Mgongano: Serikali Vs. Mwanahalisi - Mipaka ya Maoni?

Mgongano: Serikali Vs. Mwanahalisi - Mipaka ya Maoni?

Hiyo habari ya Kubenea ukiisoma kwa makini tu unajua kuna story ya kweli iliyoungwa na kuwekwa viungo vingi sana na KUPOTEZA LADHA YAKE HALISI.

Wenye fahamu na uelewa watakuwa wamenielewa.
 
Hiyo habari ya Kubenea ukiisoma kwa makini tu unajua kuna story ya kweli iliyoungwa na kuwekwa viungo vingi sana na KUPOTEZA LADHA YAKE HALISI.

Wenye fahamu na uelewa watakuwa wamenielewa.

unafikiri ni habari inayoweza kutosha kufanya gazeti lifungiwe kwa sababu ni ya kichochezi baada ya kuwekwa "viungo vingi sana"?
 
Kwa waliokosa kuyasikiliza mahojiano na Kubenea yatakuwa hewani muda si mrefu ujao kupitia KLH News... where
 
Hewala baba, asante ila sijatukana nimeweka mawazo yangu wewe premium member mawazo yako siyo idiotic.Nimejenga hoja kutokana na habari, niliposoma. Thanks again, hoja yako nzuri!

Asante kaka, sikuwa na taarifa kuwa Rweyemamu amezipinga hizo habari, sikuwa na taarifa hiyo.Kwa maneno yako simply naweza nikondoa commenta yangu.Thanks kunifumbua macho.
Pengine smart nilivyotumia hapo siyo unavyotaka wewe litumike.wala haimaanishi kama mtu hatishi siyo smart! read again friend, next time nitakuwa more clear.

Ndugu Waberoya,
Mimi siyo mtaalamu sana wa lugha hasa inapokuja hii ya malkia.Lakini hilo neno "smart" kwa haraka na katika hali ya maongezi linamaanisha mtu mwenye akili.Hata hivyo tukiacha hiyo lugha ya watu kwani msingi wetu hapa siyo kukosoa matumizi ya lugha,bado hata hivyo kuna kupingana kwa logic na dhima nzima ya bandiko lako na nio maana mimi nikachanganyikiwa hapo.

Umesema "hata hivyo huyo Ridhiwan siyo mtu makini" Wakati huohuo unatupa habari kuwa "alitaka kupindua serikali" ya wasomi pale chuo kikuu cha dar.

Sasa mimi hapo ndo natatizwa.Mtu ambaye siyo makini anawezaje kutaka kupindua serikali???
Anyways...tuyaache hayo coz umesema next time utakuwa makini zaidi.Wakondya
 
Ok; nimekuelewa kaka, sio ligi hii, tunasubiri mchango wako kuhusu hii post, what is your take? leta mambo, we wanna hear your comments

waberoya
 
Uandikaji wenyewe huo ni wa kufungiwa kweli? Labda kama nia ni kuonyesha uwepo wa DOLA. Jana, Salva alikanusha yaliyoandikwa kwenye gazeti hili na akasema Rais wetu bado anapendwa kama ilivyokuwa 2005!
 
Well binafsi wla sishangai kitu. Mume yeyote anayetumia muda mwingi nje kuliko nyumbani mara nyingi hupokewa na wataalam kuitunza nyumba...

Kikwete hana muda na mkewe mama yetu Tanzania...kila siku huja na visingizio asipokwenda nje kufanya kazi tutakula nini?....

Kosa kubwa!... ni muhimu kwa mwanaume kufahamu jinsi mwanamke anavyofikiria.. na jinsi ya kupanga priorities, kuna muda wa kazi na muda wa kupumzika nyumbani na familia...

Good choice of words.Nimekukubali mkuu
 
unafikiri ni habari inayoweza kutosha kufanya gazeti lifungiwe kwa sababu ni ya kichochezi baada ya kuwekwa "viungo vingi sana"?

Mwanahalisi haliwezi kufungiwa kwa kuwa INASEMEKANA kwamba ni gazeti la JK. Inasemekana JK anamtumia Kubenea kufikisha ujumbe kwa wanamzunguka kuwaambia kwamba anazijua mbinu zao na uozo wao.

