Mgongano: Serikali Vs. Mwanahalisi - Mipaka ya Maoni?


Mtanzania,

JK inawezekana kabisa hana machungu na Lowassa,lakini sio vice versa! Lowassa anaamini kabisa kuwa JK angeweza kumsevu wakati ule.JK on the other hand anataka kujiweka mbali na mtandao wa wakina RA kabla ya hio 2010.

2010 kwa JK sio assured tena kama alivodhania mwanzoni.Kumbuka baada ya ule uchaguzi wa 2005,lengo lake kubwa lilikuwa ni kupata kura nyingi kuliko alizopata wakati ule kwenye uchaguzi wa 2010,akiamini kuwa he was the right person to lead this country into 'greatness'.
Ghafla sasa hivi imekuwa ni kuhusu survival.

Asikudanganye mtu kuwa Mwinyi na Kawawa wanamuunga mkono Lowassa.Hawa wote walipinga vikali uteuzi wake kuwa PM,leo ndio wamtake awe raisi wetu? Watakuwa machizi basi hao wazee

Huu ni wakati mzuri wa CCM kumeguka ili upinzani wa kweli uwepo.Wakina Sitta,Malecela na wengineo wanatakiwa kubaki na CCM Asili ili hao wengine wakaunde Academia au Chipolopolo....
 
Kubenea amekutana na waandishi wa habari na hii ndio taarifa yake ya leo

 
Kwa Kubenea na yeye kuitisha Press conference kama salva, inaelekea kuna jambo linalotokea nyuma ya pazia. Inafaa kuwa Kubenea amedokeza kuwa serikali ina lengo la kulifuta gazeti lake, labda sasa tutaanza kupata mwanga wa nini kinachotokea.
Lakini Kubenea alipaswa kueleza mengi zaidi anayoyajua kuhusu mpango wa kutaka kumng'oa JK. Kujitetea kwa kutumia Rai kunaweza kusiwe relevant sana kwa sababu si busara kutumia makosa ya mwenzako kulala mlango wazi.
Au alikuwa anajaribu subira ya serikali?
 

Nilikuwa na maana Kawawa na Mwinyi wanamuunga mkono JK na wala sio Lowassa. Ni typing error tu ila mtiririko wa habari ulikuwa unaonyesha wazi naongelea JK.
 
Huku ndio kujisahau kwenyewe. Kuona madaraka ni mali yao.
 
Hiyo habari ya Kubenea ukiisoma kwa makini tu unajua kuna story ya kweli iliyoungwa na kuwekwa viungo vingi sana na KUPOTEZA LADHA YAKE HALISI.

Wenye fahamu na uelewa watakuwa wamenielewa.

...na in short serikali ikienda tu mahakamani kwa habari kama hii.......wanaumbuka.........ndio maana nikasema..........i would love to watch this game.........
 
pamoja na kubenea kuwaamsha lakini yeye bado yupo usingizini............kalaghabao!!!!!!!!!! alie lala usi mwamshe.........

Nashindwa kumwelewa huyu Bwana Salva.Sijui uwezo wake wa ku -analyse mambo ukoje!
 
Huwezi kujua mipaka ya maoni hadi utoe maoni yanayowahusu watawala. Je porojo zina haki ya kutolewa? Kama habari si za kweli ni wajibu wa wenye ukweli kuutoa hadharani.

Mimi ningetarajia mtu kutuonesha ukaribu wa Rais na wote waliotajwa. Hivi mara ya mwisho JK, RA na EL wameonekana pamoja ( i mean siyo kuwemo kwenye vikao vinavyowataka kuwemo) ni lini? Ni lini EL amekana kuwa hana mpango huo au RA? Kama Ikulu wanaona hakuna mpango huo lilikuwa ni jukumu lao kuonesha kwanini wanaamini hakuna. Na kama wanajua MwanaHalisi wamevunja sheria serikali ingepaswa kwenda mahakamani.

Hata hivyo kuna tatizo; serikali haiwezi kwenda mahakamani kwani wanayo tayari sheria ya Magazeti ya 1976 ambayo ikitumiwa in combination na sheria ya Usalama wa Taifa ya 1970 ina maana hawana sababu ya kwenda mahakamani kwani Waziri anakuwa ndiye Mtuhumu, Mwendesha Mashtaka na Jaji!

Nitaomba nichambue tishio hili tena kwa uhuru wa maoni. Wanaokumbuka watakumbuka jinsi kucha hizi za serikali zilipojaribu kunolewa pale magazeti yalipotumia neno "msanii/wasanii" kuwataja JK na EL (uhuru kwenye mtandao iliandika picha ya EL na JK kuwa ni wasanii.jpg). Tunakumbuka jinsi gani serikali ilikuja juu na Makamba aliweza kutumia kitisho cha "Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama" kuwa wasimchezee kwani bado ana hulka (instinct) za kijeshi.

Tulisimama tuliwapinga na kuwakebehi wale tuliothubutu na kucha zao zikakunjwa. Lakini sasa tukiendelea kuwachekelea watatuparua.
 
