kule Chang’ombe na kujaza mali akiuza makatoni kwa makatoni kwa wazawa au mchina amekodi frame moja ya 10x10 kama anayokodi Mkinga pale Kariakoo na kupanga sample huku akiuzia godwon?unataka kubishana kwa sababu ni hulka yako au unataka kueleweshwa?
 
Huo msururu wa kodi mnaotaka ufutwe mnataka kufanya biashara bila kulipa kodi? Kuna kundi kubwa la walipa kodi mfano watumishi wa umma na sekta binafsi kila mwezi wanakatwa PAYE wafanyabisha wao ni nani hadi wapunguziwe kodi zote hizo ? Na bado ukwepaji kodi ni mkubwa tu tunajua risiti hazitolewi na pia kufanyiwa makadirio madogo ya hesabu za biashara mnadhani serikali haijui?
Huyo mfanyakazi wa serikali analipa licence gani kila mwaka?service levy analipa huyo mfanyakazi kila baada ya miezi mitatu?unalipa fire wewe?unamlipia kodi ya jengo huyo aliyekuajiri hapo?

Lini umekutana na changamoto yoyote ya kubambikiwa kodi ukijua kabisa ulishailipa na ushahidi unao lakini unaambiwa uilipe?vitu huvielewi vyema ukakaa kimya!
 
Kodi zilipwe ila tujifunze kuwaheshimu wafanyabiashara. Tena tuwaheshimu sana, wanachofanya kwenye sekta ya fedha ni uzalendo.

Hizo PAYE ulizozitaja nani anazikusanya? Anayefanya hiyo kazi analipwa nini? Anatumia gharama za nani kuhakikisha zimefika sehemu husika? Mfanyanyakazi ukipewa pesa yako yote upeleke PAYE serikalini mwenyewe utakuwa mwaminifu?

Vipi mteja unayelipa VAT? Ukipewa jukumu la kila unachonunua uchukue 18%VAT uipeleke kwenye akaunti ya serikali kila tarehe 20 utakuwa mwaminifu kuipeleka?

Kama unataka kuwaweka mfanyabiashara chungu kimoja na mwajiriwa futa majukumu yake ya ziada chukua kodi yako kama unavyochukua kwa mfanyakazi. Mfanyakazi akishalipa PAYE si unaachana nae? Fanya hivyo kwa mfanyabiashara.

Otherwise Jifunze kuheshimu nafasi yake.
 
Watumishi wote siyo wa serikali tu hata wa binafsi hawana ujanja wa kukwepa kodi kila mwezi lazima akatwe kwenye mshahara wake. Wafanyabiashara wengi nchi hii hasa hapo kariakoo ni wakwepaji wakubwa wa kodi lakini serikali inakuja na dawa ya kudumu kuhusu hili suala.
 
Kila mwananchi amuheshimu mwenzake awe ni mfanyakazi au mfanyabiashara isitokee mlipaji mmoja ajione yeye ni bora sana kuliko mwenzie
 
Watumishi wote siyo wa serikali tu hata wa binafsi hawana ujanja wa kukwepa kodi kila mwezi lazima akatwe kwenye mshahara wake. Wafanyabiashara wengi nchi hii hasa hapo kariakoo ni wakwepaji wakubwa wa kodi lakini serikali inakuja na dawa ya kudumu kuhusu hili suala.
Then tusubiri tuone.
 
Napata sana shaka na uelewa wako wa mambo,hivi wewe unaposikia biashara ndogo ndogo akilini mwako inakujia picha gani?

Mchina akiwa amekodi ground floor ya ghorofa fulani hapo mjini au amekodi warehouse kule Chang’ombe na kujaza mali akiuza makatoni kwa makatoni kwa wazawa au mchina amekodi frame moja ya 10x10 kama anayokodi Mkinga pale Kariakoo na kupanga sample huku akiuzia godwon?unataka kubishana kwa sababu ni hulka yako au unataka kueleweshwa?
Biashara ni ushindani na ubunifu acheni kulialia
 
Mi sijawahi kuwatakia mema wafanyabiashara wa k/koo, kwasababu wengi wao wanatuibia sisi tusiofahamu bei za baadhi ya bidhaa.
 
Back
Top Bottom