Hivi mmewahi kujiuliza kwamba Kubenea anapata wapi ujasiri wa kuandika anayoya andika?
 
Hewala baba, asante ila sijatukana nimeweka mawazo yangu wewe premium member mawazo yako siyo idiotic.Nimejenga hoja kutokana na habari, niliposoma. Thanks again, hoja yako nzuri!

Asante kaka, sikuwa na taarifa kuwa Rweyemamu amezipinga hizo habari, sikuwa na taarifa hiyo.Kwa maneno yako simply naweza nikondoa commenta yangu.Thanks kunifumbua macho.
Wewe Kuhani wacha kutuharibia hii forum, unaposema habari ni ya uongo unatakiwa uweke habari kama ile yenye ukweli zaidi, otherwise uliyoitoa sio analysis ila ni ujinga period,

Kujenga hoja kama ulivyoanza ungesema kuwa hii habari ni ya uongo, kwa sababu habari ya ukweli ni hii hapa, one, two, three!

Ninarudia tena kwamba you are nothing but an idiot!
 
UONGO: Haya ninayoyasoma bado hayaniingii akilini kwa sababu zifuatazo.
1.Sijaona lolote la maana alilolifanya Kikwete kiasi kuwa ipelekee achukiwe na mafisadi

Hivi Kikwete angeigomea bunge unafikiri Lowassa angetoka uwaziri mkuu?

2 .Sijaona lolote analofanya Kikwete juu ya nchi yake so OP strategy ingefanywa na wasio mafisadi ndani ya CCM na wanaharakati basi ingeingia akilini.

Hujaona lolote, unafikiri kwa nini Karamagi, Msabaha, Meghji sio mawaziri tena? na hawa ni marafikiz ake wa karibu waliomsaidia kuwa rais?

Ridhiwani yuko smart, lakini pia sio mtu wa kutisha au kuwa eti ni fala kiasi hicho. Ridhwani ni mmoja wa watu waliotaka kupindua serikali ya DARUSO chini ya president Kayombo, nikiwa waziri, nilimsoma sana na kumuelewa, sio mjinga! Japo si wa kuwa ana nguvu mno,ushabiki wa nani awe kiongozi wa UVCCM inawezekana ni utashi wake na it has nothing to do na hilo mnalolisema.

Eti wewe ulisoma shule na Ridhiwani? When was that? Hivi umri wa Ridhiwani unaweza kuulingnaisha na wewe? huyu si anaweza kuwa mjukuu wako? ndio maana ninaita hizi analysis zako kuwa ni idiotic!

Hivyo basi gazeti la Mwanahalisi chini ya Kubenea, japo mmeshafanya mambo mengi makubwa nahuzunika kuwa inawezekana mmetugeuka. kwa sababu zifuatazo.

1. Mnataka mtuaminishe kuwa Kikwete anapigana na na mafisadi hivyo basi wako tayari kumng'oa .Kwa sababu gazeti lenu limeshaaminika, hivyo atakayesoma ataamini.

2. Kuelekea uchaguzi , ndio mnaleta taarifa kama hii.Hili hii taarifa iwe ya kuaminika , kindly provide us proof, kama ilivyo desturi yenu.

I submit

waberoya

Gazeti haliwezi kukuaminisha kitu ambacho wewe unakijua kuwa sio ukweli, sasa hapa wakupe proof ya nini hasa? Unafikiri kujaribu kubadili style yako ya uandikaji ndio itakufanya uonekane ni member mwingine that is what I call idiotic!

Kama ni hoja huna hoja ya msingi hata moja hapo, kwa sababu Mwanahalisi imezirudia te habari ambazo zimekwuepo kwa muda mrefu, zimezungumziwa kwenye vikao vya CCM, toka last week zimekwua zikiandikwa na magazeti akribu yote ya Tanzania, unless kama the whole media ya bongo iemamua kuandika habari za uongo,

Ndio maana ninasema hivi analysis zako ni very idiotic!
 
Ninapenda kusoma articles za Kubenea ila nadhani kwenye hili anaanza kutengeneza habari badala ya ku report habari.

