Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024
Uncle kashindwa kutafuta muhasibu akampa 2m akomae na TRA yeye aendelee na mambo yake ?mimi kwenye biashara yangu wananijua ni sheria kwa sheria ,utaalamu kwa utalaamu hawalambi hata 100 kila kitu kimenyooka.Sisi ndio wale wachache tuna enjoy VAT returns wengine kwa kutokujua na ubahili wanajua ni siasa za TRA ,ukiwa na mtaji wa 200m + usicheke na TRA na mahesabu , tafuta dogo mwenye CPA anayejua alichoisomea akakomae na TRA.
Mwezi uliopita walininyima tax clearance eti wananidai 300m malimbikizo tangu 2016 wakati kila mwaka napeleka hesabu zilizokaguliwa na wanapitisha kama faini nalipa na miaka yote sijawahi kunyimwa tax clearance. To cut the story short niliwapa documents za kila walichokuwa wanasema sijalipa na niliishia kuwalipa 950,000/- ndio deni. Hiki ulichosema ndio utaratibu mzuri hata mimi niliwaachia mhasibu wadili nae nilimwambia sitaenda tra kwasababu hakuna deni hapa.
 
Jana nilikuwa huko Kariakoo.
Kuna mgawanyiko baina ya Wafanyabishara.
Wapo watakaofungua na wapo watakaofungua.

Nilisikia Machinga wakisema wao sio wafanyabiashara. Wao wana umoja wao hivyo wao watafungua.

Wamachinga ni wale wenye vimeza wanaokaa na kuziba njia
Machinga hana ubavu wa kufungua biashara
Kibarua hawezi kushindana na boss wake
 
Hadi Sasa ni saa 2:24 asubuhi maduka mengi hayajafunguliwa.


Licha ya Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila, kuwasisitiza Wafanyabiashara wa Kariakoo kuendelea na shughuli zao kama kawaida, hadi Saa 9 Asubuhi Wafanyabiashara wengi wamefunga Biashara zao katika Mitaa ya Kariakoo, leo Juni 24, 2024

Awali, Chalamila akizungumzia taarifa za mgomo wa Wafanyabiashara wa #Kariakoo alisema "Yawezekana Wafanyabiashara wana Malalamiko ya dhati kabisa lakini Masuala ya mgomo yasichukuliwe kuwa ni jambo la pamoja."

Taarifa ya mgomo ilianza kusambaa kupitia vipeperushi ambavyo havikuwa na jina la Mwandishi, Juni 22, 2024 na sababu zilizotajwa ni kupinga masuala ya Kodi Kandamizi.

========
Pia, soma

Wafanyi biashara hongereni sana,sikudhani hata siku moja kwamba mtanzania anaweza kufanya hili.Tumechelewa sana.Hata lini tutaneemesha watu wachache, huku wengine tukizama katika lindi la umaskini.Lazima tufike mahali katika umoja wetu tuseme inatosha,na nadhani wakati huo ni sasa.Kazi hii tusiwaachie wafanyabiashara peke yao,tuwaunge mkono.
 
Wafanyi biashara hongereni sana,sikudhani hata siku moja kwamba mtanzania anaweza kufanya hili.Tumechelewa sana.Hata lini tutaneemesha watu wachache, huku wengine tukizama katika lindi la umaskini.Lazima tufike mahali katika umoja wetu tuseme inatosha,na nadhani wakati huo ni sasa.Kazi hii tusiwaachie wafanyabiashara peke yao,tuwaunge mkono.
Mapandikizi yakiongozwa na wasanii, wafanyabishara chawa kama akina mume wa jooo ndio vviongozi na wanakwamisha uhuru wa wafanyi biashara.
 
Mengine yana hoja mengine ni upuuzi kwamfano hiyo No.12
Unaweza ukafafanua inakuwaje upuuzi nikakuelewa?

Kwa sababu Kariakoo pale mchina aliyetakiwa alete mzigo mkubwa auzie godown amlishe mzawa mwenye frame kwa bei za jumla ili apate afadhali ndiyo kwanza amekodi frem pembeni yake anamkimbiza kwa bei za store,kama haupo kwenye hii industry huwezi elewa kitu na ndicho kinachotusibu kuwa na viongozi wabovu mandondocha wasioelewa mambo mfano wako wewe
 
Kodi si ombi. Kama umechoka biashara achia wengine wafanye hizo biashara. Mazingira Ni wezeshi hapo kariakoo. Acheni kusumbua Viongozi
Nani amekudangsnya kuwa wafanyabiashara wa kariakoo hawalipi Kodi?

Mbona Kariakoo ndio sehemu ambayo TRA inakusanya Kodi nyingi Kwa wafanyabiashara kuliko sehemu nyingine yoyote katika nchi hii

Mkishashiba ugali wa Bure Kwa shemeji zenu mnakuwa kama mandezi
 
Back
Top Bottom