Mgongano: Serikali Vs. Mwanahalisi - Mipaka ya Maoni?

Mgongano: Serikali Vs. Mwanahalisi - Mipaka ya Maoni?

Zanaki,

Mimi ni mfuatiliaji wa mijadala hii ya siasa TZ lakini nina wasiwasi sana na ukweli kamili wa habari hii. Ningelikuwa na muda ningeichambua mstari kwa mstari lakini kwasasa nitaandika machache.

Moja huyo kijana wa JK ni mpiga debe wa huyo mgombea wa UVCCM tokea wakati Lowassa ni waziri mkuu, unaweza kurudi nyuma kusoma maandishi mbalimbali hapa JF na utalikuta hilo.

Pili mfano wa Zuma na Mbeki ni tofauti kabisa na mfano wa JK na Lowassa. Kwanza Mbeki hakuwahi kuwa rafiki yake Zuma, in fact Zuma na kundi lake muda wote walikuwa wanamwona Mbeki kama wa kuja ambaye hana historia ya mapambano ya SA. Sioni chuki yoyote ya wazi kati ya JK na Lowassa.

Tatu, mtu kama Mulla wa Mbeya ni mtandao kwa muda mrefu na hata kwenye uchaguzi wa mwaka jana wakati Lowassa bado ni PM alikuwa ni mtu wao. Sijaona nyendo zozote tofauti za Mulla kwamba sasa kaanza kumsaliti JK kwa ajili ya Lowassa.

Nne, hao wenyeviti watatu wa CC ni idadi ndogo sana katika CC na mwenyekiti wa CCM ana nguvu kubwa kwenye CC kiasi kwamba sio rahisi ongezeko la hao watatu kuweza kuleta maasi. Pia kuna wazee wa chama hasa Mwinyi na Kawawa ambao wana nguvu kubwa mno kwenye hicho chama na dalili zote zinaonyesha wanamuunga mkono Lowassa.

Ukisoma kwa makini unagundua mwandishi anatumia info ambayo iko kwenye public kutaka kujenga chuki kati ya Lowassa na JK. Kubenea ni stakeholder kwenye hili maana kwa yeye angetaka kwa nguvu zote kuona Lowassa na JK wanakosana.

Mimi naona hii habari ni kama ile ya JK na Prof. Mwandosya ambayo watu wanatumia ukweli mdogo kujenga tatizo kubwa. Baada ya kushindwa kule kwa prof sasa wanaanza kuhamia kwa Lowassa.

Binafsi simtaki Lowassa tokea enzi za Nyerere na naamini hana nafasi tena ya kuwa rais au PM wa Tanzania. Anaweza kurudi kwenye baraza la mawaziri lakini sio kuwa rais au PM. Pamoja na hayo, pia sipendi kulishwa sumu na hawa waandishi ambao chuki zao binafsi zinakuwa mbele kuliko ukweli wa habari.

Mtanzania,

JK inawezekana kabisa hana machungu na Lowassa,lakini sio vice versa! Lowassa anaamini kabisa kuwa JK angeweza kumsevu wakati ule.JK on the other hand anataka kujiweka mbali na mtandao wa wakina RA kabla ya hio 2010.

2010 kwa JK sio assured tena kama alivodhania mwanzoni.Kumbuka baada ya ule uchaguzi wa 2005,lengo lake kubwa lilikuwa ni kupata kura nyingi kuliko alizopata wakati ule kwenye uchaguzi wa 2010,akiamini kuwa he was the right person to lead this country into 'greatness'.
Ghafla sasa hivi imekuwa ni kuhusu survival.

Asikudanganye mtu kuwa Mwinyi na Kawawa wanamuunga mkono Lowassa.Hawa wote walipinga vikali uteuzi wake kuwa PM,leo ndio wamtake awe raisi wetu? Watakuwa machizi basi hao wazee

Huu ni wakati mzuri wa CCM kumeguka ili upinzani wa kweli uwepo.Wakina Sitta,Malecela na wengineo wanatakiwa kubaki na CCM Asili ili hao wengine wakaunde Academia au Chipolopolo....
 