Ni rahisi sana kwa mwandishi wa habari kuzidiwa na umaarufu na kuanza kukiuka maadili ya hiyo kazi. Inaelekea Kubenea ana hasira kubwa na Lowassa na hivyo kufanya judgement zake kuwa mbovu inapokuja mambo ya Lowassa.

Naona sasa nguvu inahamishwa kutoka kwa prof. Mwandosya na kuhamia kwa Lowassa. Siamini kabisa Lowassa ana mpango wa kumwondoa JK. Hawa watu ni kitu kimoja. Kama kuna mtu wanamwandaa basi ni kwa ajili ya 2015. Kama kuna kutofautiana kwa JK na Lowassa basi itakuwa wakati wa kumchagua rfais wa 2015 na wala sio 2010.

Hivi kweli mnataka kuamini huyo mtoto atamsaliti babake ambaye ni rais kwa ajili ya Lowassa?

Haya wengine yetu macho. Taaluma ya uandishi wa habari inatakiwa ikae pamoja na kutengeneza code of conduct, vinginevyo tunakoenda hiyo taaluma itakuwa ya mafisadi.
 
Kubenea huwa anaandika habari ambazo wengine wanashindwa kuziandika.

Wahariri wengi wa magazeti wamewekwa mkononi na Mengi,na inasemekana kuwa wamekubaliana kuwa habari ambazo magazeti ya Mengi au mengineyo hayawezi kuandika,apelekewe Kubenea.
Hilo Mwana Halisi inasemakana lina mkono wa Mengi.

Hao wakina Rostam wenyewe walishataka kuomba suluhu kwa Mengi na inasemekana aliwatolea nje.

Hizi habari sio za uongo,jipya hapo ni hilo la mwanawe JK kuhusishwa,ambalo ninaamini kabisa kuwa litakuwa na ukweli ndani yake.Kuna mambo mengi yamo humo,kati ya uhisiano wa wote waliotajwa na yana connect all the dots.

Ikiwa hii taarifa ni mpya kabisa kwa msomaji,then kutokuiamini ni rahisi sana(na ndio wanavyotegemea hao wakina Rweyemamu) Lakini kama mtu ulikuwa nafuatilia kwa makini toka baada ya uchaguzi,utaona kuna ukweli ambao ni dhahiri.

Mimi nilisema kwenye thread nyingine kuwa,yeye JK alitegemea nini kuwa na mke na mtoto kama wajumbe wa NEC? Huyo mtoto naye labda anaona urais ataukwaa tu
 
Gazeti halijachochea bali limetahadharisha tu. Ingekuwa vizuri badala ya kutishia kulipeleka mahakamani au kulifungia, wangemuita Kubenea kwa siri ili awape ushahidi na wautumie.

Nilimsikiliza Salva jana kwenye vyombo vya habari eti "kungalikuwapo njama za kumng'oa rais zingejulikana na wa kuzijua kwanza angekuwa ni rais mwenyewe kwani ana vyombo vingi" This is nonsense kabisa - kwani serikali zote zinazopinduliwaga huwa hazina vyombo hivyo?

Halafu anamtete JK eti anafanya kazi nzuri na ni maarufu ndani na nje ya nchi - upuuzi mwingine. Wewe Rweyemamu unajifungia tu Ikulu, hujui kinachoendelea huku nje. Anyway kwa kuwa wewe ni mdomo tu wa JK, usingeweza kusema tofauti - usingeweza kusema kweli kuna njama maana hiyo ingekuwa kauli ya Ikulu.

Mimi namwamini Kubenea; kwa kutaja waziwazi majina ya wahusika lazima anao ushahidi wa kutosha.

Ni kweli pia kuwa mafisadi wakimuondoa JK waTZ hatutafaidika iwapo wao watashika madaraka; lakini wana JF tusiogope maana huo utakuwa ndio mwanzo wa CCM kumeguka kabisa na hivyo neema kwa waTZ. Amini amini nawaambieni hakuna empire iitakayodumu milele maana hata US inadidimia.
 
