Tetesi: Mgomo wa Wasafirishaji Dar kuanza Tarehe 1 Julai 2026

Hebu tafakari hata wewe, unatoaje Daladala ili ibaki mwendokasi?

Nina hakika Mwendokasi inabei tofauti na daladala, sasa watu hawajajiandaa unawatoa ghafla
Ndio maana barua imeandikwa kwa hasira sana kwamba wewe Chala ulipotoka Mbeya kuja Dar sisi ndio tumekupokea acha ufala
 
Hawa walioandika barua wana hoja za msingi sana. Siungi mkono kampuni moja kumilikishwa ruti nzima ya Mbagala. Athari kiuchumi ni kubwa hasa upande wa ajira. Mbaya zaidi hana uwezo wa kuhudumia wateja wake. Serikali iwasikilize wasafirishaji na kusitisha hilo zuio.
 
Issue sio mwendokasi issue ni Malori ila mabasi yamefanywa mbuzi wa kafara tu, ili waisikie milio vizuri October 29
 
Ila hata kama Dar es salaam, kweli unatoaje daladala Mbagala na kusema watu wato subirie mwendokasi.

Ni sawa route ya kwenda Dodoma waseme mabasi yasitumike iwe SGR peke yake
Wakati mbagala daladala zinaanza kazi saa tisa usiku
Raia wanadamka wanawahi kwenye majukumu yao
Sasa hao mofat sjui mwendokasi wataweza

Ova
 
Wakati mbagala daladala zinaanza kazi saa tisa usiku
Raia wanadamka wanawahi kwenye majukumu yao
Sasa hao mofat sjui mwendokasi wataweza

Ova
Yaani Mzee wa Kino kuna watu serikalini wanachofanya ni kama kuihujumu serikali iliyopo. Imagine watu wanaamua kumpa biashara inayogusa mamilioni ya watu mtu mmoja bila kujali chochote.
 
Issue sio mwendokasi issue ni Malori ila mabasi yamefanywa mbuzi wa kafara tu, ili waisikie milio vizuri October 29
Ila Barua yao haijazungumzia malori.. shida yao ni BRT.

Hata hivyo kama issue ni malori baado hoja yangu iko pale pale hatuna Mfumo mzuri wa transport planning.
 
Umeongea vyema, ndio maana naona hili lakutoa mwendo kasi sio la kitaalamu kutakuwa na mkubwa mmoja amechomeka hili...

Ninavisikiaga ni kuwa kuna watu hata hela ya Mwendokasi hawana
 
Yaani Mzee wa Kino kuna watu serikalini wanachofanya ni kama kuihujumu serikali iliyopo. Imagine watu wanaamua kumpa biashara inayogusa mamilioni ya watu mtu mmoja bila kujali chochote.
Samia anatakiwa alione hili, ndani ya serikali kuna watu wanachochea migogoro kati ya Serikali na wananchi
 
"Wakigoma tu tutawapa kipigo cha mbwa mwizi"‐— sensu Muroto
🤣🤣🤣🤣 Hakuna kitu kirahisi kama kugoma alafu hao wanataka kuikoa serikali na maandamano ya wananchi, fungua akili.

Mwendokasi moja haina uwezo wa kuhudumia watu wa Mbagala wote. Na wakitoka hapo hizo route mpya zitakuwa na impact gani kwenye biashara zao
 
Umeongea vyema, ndio maana naona hili lakutoa mwendo kasi sio la kitaalamu kutakuwa na mkubwa mmoja amechomeka hili...
Kuna jamaa mmoja alikua huko aliwai nisanua, kwenye mwendokasi huko kila nauli inayo lipwa Asilimia 25% inaenda kwa mkubwa mmoja, zingine zinazo Baki wanagawana.

Sasa mwisho wa siku, hata zile operational cost zinakosekana kabsa hela imeliwa, badala yake yanapelekwa garage kutunzwa, maana hata hela ya kuyatengeneza haipo
Ninavisikiaga ni kuwa kuna watu hata hela ya Mwendokasi hawana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…