Udhaifu wa Kikwete na Kawambwa hauwezi kutatua madai yalosababisha mgomo wa walimu, hapo ndio pakuanzia.
Ombi ni kuwa taasisi/asasi kama bunge, mabaraza ya haki za kiraia na NGOs waishinikize serikali hii kukaa chini na walimu na kutekeleza madai yao ambayo mengi ni ya msingi. Masikitiko ni kuwa tayari kiwango cha elimu kimeshuka mno na madhara ya mgomo huu yatazidi kuharibu mambo.
Hawa watoto kwenye picha ni wadogo, sasa kama tutawalea kwenye utamaduni kuwa kudai haki ni mpaka fujo baadaye hali itakuwa mbaya sana.