Kubenea amekutana na waandishi wa habari na hii ndio taarifa yake ya leo

Kasaba Street, Plot 57/31A Kinondoni
P. O. Box 67311, Dar es Salaam, Tel.: +255 784 440 073, 0784 447077
Fax: +255 22 276 0560, website:www.halihalisi.com.tz/mwana
E-mail: halihalisi06@yahoo.com

10 – 10 – 2008

Taarifa kwa vyombo vya habari

NIA YA SERIKALI YA KUFUNGA MwanaHALISI

NI wazi sasa kwamba serikali imedhamiria kuangamiza gazeti la MwanaHALISI. Inalituhumu “kufanya uchochezi.”

Juzi, 8 Oktoba, 2008 Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo ilitoa tamko la kulaani gazeti letu kwa kuandika kuwa “kuna njama za kumg’oa Rais Kikwete” ili asigombee urais mwaka 2010.

Taarifa ya wizara iliyosambazwa Jumatano kwa vyombo vya habari ilitupa siku tatu hadi leo tuwe tumejieleza kwa nini tusichukuliwe hatua kwa kuandika hivyo pamoja na madai mengine ya serikali.

Siku hiyohiyo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) ambaye kwa nafasi yake ndiye Msajili wa Magazeti, alituandikia akitaka tujitetee kwa nini tusichukuliwe hatua kwa kuandika habari hiyo.
Tofauti na Wizara iliyotaka maelezo katika siku tatu, MAELEZO ilitaka utetezi kesho yake – jana kabla ya saa 9.30. Tofauti ya muda wa utetezi inaweza kutafsiriwa kuwa nia ya haraka ya kutaka kuzima gazeti letu.

Hata tulipoomba muda wa kujibu hadi Jumatatu, MAELEZO ilikataa, kwa maandishi kuwa lazima tujibu jana hiyohiyo. Kazi hiyo tumeifanya na maelezo tuliyopeleka mnaweza kuyapa hukohuko, MAELEZO.

Kama kwamba hiyo haitoshi, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa habari iliyoandikwa na gazeti letu ulikuwa “uongo uliotungwa na kutiwa chumvi nyingi tu kwa lengo la kutaka kuuza gazeti. Ni porojo tu za kutaka kuuza gazeti.”

Nimewaiteni hapa kuwaambia kuwa serikali, kwa kauli za Wizara ya Habari, MAELEZO na kauli za Salva Rweyemamu, imedhamiria kuua gazeti letu.

Tayari tumejieleza MAELEZO na wizarani. Lakini tunaweza kusema kitu kimoja hapa; kuwa tusingependa serikali ichukue hatua ya kufungia wala kufuta gazeti hili la wananchi.

Rweyemamu anasema tuliandika “porojo” ili kuganga njaa. Tunasema siyo porojo. Lakini kuna porojo ngapi mitaani na katika vyombo vya habari ambazo hazijaitikiwa kwa kishindo kama hiki?

Lakini kichekesho ni kwamba gazeti la Rai lilipoandika kuwa “Waziri aanza mbio za kumng’oa JK 2010” (Rai Aprili 10-16, 2008), si Rweyemamu wala MAELEZO wala wizara ya habari ilijitokeza kulaani

Rai liliandika, “Waziri mmoja aliyepo katika serikali ya Rais Kikwete, ameanza harakati za kugombea urais mwaka 2010, akitumaini kumuangusha rais aliyeko madarakani.”

Tofauti iliyopo kati ya “kuangusha” na “kung’oa” ni ya uchaguzi tu wa neno lipi litumike kwa shabaha ya kuweka uzito upi. Serikali ilikaa kimya.

Tunataka kusema kuwa habari ya MwanaHALISI inayolalamikiwa haina uchochezi ndani yake.

Tulitarajia serikali kusema inachunguza habari tulizochapa na kutafuta ukweli wake. Tulitarajia kuombwa msaada na wahusika katika uchunguzi huu. Tulitarajia Rweyemamu aseme hajapata taarifa za kikundi au watu binafsi kufanya njama, kwa hiyo anahitaji taarifa zaidi, badala ya kukimbilia kudai kuwa hakuna njama.

Tulitarajia wale walioguswa kulalamika na hata kwenda mahakamani ili watafute, siyo tu ukweli, bali haki mbele ya chombo cha kutoa haki kikatiba.

