bushman
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 2,412
- 747
Napingana na john marwa aliposema kuwa godbless lema alikuwa udom kuhamasisha maandamano sio kweli na hiyo inalenga kuingiza siasa katika elimu kitu ambacho ni kibaya sana,jana chadema walikuwa ukumbi wa polisi jamii na wanafunzi wakutoka vyuo vyote hapa dodoma mjini system kamwe haiwezi kumruhusu mwanasiasa hasa wq chama cha upinzani kam chadema afanye uhamasishaji wakati utulivu ulishapotea toka ijumaa. Kiini cha mgomo ni wanasiasa na mawaziri wa wili shamsi vuai nahodha waziri wa mambo ya ndani na shukuru kawambwa waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi,hawa mgomo wa mara ya mwisho ulihusiana na mambo hayohayo ya mafunzo kwa vitendo walikuja hapa kwa ndege ya kukodi ya serikali kusululisha mgogoro huu lakini njia iliyotumika kutatua mgogoro huu haukuzingatia taratibu za kisheria isipokuwa siasa ndiyo iliyotumika,management ya chuo ilipuuzwa na wanafunzi wakaambiwa "practical training ni haki yenu,wizara ya elimu inafungu la dharula mtakwenda wote field hata kwa degree zile ambazo hazikuwa na practical training" ikumbukwe kuwa kuna utaratibu wa kuboresha degree programme kila zinapoonekana kuleta shida na katika kulifanikisha hilo kunakuwa na kamati mbalimbali kuanzia ngazi ya idara,skuli,chuo mpaka senete chombo cha juu ktk kufanya maamuzi yanayohusiaana na taaluma,katika hili nahodha na kawambwa walikurupuka kutoa ahadi bila kuzingatia taratibu za kuborsha course content kutoka tcu zinasemaje,matokeo yake wanataka kufanya kitu ambacho huwezi kukifanya kwa miezi mitatu kiwe kimekwisha na ubora ukawa guaranteed,ni ukweli usiopingia migogoro yote hii inachangiwa na wanasiasa kuingilia taratibu za kielimu,haingiii akilini mwanafunzi anasoma degree public adm,project mgt,acc,bba n.k asiwe na mafunzo ya vitendo najiuliza waliopewa consultancy ya kuandaa mitaala hiyo walikuwa wanakusudia nini? Lakini najaribu kuiangalia serikali inalenga kuwa na wnafunzi 40,000 kwa muda mfupi sana bila kuguarantee quality ya products au inataka kuwafanyia hawa wanafunzi wa udom majaribio ya kuwa inawezekana kusoma bila mafunzo? Ili baadae practical zifutwe vyuo vyote? Mgogoro huu wanaotakiwa kuumaliza ni kawambwa na nahodha waende wakawambie tena practical ni haki yenu lakini serikali saizi haina hela mpaka majaliwa,na kwa nini wanasiasa hwataki kuichia udom ikajiamlia kufanya mambo yake yanayohusiana na taaluma badala ya kutoa maelezo yasiozingatia maelezo ya kikanuni za taaluma,baadala ya kuangalia wanafunzi wanaonyesha nini angani tunaangalia kidole anachotumia kuonyesha ni ujinga,serkali kukurupuka kufanya mambo zaidi ya wanafunzi 7000 wanatakiwa kwenda field hamkubajeti mkawakikishia fedha ipo leo mnasema haipo,wapeni wanachotaka.