up dates tafadhali leo maeneo mbalimbali hali ikoje juu ya huu mgomo........ jamjiiforums come on guys..... updates plzzzz
kuna kundi kubwa la wanafunzi wamevamia jengo la ITV na wanapiga kelele tunataka walimu wetu..aya yanaendelea ivi sasa hapa Mwenge.
Unakumbuka Yesu aliwaambiaje Mitume wake kuhusu Uongozi?.Kazi ya ualimu ni wito, Tafadhalini rudini darasani mkafundishe. hakuna haja ya kudai maslahi, kwani mnapata baraka kwa kujitoa kwenu sadaka kwa maendeleo ya taifa hili. hakuna mtaalamu au kiongozi ambaye hakupita katika mikono ya waalimu. kwa wale wakrisu turejee maandiko kwa upande wa waislamu kwa kweli sijui, lakini biblia inasisitiza kujitolea sadaka.
kafanye wewe kama ni wito! ndio wamekutuma kuja kumwaga huu ***** hapa???Kazi ya ualimu ni wito, Tafadhalini rudini darasani mkafundishe. hakuna haja ya kudai maslahi, kwani mnapata baraka kwa kujitoa kwenu sadaka kwa maendeleo ya taifa hili. hakuna mtaalamu au kiongozi ambaye hakupita katika mikono ya waalimu. kwa wale wakrisu turejee maandiko kwa upande wa waislamu kwa kweli sijui, lakini biblia inasisitiza kujitolea sadaka.
Tunaiomba SERIKALI isichukulie swala hili kimzahamzaha na kupandikiza PROPAGANDA lukuki. Ni vema serikali ikawa makini hasa kwa kuelezea namna wanavyoyashughulikia matatizo ya walimu na kuyatekeleza. Tunafahamu huu mgoma ulianza siku nyingi na ndiyo chanzo kikubwa cha elimu yetu kushuka (rejea matokeo ya mitihani shule za msingi na sekondari). Vilevile tunawajenga vijana wetu kutoiamini serikali na kuamini kuwa haki ni lazima ipiganiwe ndiyo ipatikane. Baada ya miaka 10-15 ndiyo tutaona madhara makubwa ya kuachia upepo huu upite.
Udhaifu wa Kikwete na Kawambwa hauwezi kutatua madai yalosababisha mgomo wa walimu, hapo ndio pakuanzia.
Ombi ni kuwa taasisi/asasi kama bunge, mabaraza ya haki za kiraia na NGOs waishinikize serikali hii kukaa chini na walimu na kutekeleza madai yao ambayo mengi ni ya msingi. Masikitiko ni kuwa tayari kiwango cha elimu kimeshuka mno na madhara ya mgomo huu yatazidi kuharibu mambo.
Hawa watoto kwenye picha ni wadogo, sasa kama tutawalea kwenye utamaduni kuwa kudai haki ni mpaka fujo baadaye hali itakuwa mbaya sana.
mkuu sasa itv na madai ya walimu wao imekuiwaje tena.....sipati connection hapo ebu nisaidie au wanataka wauze sura maana hawa watotowetu wa kiduku, face book, na .com hawa ni hatari sana
Kazi ya ualimu ni wito, Tafadhalini rudini darasani mkafundishe. hakuna haja ya kudai maslahi, kwani mnapata baraka kwa kujitoa kwenu sadaka kwa maendeleo ya taifa hili. hakuna mtaalamu au kiongozi ambaye hakupita katika mikono ya waalimu. kwa wale wakrisu turejee maandiko kwa upande wa waislamu kwa kweli sijui, lakini biblia inasisitiza kujitolea sadaka.
Ukiwauliza mmoja mmoja kwanini unaandamana, kila mmoja anajibu lake
Kuna mtoto ameulizwa kwanini unaandamana kajibu sijui, unaenda hadi wapi kajibu sijui, mbona uko barabarani kajibu basi tu kwa sababu wenzangu wamekuja na mie nimekuja tunashangilia.! Unashangilia nini kajibu mwenge.lol!
Yeye mwenyewe ni TISS. AAARGH, liwalo na liwe!Liwalo na Liwe, hizi Picha huziona? ama mpaka uambiwe na TISS?