Tunaitaka serikali kuwa na uvumilivu katika kila jambo na hasa katika mambo yanayoigusa yenyewe na watendaji wake.

Tunatarajia hekima itatawala huku tukiendelea kuamini kuwa tulichoandika ni sahihi, siyo porojo na siyo uchochezi.

Tunataka kuamini pia kuwa serikali ina wajibu wa kuheshimu na kulinda uhuru wa wananchi wa kuendelea kutumia MwanaHALISI kama chombo chao cha mawasiliano.

…………….
Saed Kubenea
Mkurugenzi
Hali Halisi Publishers Limited
 
Kwa Kubenea na yeye kuitisha Press conference kama salva, inaelekea kuna jambo linalotokea nyuma ya pazia. Inafaa kuwa Kubenea amedokeza kuwa serikali ina lengo la kulifuta gazeti lake, labda sasa tutaanza kupata mwanga wa nini kinachotokea.
Lakini Kubenea alipaswa kueleza mengi zaidi anayoyajua kuhusu mpango wa kutaka kumng'oa JK. Kujitetea kwa kutumia Rai kunaweza kusiwe relevant sana kwa sababu si busara kutumia makosa ya mwenzako kulala mlango wazi.
Au alikuwa anajaribu subira ya serikali?
 
Mtanzania,

JK inawezekana kabisa hana machungu na Lowassa,lakini sio vice versa! Lowassa anaamini kabisa kuwa JK angeweza kumsevu wakati ule.JK on the other hand anataka kujiweka mbali na mtandao wa wakina RA kabla ya hio 2010.

2010 kwa JK sio assured tena kama alivodhania mwanzoni.Kumbuka baada ya ule uchaguzi wa 2005,lengo lake kubwa lilikuwa ni kupata kura nyingi kuliko alizopata wakati ule kwenye uchaguzi wa 2010,akiamini kuwa he was the right person to lead this country into 'greatness'.
Ghafla sasa hivi imekuwa ni kuhusu survival.

Asikudanganye mtu kuwa Mwinyi na Kawawa wanamuunga mkono Lowassa.Hawa wote walipinga vikali uteuzi wake kuwa PM,leo ndio wamtake awe raisi wetu? Watakuwa machizi basi hao wazee

Huu ni wakati mzuri wa CCM kumeguka ili upinzani wa kweli uwepo.Wakina Sitta,Malecela na wengineo wanatakiwa kubaki na CCM Asili ili hao wengine wakaunde Academia au Chipolopolo....

Nilikuwa na maana Kawawa na Mwinyi wanamuunga mkono JK na wala sio Lowassa. Ni typing error tu ila mtiririko wa habari ulikuwa unaonyesha wazi naongelea JK.
 
Hiyo habari ya Kubenea ukiisoma kwa makini tu unajua kuna story ya kweli iliyoungwa na kuwekwa viungo vingi sana na KUPOTEZA LADHA YAKE HALISI.

Wenye fahamu na uelewa watakuwa wamenielewa.

...na in short serikali ikienda tu mahakamani kwa habari kama hii.......wanaumbuka.........ndio maana nikasema..........i would love to watch this game.........
 
pamoja na kubenea kuwaamsha lakini yeye bado yupo usingizini............kalaghabao!!!!!!!!!! alie lala usi mwamshe.........

Nashindwa kumwelewa huyu Bwana Salva.Sijui uwezo wake wa ku -analyse mambo ukoje!
 
Huwezi kujua mipaka ya maoni hadi utoe maoni yanayowahusu watawala. Je porojo zina haki ya kutolewa? Kama habari si za kweli ni wajibu wa wenye ukweli kuutoa hadharani.

Mimi ningetarajia mtu kutuonesha ukaribu wa Rais na wote waliotajwa. Hivi mara ya mwisho JK, RA na EL wameonekana pamoja ( i mean siyo kuwemo kwenye vikao vinavyowataka kuwemo) ni lini? Ni lini EL amekana kuwa hana mpango huo au RA? Kama Ikulu wanaona hakuna mpango huo lilikuwa ni jukumu lao kuonesha kwanini wanaamini hakuna. Na kama wanajua MwanaHalisi wamevunja sheria serikali ingepaswa kwenda mahakamani.

