Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 15,328
- 11,192
Mkuu wangu Ushi Wa Rombo,
Heshima mbele sana, msimpe nafasi huyu jamaa akaharibu flaw ya hii habari maana bado, tunaendelea kuzi-monitor hizi habri muhimu sana maana some how somewhere ninaamini kwamba jupi linataka kupasuka huko ndani ya CCM.
Sasa msimpe nafasi huyu jamaa kuubadili huu mjadala kuwa yeye kama anavyotaka sasa badala ya taifa letu, mind you huyu jamaa wala sio raia wa Tanzania kama mimi na wewe, ndio maana hulilia sana dual-citizen ipitishwe, lakini tulishawafahamisha wabunge wengi kwua wakipitisha hiyo basi Tanzania tutegemee watu wengi kama huyu bwana kuja kutuchafulia amani ya taifa letu.
Pole sana kwa kazi hii mkuu FMES.
Tuko pamoja kuwakoma hawa mafisadi
Nimekuwa msomaji mzuri sana wa Mwanahalisi, sijasikia Kikwete akikanusha ama kukaripia habari zinazoandikwa Mwanahalisi. Ninachokumbuka ni kwamba, wakati Kubenea alipomwagiwa tindikali, JK alienda hospitali ' in person' kwenda kumjulia hali na kumwambia kwamba asikatishwe tamaa na watu (isomeke M.A.F.I.S.A.D.I) wasiomtakia mema yeye na taifa kwa ujumla.
Kwa sababu hiyo basi naamini kabisa kwamba JK anajua kabisa kinachoendelea katika sakata zima hili, ndio sababu kaamua kukaa kimya.
Tuendelee kulumbana!