Hivi kweli mnataka kuamini huyo mtoto atamsaliti babake ambaye ni rais kwa ajili ya Lowassa?

Mtanzania soma makala vizuri Gazeti limeandika ".... limeshindwa kuthibitisha mara moja kama Ridhiwani anaufahamu kwa undani mpango wa kumuondoa baba yake ikulu, japokuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwa anatumiwa"

Maana yake Gazeti lina ushahidi kuwa anatumiwa ila limeshindwa kuthibitisha kama anaufahamu kwa undani mpango huo. Yaani kuna watu wanamtumia Ridhiwani kuhakikisha wanawasimika viongozi wanaowataka bila ya yeye (Ridhiwani) kujua ajenda yao ya siri.

Hivyo tusimlaumu Ridhiwani kuwa anataka kumuondoa baba yake - hajui! anatumiwa tu!!
 
Kubenea huwa anaandika habari ambazo wengine wanashindwa kuziandika.

Wahariri wengi wa magazeti wamewekwa mkononi na Mengi,na inasemekana kuwa wamekubaliana kuwa habari ambazo magazeti ya Mengi au mengineyo hayawezi kuandika,apelekewe Kubenea.
Hilo Mwana Halisi inasemakana lina mkono wa Mengi.

Hao wakina Rostam wenyewe walishataka kuomba suluhu kwa Mengi na inasemekana aliwatolea nje.

Hizi habari sio za uongo,jipya hapo ni hilo la mwanawe JK kuhusishwa,ambalo ninaamini kabisa kuwa litakuwa na ukweli ndani yake.Kuna mambo mengi yamo humo,kati ya uhisiano wa wote waliotajwa na yana connect all the dots.

Ikiwa hii taarifa ni mpya kabisa kwa msomaji,then kutokuiamini ni rahisi sana(na ndio wanavyotegemea hao wakina Rweyemamu) Lakini kama mtu ulikuwa nafuatilia kwa makini toka baada ya uchaguzi,utaona kuna ukweli ambao ni dhahiri.

Mimi nilisema kwenye thread nyingine kuwa,yeye JK alitegemea nini kuwa na mke na mtoto kama wajumbe wa NEC? Huyo mtoto naye labda anaona urais ataukwaa tu

Zanaki,

Mimi ni mfuatiliaji wa mijadala hii ya siasa TZ lakini nina wasiwasi sana na ukweli kamili wa habari hii. Ningelikuwa na muda ningeichambua mstari kwa mstari lakini kwasasa nitaandika machache.

Moja huyo kijana wa JK ni mpiga debe wa huyo mgombea wa UVCCM tokea wakati Lowassa ni waziri mkuu, unaweza kurudi nyuma kusoma maandishi mbalimbali hapa JF na utalikuta hilo.

Pili mfano wa Zuma na Mbeki ni tofauti kabisa na mfano wa JK na Lowassa. Kwanza Mbeki hakuwahi kuwa rafiki yake Zuma, in fact Zuma na kundi lake muda wote walikuwa wanamwona Mbeki kama wa kuja ambaye hana historia ya mapambano ya SA. Sioni chuki yoyote ya wazi kati ya JK na Lowassa.

Tatu, mtu kama Mulla wa Mbeya ni mtandao kwa muda mrefu na hata kwenye uchaguzi wa mwaka jana wakati Lowassa bado ni PM alikuwa ni mtu wao. Sijaona nyendo zozote tofauti za Mulla kwamba sasa kaanza kumsaliti JK kwa ajili ya Lowassa.

Nne, hao wenyeviti watatu wa CC ni idadi ndogo sana katika CC na mwenyekiti wa CCM ana nguvu kubwa kwenye CC kiasi kwamba sio rahisi ongezeko la hao watatu kuweza kuleta maasi. Pia kuna wazee wa chama hasa Mwinyi na Kawawa ambao wana nguvu kubwa mno kwenye hicho chama na dalili zote zinaonyesha wanamuunga mkono JK.

Ukisoma kwa makini unagundua mwandishi anatumia info ambayo iko kwenye public kutaka kujenga chuki kati ya Lowassa na JK. Kubenea ni stakeholder kwenye hili maana kwa yeye angetaka kwa nguvu zote kuona Lowassa na JK wanakosana.