Hata hivyo kuna tatizo; serikali haiwezi kwenda mahakamani kwani wanayo tayari sheria ya Magazeti ya 1976 ambayo ikitumiwa in combination na sheria ya Usalama wa Taifa ya 1970 ina maana hawana sababu ya kwenda mahakamani kwani Waziri anakuwa ndiye Mtuhumu, Mwendesha Mashtaka na Jaji!

Nitaomba nichambue tishio hili tena kwa uhuru wa maoni. Wanaokumbuka watakumbuka jinsi kucha hizi za serikali zilipojaribu kunolewa pale magazeti yalipotumia neno "msanii/wasanii" kuwataja JK na EL (uhuru kwenye mtandao iliandika picha ya EL na JK kuwa ni wasanii.jpg). Tunakumbuka jinsi gani serikali ilikuja juu na Makamba aliweza kutumia kitisho cha "Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama" kuwa wasimchezee kwani bado ana hulka (instinct) za kijeshi.

Tulisimama tuliwapinga na kuwakebehi wale tuliothubutu na kucha zao zikakunjwa. Lakini sasa tukiendelea kuwachekelea watatuparua.
 
Hivi na huyu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) ana elimu gani huyu........wenye CV yake please
 
Hivi Kikwete angeigomea bunge unafikiri Lowassa angetoka uwaziri mkuu?

Asante kumbe Lowasa alitolewa na Kikwete!

Hujaona lolote, unafikiri kwa nini Karamagi, Msabaha, Meghji sio mawaziri tena? na hawa ni marafikiz ake wa karibu waliomsaidia kuwa rais?

Asante kunifunua mawazo


Eti wewe ulisoma shule na Ridhiwani? When was that? Hivi umri wa Ridhiwani unaweza kuulingnaisha na wewe? huyu si anaweza kuwa mjukuu wako? ndio maana ninaita hizi analysis zako kuwa ni idiotic!


(una proof?)Nina miaka 31, kaka muulize Ridhwani, waziri wa afya Daruso, during Kayombo's

Gazeti haliwezi kukuaminisha kitu ambacho wewe unakijua kuwa sio ukweli, sasa hapa wakupe proof ya nini hasa? Unafikiri kujaribu kubadili style yako ya uandikaji ndio itakufanya uonekane ni member mwingine that is what I call idiotic!

Kama ni hoja huna hoja ya msingi hata moja hapo, kwa sababu Mwanahalisi imezirudia te habari ambazo zimekwuepo kwa muda mrefu, zimezungumziwa kwenye vikao vya CCM, toka last week zimekwua zikiandikwa na magazeti akribu yote ya Tanzania, unless kama the whole media ya bongo iemamua kuandika habari za uongo,
Ndio maana ninasema hivi analysis zako ni very idiotic!

Asante kumbe mtu asiyejua jambo, akaweka analyisis zake based on what he knows ni idiotic.



Asante kaka kwa analyisis nzuri, just imagine ulivyofanya analyisis hapa, na ile comment yako ya mwanzo vinaeleza jinsi ulivyo. Sina ugomvi na wewe wala sijajua ni wapi nimekosea.Nimeweka mawazo yangu kama forums inavyotaka.....Mtu anapoweka mawazo inabidi asaidiwe kama ulivyosema hapa.

Kaka unataka kila mtu awaze kama wewe..., na yeyote atakayetofautian na wewe basi ni idiot.Angalia ulivyojibu hoja hapa shows that your mature , though is not necessary agreeable, au ndio umewin!

Simjui hata huyo mtu aitwaye Kuhani, wala sijajua kwa nini hayumo humu ndani.Wala sijajua ameaha kivuli gani nyuma, pengine comments zako ulizotoa kwa kujua mimi ni huyo kuhani. I am simply mere man, studying abroad, sina akili sana wala premeium member kama wewe. Ila kwa akili zangu ndogo niliweka mawazo kama nionavyo. FM I am not only one who thinks different concerning this matter. wengi wana mawazo tofauti.

NAKUOMBA UNIPE NAFASI MOYONI MWAKO MIMI AMBAYE MAWAZO YANGU NI IDIOT, ILI NINAPOTOA MAWAZO IDIOT WEWE AU MWINGINE ANAIELEWESHE AU AJENGE HOJA, first time ulichemsha kaka haihitji debate, angalia mlalahoi alivyonielewesha, I said my first comment relied only on what I read nothing else, Lakini sikuwa peke yangu

Could this be idiot again? should I give you proof that I am not Kuhani, well this also may sound idiot, but kindly receive me as member of JF, who can have different opinions(idiotic ones) .