Hivi na huyu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) ana elimu gani huyu........wenye CV yake please
 

Asante kumbe mtu asiyejua jambo, akaweka analyisis zake based on what he knows ni idiotic.



Asante kaka kwa analyisis nzuri, just imagine ulivyofanya analyisis hapa, na ile comment yako ya mwanzo vinaeleza jinsi ulivyo. Sina ugomvi na wewe wala sijajua ni wapi nimekosea.Nimeweka mawazo yangu kama forums inavyotaka.....Mtu anapoweka mawazo inabidi asaidiwe kama ulivyosema hapa.

Kaka unataka kila mtu awaze kama wewe..., na yeyote atakayetofautian na wewe basi ni idiot.Angalia ulivyojibu hoja hapa shows that your mature , though is not necessary agreeable, au ndio umewin!

Simjui hata huyo mtu aitwaye Kuhani, wala sijajua kwa nini hayumo humu ndani.Wala sijajua ameaha kivuli gani nyuma, pengine comments zako ulizotoa kwa kujua mimi ni huyo kuhani. I am simply mere man, studying abroad, sina akili sana wala premeium member kama wewe. Ila kwa akili zangu ndogo niliweka mawazo kama nionavyo. FM I am not only one who thinks different concerning this matter. wengi wana mawazo tofauti.

NAKUOMBA UNIPE NAFASI MOYONI MWAKO MIMI AMBAYE MAWAZO YANGU NI IDIOT, ILI NINAPOTOA MAWAZO IDIOT WEWE AU MWINGINE ANAIELEWESHE AU AJENGE HOJA, first time ulichemsha kaka haihitji debate, angalia mlalahoi alivyonielewesha, I said my first comment relied only on what I read nothing else, Lakini sikuwa peke yangu

Could this be idiot again? should I give you proof that I am not Kuhani, well this also may sound idiot, but kindly receive me as member of JF, who can have different opinions(idiotic ones) .

Asante

Waberoya
 
Mtanzania,

JK inawezekana kabisa hana machungu na Lowassa,lakini sio vice versa! Lowassa anaamini kabisa kuwa JK angeweza kumsevu wakati ule.JK on the other hand anataka kujiweka mbali na mtandao wa wakina RA kabla ya hio 2010.

Hivi nani alimwambia Lowassa ajiuzulu? ni Kikwete? Nani aliyeandika barua ya kujiuzulu? na kumpelekea rais? Kikwete angefanya nini, wakati ule na ule upepo ulivyokuwa?

waberoya
 

Una busara sana kaka!hili libaba linalojiita FMS ni kama vile halina akili!yaani hata mimi lilinidhania ni huyo kuhani!Yaani wewe ukiwa tofauti tu basi!

Any way ndo maisha na ukizingatia watu wanaunganishwa na internet basi mtu anakuwa na hisia tu mbaya zaidi anaamini hisia zake hata kama ni uongo!
 

Angalizo:
Mie kwa hili sina mengi sana ila nitawakumbusha wanaJF wenzangu kuwa vitabu vya Mwenzimungu vimesema Yeye(Mungu) atatupa viongozi wanaofanana na watakao waongoza. Ninaheshimu sana maandiko na nina amini kuwa yana ukweli ukweli mtupu.
 
Angalizo:
Mie kwa hili sina mengi sana ila nitawakumbusha wanaJF wenzangu kuwa vitabu vya Mwenzimungu vimesema Yeye(Mungu) atatupa viongozi wanaofanana na watakao waongoza. Ninaheshimu sana maandiko na nina amini kuwa yana ukweli ukweli mtupu.

Mkuu, maneno mazito sana haya. lakini yanahitaji ufafanuzi wa kina na kuyapa muktadha wa hoja iliyo mezani
 
Date::10/10/2008
Hatua ya serikali kuhusu gazeti MwanaHalisi yawakera wahariri
Kizitto Noya Fidelis Butahe
Mwananchi

JUKWAA la Wahariri limesema limehuzunishwa na hatua, jinsi na nguvu iliyotumika na Serikali kushughulikia habari iliyoandikwa na gazeti la MwanaHalisi Jumatano wiki hii.

Taarifa iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Sakina Datoo ilisema jukwaa limehuzunika kwa kuwa inaonekana serikali ilikuwa ikilitafuta gazeti hilo na Mhariri wake siku nyingi kwani habari inayosema kuwa ya uchochezi, sio mpya kuripotiwa na vyombo vya habari.

"Kwa nini habari hii ilete shida kwa Gazeti la MwanaHalisi pekee wakati tayari iliripotiwa na kuandikwa na Gazeti la Rai kwenye moja ya matoleo yake ya Aprili mwaka huu?" alihoji.

Alisema mbali na habari kutokuwa mpya, serikali inaonekana kukosa nia njema kwa Gazeti la MwanaHalisi kwani Mhariri wake hakupewa muda wa kutosha kuitetea habari yake.

"Tunaishangaa Serikali na tunaamini haina nia njema na MwanaHalisi kwani hata maelekezo yake ya kumtaka mhariri atoe utetezi yanatofautiana," alisema.