Mimi naona hii habari ni kama ile ya JK na Prof. Mwandosya ambayo watu wanatumia ukweli mdogo kujenga tatizo kubwa. Baada ya kushindwa kule kwa prof sasa wanaanza kuhamia kwa Lowassa.

Binafsi simtaki Lowassa tokea enzi za Nyerere na naamini hana nafasi tena ya kuwa rais au PM wa Tanzania. Anaweza kurudi kwenye baraza la mawaziri lakini sio kuwa rais au PM. Pamoja na hayo, pia sipendi kulishwa sumu na hawa waandishi ambao chuki zao binafsi zinakuwa mbele kuliko ukweli wa habari.
 
Hivi mmeshawahi kujiuliza kuwa labda yote haya ni mpango maalumu kati ya JK, Low na Rost,yakuwa hawa jamaa ni marafiki wa karibu sana na hakuna tofauti zozote kati yao, labda hii ni strategy ya kisiasa JK aonekane anamaadui and the rest of wananchi wa-sympathize naye....hivi sasa kila kitu kibaya kinachotokea Tz utasikia ni Low na Rost hao wanajaribu kumhujumu muungwana kutokea kwenye mgao wa mmeme ambao umetokana na mitambo kukorofisha, kuvuja kwa mitihani e.t.c hii inaweza ikawa mbinu ya kisiasa ya kumnusuru muungwana, ili wananchi wamwone yeye ni bore sana lakini kuna watu wachache wanamuharibia tu....

Nchi inajegwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno.

Kalaga baho.
 
Zanaki,

Mimi ni mfuatiliaji wa mijadala hii ya siasa TZ lakini nina wasiwasi sana na ukweli kamili wa habari hii. Ningelikuwa na muda ningeichambua mstari kwa mstari lakini kwasasa nitaandika machache.

Moja huyo kijana wa JK ni mpiga debe wa huyo mgombea wa UVCCM tokea wakati Lowassa ni waziri mkuu, unaweza kurudi nyuma kusoma maandishi mbalimbali hapa JF na utalikuta hilo.

Pili mfano wa Zuma na Mbeki ni tofauti kabisa na mfano wa JK na Lowassa. Kwanza Mbeki hakuwahi kuwa rafiki yake Zuma, in fact Zuma na kundi lake muda wote walikuwa wanamwona Mbeki kama wa kuja ambaye hana historia ya mapambano ya SA. Sioni chuki yoyote ya wazi kati ya JK na Lowassa.

Tatu, mtu kama Mulla wa Mbeya ni mtandao kwa muda mrefu na hata kwenye uchaguzi wa mwaka jana wakati Lowassa bado ni PM alikuwa ni mtu wao. Sijaona nyendo zozote tofauti za Mulla kwamba sasa kaanza kumsaliti JK kwa ajili ya Lowassa.

Nne, hao wenyeviti watatu wa CC ni idadi ndogo sana katika CC na mwenyekiti wa CCM ana nguvu kubwa kwenye CC kiasi kwamba sio rahisi ongezeko la hao watatu kuweza kuleta maasi. Pia kuna wazee wa chama hasa Mwinyi na Kawawa ambao wana nguvu kubwa mno kwenye hicho chama na dalili zote zinaonyesha wanamuunga mkono Lowassa.

Ukisoma kwa makini unagundua mwandishi anatumia info ambayo iko kwenye public kutaka kujenga chuki kati ya Lowassa na JK. Kubenea ni stakeholder kwenye hili maana kwa yeye angetaka kwa nguvu zote kuona Lowassa na JK wanakosana.

Mimi naona hii habari ni kama ile ya JK na Prof. Mwandosya ambayo watu wanatumia ukweli mdogo kujenga tatizo kubwa. Baada ya kushindwa kule kwa prof sasa wanaanza kuhamia kwa Lowassa.

Binafsi simtaki Lowassa tokea enzi za Nyerere na naamini hana nafasi tena ya kuwa rais au PM wa Tanzania. Anaweza kurudi kwenye baraza la mawaziri lakini sio kuwa rais au PM. Pamoja na hayo, pia sipendi kulishwa sumu na hawa waandishi ambao chuki zao binafsi zinakuwa mbele kuliko ukweli wa habari
.

