azithromycim
JF-Expert Member
- Apr 18, 2019
- 288
- 714
Ulishawahi kumiliki biashara?Kodi si ombi. Kama umechoka biashara achia wengine wafanye hizo biashara. Mazingira Ni wezeshi hapo kariakoo. Acheni kusumbua Viongozi
Kwani ni kina nani wamefunga biashara kisa hawataki kulipa kodi? Hivi ukiitwa wewe ni mpumbavu utakataa?1. Mnataka kufanya biashara bila kulipa kodi? Uliona wapi?
2. Viongozi wa mgomo wakamatwe na kufikishwa mahakamani Kwa kosa la uhujumu uchumi.
Cc: Mama Sinyarah kimamnbo
Kodi si ombi. Kama umechoka biashara achia wengine wafanye hizo biashara. Mazingira Ni wezeshi hapo kariakoo. Acheni kusumbua Viongozi
Napata sana shaka na uelewa wako wa mambo,hivi wewe unaposikia biashara ndogo ndogo akilini mwako inakujia picha gani?Unawazuia wageni wasifanye biashara ili iweje?
Huyo mfanyakazi wa serikali analipa licence gani kila mwaka?service levy analipa huyo mfanyakazi kila baada ya miezi mitatu?unalipa fire wewe?unamlipia kodi ya jengo huyo aliyekuajiri hapo?Huo msururu wa kodi mnaotaka ufutwe mnataka kufanya biashara bila kulipa kodi? Kuna kundi kubwa la walipa kodi mfano watumishi wa umma na sekta binafsi kila mwezi wanakatwa PAYE wafanyabisha wao ni nani hadi wapunguziwe kodi zote hizo ? Na bado ukwepaji kodi ni mkubwa tu tunajua risiti hazitolewi na pia kufanyiwa makadirio madogo ya hesabu za biashara mnadhani serikali haijui?
Kodi zilipwe ila tujifunze kuwaheshimu wafanyabiashara. Tena tuwaheshimu sana, wanachofanya kwenye sekta ya fedha ni uzalendo.Huo msururu wa kodi mnaotaka ufutwe mnataka kufanya biashara bila kulipa kodi? Kuna kundi kubwa la walipa kodi mfano watumishi wa umma na sekta binafsi kila mwezi wanakatwa PAYE wafanyabisha wao ni nani hadi wapunguziwe kodi zote hizo ? Na bado ukwepaji kodi ni mkubwa tu tunajua risiti hazitolewi na pia kufanyiwa makadirio madogo ya hesabu za biashara mnadhani serikali haijui?
Watumishi wote siyo wa serikali tu hata wa binafsi hawana ujanja wa kukwepa kodi kila mwezi lazima akatwe kwenye mshahara wake. Wafanyabiashara wengi nchi hii hasa hapo kariakoo ni wakwepaji wakubwa wa kodi lakini serikali inakuja na dawa ya kudumu kuhusu hili suala.Huyo mfanyakazi wa serikali analipa licence gani kila mwaka?service levy analipa huyo mfanyakazi kila baada ya miezi mitatu?unalipa fire wewe?unamlipia kodi ya jengo huyo aliyekuajiri hapo?
Lini umekutana na changamoto yoyote ya kubambikiwa kodi ukijua kabisa ulishailipa na ushahidi unao lakini unaambiwa uilipe?vitu huvielewi vyema ukakaa kimya!
Kila mwananchi amuheshimu mwenzake awe ni mfanyakazi au mfanyabiashara isitokee mlipaji mmoja ajione yeye ni bora sana kuliko mwenzieKodi zilipwe ila tujifunze kuwaheshimu wafanyabiashara. Tena tuwaheshimu sana, wanachofanya kwenye sekta ya fedha ni uzalendo.
Hizo PAYE ulizozitaja nani anazikusanya? Anayefanya hiyo kazi analipwa nini? Anatumia gharama za nani kuhakikisha zimefika sehemu husika? Mfanyanyakazi ukipewa pesa yako yote upeleke PAYE serikalini mwenyewe utakuwa mwaminifu?
Vipi mteja unayelipa VAT? Ukipewa jukumu la kila unachonunua uchukue 18%VAT uipeleke kwenye akaunti ya serikali kila tarehe 20 utakuwa mwaminifu kuipeleka?
Kama unataka kuwaweka mfanyabiashara chungu kimoja na mwajiriwa futa majukumu yake ya ziada chukua kodi yako kama unavyochukua kwa mfanyakazi. Mfanyakazi akishalipa PAYE si unaachana nae? Fanya hivyo kwa mfanyabiashara.
Otherwise Jifunze kuheshimu nafasi yake.
Then tusubiri tuone.Watumishi wote siyo wa serikali tu hata wa binafsi hawana ujanja wa kukwepa kodi kila mwezi lazima akatwe kwenye mshahara wake. Wafanyabiashara wengi nchi hii hasa hapo kariakoo ni wakwepaji wakubwa wa kodi lakini serikali inakuja na dawa ya kudumu kuhusu hili suala.
Biashara ni ushindani na ubunifu acheni kulialiaNapata sana shaka na uelewa wako wa mambo,hivi wewe unaposikia biashara ndogo ndogo akilini mwako inakujia picha gani?
Mchina akiwa amekodi ground floor ya ghorofa fulani hapo mjini au amekodi warehouse kule Chang’ombe na kujaza mali akiuza makatoni kwa makatoni kwa wazawa au mchina amekodi frame moja ya 10x10 kama anayokodi Mkinga pale Kariakoo na kupanga sample huku akiuzia godwon?unataka kubishana kwa sababu ni hulka yako au unataka kueleweshwa?
Wanapewa tax holiday.Unawazuia wageni wasifanye biashara ili iweje?