Sakina alisema, Jumatano wiki hii siku ambayo habari hiyo ilichapishwa kwenye gazeti, Serikali ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari iliyosema Mhariri wa gazeti hilo ameaandikiwa barua kumtaka atoe utetezi ifikapo Ijumaa (jana) saa 10 jioni, lakini muda mfupi baadaye agizo hilo lilibadilishwa na kumtaka mhariri huyo awasilishe utetezi Alhamisi (juzi).

"Kwa nini Serikali haina utaratibu wa maelekezo ya utetezi kama ina nia njema. Inaonekana haitaki kumpa muda Mhariri kujitetea?,"


Kwa mujibu wa Sakina kitendo hicho cha kubadilisha muda wa kuwasilisha utetezi pamoja na kauli ya Ikulu juzi, zinaonyesha dhahiri kumhukumu Mhariri wa MwanaHalisi kabla ya utetezi wake, ni ishara kwamba kuna jambo nyuma ya pazia katika suala hilo.

Sakina aliisihi serikali na taasisi zingine zote nchini kuwa na uvumilivu katika kutatua masuala mbalimbali hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linajenga demokrasia badala ya kuvitisha vyombo vya habari kwa lengo la kuvinyamazisha.

Alisema uamuzi wowote wa serikali wa kutaka kulifuta ama kulifungia Gazeti la MwanaHalisi kwa sababu ya habari hiyo itakuwa ni uonevu usiokuwa na msingi wenye busara.

Kauli hiyo ya Jukwaa la wahariri ilikuja baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi inayochapicha magazeti ya MwanaHalisi na Mseto, Saed Kubenea kusema kuwa Serikali ina lengo la kuangamiza gazeti lake.


Kubenea alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana na kubainisha kuwa tamko la serikali kwamba, habari iliyoandikwa na Gazeti la MwanaHalisi kuwa 'kuna njama za kumng'oa Rais Jakaya Kikwete asigombee urais 2010' ni uchochezi inaashiria jinsi serikali ilivyodhamiria kuliangamiza gazeti hilo.
 
Angalizo:
Mie kwa hili sina mengi sana ila nitawakumbusha wanaJF wenzangu kuwa vitabu vya Mwenzimungu vimesema Yeye(Mungu) atatupa viongozi wanaofanana na watakao waongoza. Ninaheshimu sana maandiko na nina amini kuwa yana ukweli ukweli mtupu.

Nimecheka sana, nadhani hii sentensi inahitaji kitabu kufafanua, anyway let me try using few lines.

Rais wa nchi huwekwa na watu, kama Rais fisadi, ina maana waliomchagua ni mafisadi, kama alikuwa safi akageuka, it means we have poor systems ambazo haziwezi kumfanya lolote Rais aliye madarakani. Na izi sytems huwekwa na watu.


Hamna jamii safi yenye system safi ikamuweka RaiS wa haina hii madarakani.

Kikwete ana wakilisha tamaduni zetu, majumbani, makazini na kila mahali.Kama jamii fisadi Rais atapatikana kifisadi, kwa hiyo na yeye fisadi,Mtu safi hakai kwenye system chafu, akikaa akijua aamekubaliana nao!

Walio wasafi kumchagua kiongozi mchafu kuna mawili aidha jamii mbumbumbu(wajinga)au HAIJAWEKA SYESTEM RAIS WAO HAWEJE. hatujui historia za hawa viongozi, walifanya nini huko nyuma. aidha kama walihusika kusaini mikataba mibovu au la, na ahata kama tulijua walifanya ubaya, Lakini wanakuja wakivaa nguo nyingine, na kuomba cheo kikubwa kuliko kile, tunajiaminisha kuwa siyo yeye!

Wote wamepotea na kupungukiwa utukufu wa uadilifu, kila mahali Tanzania imeoza, makanisani na misikitini jamii imeoza. Kama msafi ni wewe mweyewe ujuaye, lakini usishangae wapiga kelele wengi wa ufisadi wao wenyewe mafisadi, tunajiaminisha kila mtu atakula "ofsini mwake"

I submit

waberoya
 
Kinachotakiwa sasa ni hiyo serikali ifungie hilo gazeti, halafu Kubenea aende mahakamani kushitaki kuwa hajatendewa haki. Hapo ni mambo yote hadharani! Ngoja tuone!
 
Kinachotakiwa sasa ni hiyo serikali ifungie hilo gazeti, halafu Kubenea aende mahakamani kushitaki kuwa hajatendewa haki. Hapo ni mambo yote hadharani! Ngoja tuone!

Umemaliza!

Wasipompeleka mahakamani. kuna jambo, maana habari hii si nyepesi ni nzito yamkini.Wakimpeleka mahakamani akashinda kesi tutaangalia ameshindaje? kuna kitu kinaendelea na tunaangalia, kama Mwanahalisi si ya JK, tuone ya nani. by the way kwa nini imekuwa kama taarifa ya vijiweni, withou proof, angekaa kimya au atoe kila kitu hadharani.Au ndiyo biashara watu tununue gazeti lake?

waberoya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…