Mkuu mtu akisoma btwn the lines..Inaonekana hata wewe umeshatake sides.

Well sijui..from what I read from your post inaonekana umetofautiana na huyu mwandishi na at the centre ni Mwandosya. Anyway that was my observation. Which may be wrong or right. But all in all nimeisoma barua ya Kubenea..iko very tricky sana, na ukienda mahakamani kwa barua kama hii..itapigwa chini mapema kabisa! ila mwenye kupata ujumbe amepata. Na nadhani ndo lengo kuu la Kubenea.

Hivi jamani kuna mtu anaye dare kutwambia kwamba Lowassa arudi kwenye nafasi ya maamuzi katika nchi yetu? hata kwenye cabinet?

Folks, watanzania million 40..tunakosa watu wa kutuongoza mpaka tukawainamie akina Lowassa waliokwisha tutenda?

Guys lets know that Tanzania is bigger than JK, Lowassa, Rostam etc...Honestly we can do better.
 
Ikulu: JK hang’oki

na Happiness Katabazi na Sauli Giliard
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

OFISI ya Rais (Ikulu) imesema hakuna kundi lolote linalopanga njama za kutaka kumzuia Rais Jakaya Kikwete ili ashindwe kugombea urais katika muhula mwingine wa pili mwaka 2010.

Tamko hilo la Ikulu lilitolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Salvatory Rweyemamu, aliyekuwa akizungumza na wanahabari ofisini kwake kuhusu habari zilizoandikwa katika gazeti la kila wiki lililochapishwa juzi Jumatano.

Katika mazungumzo yake hayo, Rweyemamu aliielezea habari hiyo iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho: ‘Njama za kumngo’a Kikwete zafichuka’ kuwa ni za uzushi na zenye lengo la kumfitinisha rais na mawaziri wake.

Mbali ya hilo, Rweyemamu alisema habari hiyo ya MwanaHalisi ilikuwa ni porojo za ‘kuganga njaa’ na akawataka wanaoliendesha gazeti hilo kuachana na kazi ya habari iwapo wameshindwa kuifanya.

“Huu ni uongo uliotungwa na kutiwa chumvi nyingi tu kwa lengo la kutaka kuuza gazeti. Ni porojo tu za kutaka kuuza gazeti,” alisema mkurugenzi huyo.

Rweyemamu alichukua fursa hiyo kuwahakikishia wananchi kutokuwapo kwa tishio wala njama za kumng’oa Kikwete katika uongozi wake.

“Unamng’oa vipi rais ambaye utendaji wake wa kazi umeleta mafanikio makubwa kwa wananchi na umekuwa mfano wa kuigwa mbele ya mataifa mengine?

‘‘Hakuna tishio lolote, hakuna njama zozote za kumng’oa rais madarakani, iwe ni leo au mwaka 2010, kama gazeti hilo lilivyodai... kama kungekuwa na njama hizo mtu wa kwanza kujua angekuwa ni rais mwenyewe, kwani rais ana vyombo vya ulinzi na usalama,” alisema Rweyemamu.

Alisema kuwa Kikwete ameendelea kupendwa, kuungwa mkono na kuaminiwa na wananchi waliomchagua kwa kishindo, na zaidi ya yote, vyombo vya ulinzi viko macho wakati wote kuhakikisha kuwa yuko salama.

Katika hatua nyingine, mkurugenzi huyo alisema gazeti hilo linatumiwa na vyama vya upinzani na kazi yake imekuwa ni kueneza propaganda za vyama hivyo.

Wakati Ikulu ikitoa tamko hilo, Mbunge wa Igunga Rostam Aziz (CCM), amefungua kesi ya madai Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam dhidi ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Hali Halisi Ltd, inayochapisha gazeti la MwanaHALISI na Mseto, Saed Kubenea, akitaka amlipe fidia ya sh bilioni tatu kwa kumkashfu.