Asante

Waberoya
 
Mtanzania,

JK inawezekana kabisa hana machungu na Lowassa,lakini sio vice versa! Lowassa anaamini kabisa kuwa JK angeweza kumsevu wakati ule.JK on the other hand anataka kujiweka mbali na mtandao wa wakina RA kabla ya hio 2010.

Hivi nani alimwambia Lowassa ajiuzulu? ni Kikwete? Nani aliyeandika barua ya kujiuzulu? na kumpelekea rais? Kikwete angefanya nini, wakati ule na ule upepo ulivyokuwa?

waberoya
 
Asante kumbe mtu asiyejua jambo, akaweka analyisis zake based on what he knows ni idiotic.

Asante kaka kwa analyisis nzuri, just imagine ulivyofanya analyisis hapa, na ile comment yako ya mwanzo vinaeleza jinsi ulivyo. Sina ugomvi na wewe wala sijajua ni wapi nimekosea.Nimeweka mawazo yangu kama forums inavyotaka.....Mtu anapoweka mawazo inabidi asaidiwe kama ulivyosema hapa.

Kaka unataka kila mtu awaze kama wewe..., na yeyote atakayetofautian na wewe basi ni idiot.Angalia ulivyojibu hoja hapa shows that your mature , though is not necessary agreeable, au ndio umewin!

Simjui hata huyo mtu aitwaye Kuhani, wala sijajua kwa nini hayumo humu ndani.Wala sijajua ameaha kivuli gani nyuma, pengine comments zako ulizotoa kwa kujua mimi ni huyo kuhani. I am simply mere man, studying abroad, sina akili sana wala premeium member kama wewe. Ila kwa akili zangu ndogo niliweka mawazo kama nionavyo. FM I am not only one who thinks different concerning this matter. wengi wana mawazo tofauti.

NAKUOMBA UNIPE NAFASI MOYONI MWAKO MIMI AMBAYE MAWAZO YANGU NI IDIOT, ILI NINAPOTOA MAWAZO IDIOT WEWE AU MWINGINE ANAIELEWESHE AU AJENGE HOJA, first time ulichemsha kaka haihitji debate, angalia mlalahoi alivyonielewesha, I said my first comment relied only on what I read nothing else, Lakini sikuwa peke yangu

Could this be idiot again? should I give you proof that I am not Kuhani, well this also may sound idiot, but kindly receive me as member of JF, who can have different opinions(idiotic ones) .

Asante

Waberoya

Una busara sana kaka!hili libaba linalojiita FMS ni kama vile halina akili!yaani hata mimi lilinidhania ni huyo kuhani!Yaani wewe ukiwa tofauti tu basi!

Any way ndo maisha na ukizingatia watu wanaunganishwa na internet basi mtu anakuwa na hisia tu mbaya zaidi anaamini hisia zake hata kama ni uongo!
 
Ni vigumu kuhudhunika au kufurahia habari hii kwani kwa upande mmoja Muungwana has to go,ikiwezekana hata kesho maana 2010 ni mbali mno.Lakini kwa upande mwingine,hao mafisadi wako worse than Muungwana,na kibaya zaidi hawapangi kumuondoa Muungwana kwa sababu ameshindwa ku-deliver bali kulipa kisasi na kudumisha ufisadi wao.Siasa za Tanzania zinapitia kipindi kigumu sana.

Na hapo tumetajiwa wanasiasa tu,hatujui positions za wakuu wa vyombo vya dola (wa sasa na wastaafu) katika mkakati huo.Ikitokea mkakati huo mufilisi ukafanikiwa,God forbid,basi Muungwana hatakuwa na wa kumlaumu zaidi ya uzembe na uoga wake yeye mwenyewe.He has every ways and means at his disposal kuwashughulikia mafisadi but he chose to protect them.Alichosahau ni kwamba ushirika wa wachawi (au maharamia) haudumu.

