- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Nimeona Tanzania Abroad huko X ameweka picha hii na kusema ni "Mgomo wa wanafunzi Mbeya wameamua kufanya haya!! Hiki kizazi bado kipo kumbe nilidhan ni mayai mayai sana Shule zirejeshe watu wenye ujasiri"
JamiiCheck vipi kuna ukweli hapa?
JamiiCheck vipi kuna ukweli hapa?
- Tunachokijua
- Uhakiki wa Picha kwa kutumia Google Image Search ni njia muhimu ya kubaini asili au maelezo zaidi kuhusu picha fulani.
JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha. Rejea kiungo hiki kufuata hatua zote.
Kumekuwapo na picha inayosambazwa mtandaoni na kudaiwa kuwa ni mgomo wa wanafunzi mkoani Mbeya walioamua kufanya haya! Hiki kizazi bado kipo kumbe nilidhan ni mayai mayai sana Shule zirejeshe watu wenye ujasiri
Aidha picha hiyo bia baadhi ya kurasa za mitandao mbalimbali ya kijamii imedai kuwa ni kutoka shule ya sekondari Kisii nchini Kenya baada ya wanafunzi kufanya mgomo wa chakula.
Je, ni upi uhalisia wa picha?
Kupitia google reverse image search inabainisha kuwa picha hiyo imetengenezwa kwa kutumia Google AI.
Kadhalika picha hii imebainika kuwa na kiashiria kinachoonesha kuhusika kwa Akili Unde