Mbali na Kubenea, wengine walioshitakiwa katika kesi hiyo ni mhariri wa MwanaHALISI, Hali Halisi Puplishers na Kampuni ya Uchapaji ya Printech Ltd.

Kesi hiyo ambayo tayari imeshapewa namba 143 ya mwaka huu, muda wowote kuanzia sasa inatarajiwa kupangiwa jaji wa kuiendesha.

Katika kesi hiyo, Rostam anadai kuwa, wadaiwa wote kwa nafasi zao wamekiuka miiko na maadili kwa kuchapisha habari ya uzushi dhidi yake.

Rostam anayetetewa na wakili wa kujitegemea, Kennedy Fungamtama, alidai gazeti la MwanaHALISI la Septemba 24-30 toleo namba 116, katika ukurasa wa 1 na 2, wadaiwa waliandika na kuchapisha habari iliyokuwa na picha ya mlalamikaji na kichwa cha habari: ‘Rostam atajwa tena. Ni katika ukwapuaji wa sh bilioni 13, ofisi, wafanyakazi wake watuhumiwa’.

Anadai yeye (Rostam) akiwa mbunge, mfanyabiashara na mtu mwenye heshima ndani ya jamii, amefedheheshwa na habari hiyo, kwani inajenga chuki kwa wananchi. Kutokana na sababu hiyo, anaiomba mahakama hiyo iamuru (Kubenea) amlipe kiasi hicho cha fedha na pia aombwe radhi ukurasa wa mbele kwenye gazeti hilo.

“Habari hiyo imejaa uzushi na haina ukweli wowote, haijafanyiwa utafiti kabla haijaandikwa, hivyo mwandishi wa habari hiyo amekiuka maadili ya kazi yake. Na kwa sababu hiyo, nataka nilipwe fidia ya kiasi hicho na (mahakama) iwaamuru wadaiwa waniombe radhi katika gazeti lao,” alidai mbunge huyo katika hati hiyo ya mashitaka.

Juzi serikali ililitaka gazeti hilo kujitetea kwa nini lisichukuliwe hatua kutokana na habari iliyochapishwa kuwa kuna njama za kumng’oa Rais Jakaya Kikwete ili asigombee urais mwaka 2010.

Kutokana na habari hiyo, serikali ilimpa siku tatu Kubenea, ambazo zinamalizika leo kuwasilisha maelezo yake ya kina Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kuhusu tuhuma mbalimbali alizoziibua katika habari hiyo.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa juzi na wizara hiyo na kusainiwa na msemaji wake, Jacob Tesha, ilieleza gazeti hilo limedai kundi la watuhumiwa wa ufisadi limejipanga kumng’oa Rais Kikwete mwaka 2010 na kuwataja baadhi ya viongozi wa CCM na mwanawe Rais, Ridhiwani, kuwa wanahusika katika njama hizo.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa habari hiyo ni ya uchochezi, inayolenga kumgombanisha rais na viongozi waandamizi wa CCM na kuleta mtafaruku katika familia yake.

Mbali na hilo, kupitia taarifa hiyo, serikali imewaonya baadhi ya waandishi wa habari ambao kwa makusudi, wamekuwa wakiandika habari zisizo sahihi na zenye kuchochea chuki miongoni mwa jamii.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, katika miezi ya hivi karibuni, gazeti hilo limekuwa likiandika habari zisizo sahihi na za uchochezi, jambo lililosababisha wahariri wa gazeti hilo kuonywa na serikali mara kadhaa.
 
Mhh Lets see.But what im sure of Kubenea usually write what He knows and He is sure of.I know him
 
Mafisadi mbali mbali bado wamekumbatiwa na CCM akina RA, Manji, Karamagi, Lowassa, Mzee wa Vijisenti Chenge n.k. CCM ni wanafiki wanakumbatia hata watu wenye sifa mbaya katika umma wa Watanzania na pia ni chama cha mafisadi. Hatutashangaa chama cha mafisadi kikimlinda Kikwete ili aendelee na miaka mingine mitano pamoja na kuonyesha uwezo finyu, woga, kutolinda au kutetea maslahi ya Tanzania badala ta mafisadi na wageni.
 
Back
Top Bottom