Nimekuwa muumini mkubwa wa theory kwamba Lowassa na mafisadi wenzie could hardly wait till 2015,hasa kwa vile wanafahamu fika kuwa by then mambo kadhaa yanaweza kubadili political landscape ya Tanzania na hivyo nyota yake na wenzake kuwa imefifia.He also knows kwamba kwa vile Muungwana will have nothing to lose kama hatamsapoti Lowassa katika presidential bid yake ya 2015,anaweza kabisa kuacha kudhibiti any dirty that could be unleashed against him,especially kutokana na kushamiri kwa siasa za majitaka huko home.

Wanaoujua mtandao wanasema kwamba ni vigumu sana kwa Muungwana kuwageuka baadhi ya watu walimwingiza madarakani hasa kwa vile wanajua mengi machafu kuhusu yeye.However,mie naendelea kumwona kuwa ni dhaifu kwani urais katika nchi za dunia ya tatu ni u-mungu mtu,akiamua lolote dhidi ya yeyote linawezekana.

Tutashuhudia mengi sana kati ya sasa na 2010.Bad news is mengi hayo hayatakuwa na manufaa yoyote kwa wanyonge.At last sasa naona relevancy ya mstari "Mungu Ibariki Tanzania" kwenye our national anthem

Angalizo:
Mie kwa hili sina mengi sana ila nitawakumbusha wanaJF wenzangu kuwa vitabu vya Mwenzimungu vimesema Yeye(Mungu) atatupa viongozi wanaofanana na watakao waongoza. Ninaheshimu sana maandiko na nina amini kuwa yana ukweli ukweli mtupu.
 
Angalizo:
Mie kwa hili sina mengi sana ila nitawakumbusha wanaJF wenzangu kuwa vitabu vya Mwenzimungu vimesema Yeye(Mungu) atatupa viongozi wanaofanana na watakao waongoza. Ninaheshimu sana maandiko na nina amini kuwa yana ukweli ukweli mtupu.

Mkuu, maneno mazito sana haya. lakini yanahitaji ufafanuzi wa kina na kuyapa muktadha wa hoja iliyo mezani
 
Date::10/10/2008
Hatua ya serikali kuhusu gazeti MwanaHalisi yawakera wahariri
Kizitto Noya Fidelis Butahe
Mwananchi

JUKWAA la Wahariri limesema limehuzunishwa na hatua, jinsi na nguvu iliyotumika na Serikali kushughulikia habari iliyoandikwa na gazeti la MwanaHalisi Jumatano wiki hii.

Taarifa iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Sakina Datoo ilisema jukwaa limehuzunika kwa kuwa inaonekana serikali ilikuwa ikilitafuta gazeti hilo na Mhariri wake siku nyingi kwani habari inayosema kuwa ya uchochezi, sio mpya kuripotiwa na vyombo vya habari.

"Kwa nini habari hii ilete shida kwa Gazeti la MwanaHalisi pekee wakati tayari iliripotiwa na kuandikwa na Gazeti la Rai kwenye moja ya matoleo yake ya Aprili mwaka huu?" alihoji.

Alisema mbali na habari kutokuwa mpya, serikali inaonekana kukosa nia njema kwa Gazeti la MwanaHalisi kwani Mhariri wake hakupewa muda wa kutosha kuitetea habari yake.

"Tunaishangaa Serikali na tunaamini haina nia njema na MwanaHalisi kwani hata maelekezo yake ya kumtaka mhariri atoe utetezi yanatofautiana," alisema.

Sakina alisema, Jumatano wiki hii siku ambayo habari hiyo ilichapishwa kwenye gazeti, Serikali ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari iliyosema Mhariri wa gazeti hilo ameaandikiwa barua kumtaka atoe utetezi ifikapo Ijumaa (jana) saa 10 jioni, lakini muda mfupi baadaye agizo hilo lilibadilishwa na kumtaka mhariri huyo awasilishe utetezi Alhamisi (juzi).

"Kwa nini Serikali haina utaratibu wa maelekezo ya utetezi kama ina nia njema. Inaonekana haitaki kumpa muda Mhariri kujitetea?,"


Kwa mujibu wa Sakina kitendo hicho cha kubadilisha muda wa kuwasilisha utetezi pamoja na kauli ya Ikulu juzi, zinaonyesha dhahiri kumhukumu Mhariri wa MwanaHalisi kabla ya utetezi wake, ni ishara kwamba kuna jambo nyuma ya pazia katika suala hilo.

Sakina aliisihi serikali na taasisi zingine zote nchini kuwa na uvumilivu katika kutatua masuala mbalimbali hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linajenga demokrasia badala ya kuvitisha vyombo vya habari kwa lengo la kuvinyamazisha.

Alisema uamuzi wowote wa serikali wa kutaka kulifuta ama kulifungia Gazeti la MwanaHalisi kwa sababu ya habari hiyo itakuwa ni uonevu usiokuwa na msingi wenye busara.

Kauli hiyo ya Jukwaa la wahariri ilikuja baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi inayochapicha magazeti ya MwanaHalisi na Mseto, Saed Kubenea kusema kuwa Serikali ina lengo la kuangamiza gazeti lake.


Kubenea alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana na kubainisha kuwa tamko la serikali kwamba, habari iliyoandikwa na Gazeti la MwanaHalisi kuwa 'kuna njama za kumng'oa Rais Jakaya Kikwete asigombee urais 2010' ni uchochezi inaashiria jinsi serikali ilivyodhamiria kuliangamiza gazeti hilo.
 
Angalizo:
Mie kwa hili sina mengi sana ila nitawakumbusha wanaJF wenzangu kuwa vitabu vya Mwenzimungu vimesema Yeye(Mungu) atatupa viongozi wanaofanana na watakao waongoza. Ninaheshimu sana maandiko na nina amini kuwa yana ukweli ukweli mtupu.

Nimecheka sana, nadhani hii sentensi inahitaji kitabu kufafanua, anyway let me try using few lines.

Rais wa nchi huwekwa na watu, kama Rais fisadi, ina maana waliomchagua ni mafisadi, kama alikuwa safi akageuka, it means we have poor systems ambazo haziwezi kumfanya lolote Rais aliye madarakani. Na izi sytems huwekwa na watu.


Hamna jamii safi yenye system safi ikamuweka RaiS wa haina hii madarakani.

Kikwete ana wakilisha tamaduni zetu, majumbani, makazini na kila mahali.Kama jamii fisadi Rais atapatikana kifisadi, kwa hiyo na yeye fisadi,Mtu safi hakai kwenye system chafu, akikaa akijua aamekubaliana nao!

Walio wasafi kumchagua kiongozi mchafu kuna mawili aidha jamii mbumbumbu(wajinga)au HAIJAWEKA SYESTEM RAIS WAO HAWEJE. hatujui historia za hawa viongozi, walifanya nini huko nyuma. aidha kama walihusika kusaini mikataba mibovu au la, na ahata kama tulijua walifanya ubaya, Lakini wanakuja wakivaa nguo nyingine, na kuomba cheo kikubwa kuliko kile, tunajiaminisha kuwa siyo yeye!

Wote wamepotea na kupungukiwa utukufu wa uadilifu, kila mahali Tanzania imeoza, makanisani na misikitini jamii imeoza. Kama msafi ni wewe mweyewe ujuaye, lakini usishangae wapiga kelele wengi wa ufisadi wao wenyewe mafisadi, tunajiaminisha kila mtu atakula "ofsini mwake"

I submit

waberoya
 
Kinachotakiwa sasa ni hiyo serikali ifungie hilo gazeti, halafu Kubenea aende mahakamani kushitaki kuwa hajatendewa haki. Hapo ni mambo yote hadharani! Ngoja tuone!
 
Kinachotakiwa sasa ni hiyo serikali ifungie hilo gazeti, halafu Kubenea aende mahakamani kushitaki kuwa hajatendewa haki. Hapo ni mambo yote hadharani! Ngoja tuone!

Umemaliza!

Wasipompeleka mahakamani. kuna jambo, maana habari hii si nyepesi ni nzito yamkini.Wakimpeleka mahakamani akashinda kesi tutaangalia ameshindaje? kuna kitu kinaendelea na tunaangalia, kama Mwanahalisi si ya JK, tuone ya nani. by the way kwa nini imekuwa kama taarifa ya vijiweni, withou proof, angekaa kimya au atoe kila kitu hadharani.Au ndiyo biashara watu tununue gazeti lake?

waberoya
 
Back
Top Bottom