Mgongano: Serikali Vs. Mwanahalisi - Mipaka ya Maoni?

sorry.. sijui ilikuwa inasikikaje; I had to try new program... Natumaini mtakuwa mmesikiliza waliyoyakosa mahojiiano hayo nitayarusha tena kesho ili uweze kuyasikia katika njia mbalimbali kupitia KLHN..na hapa JF...

Mwanakijiji, nilikupata loud & clear; shukurani sana mkuu! ... taratibu tutafika nchi ya ahadi.
 
Nafikiri hata mafao Lowassa hakusi kabisa, kuna mtu kwenye serikali yetu wa kuweka kifua pale, hata kama sheria inasema waziri mkuu apate mafao nafikiri wangerekebisha ili mtu akivurunda anapigwa chini na mafao hakuna.

Mkuu nimethibitisha 100%, kuwa hapewi huyu ila mkulu alimuonea huruma akampa walinzi wawili kwa kuogopa kuhusu ufisadi wake kuna wanaoweza kummuwinda na kumuumiza, lakini anaposafriri hulipa mwenyewe, na hata mabalozi yetu huwa hayajishughulishi naye tena kama wenziwe wanavyofanyiwa, hii ni safi sana.
 
Granted that the prospect of prosecution is real, the cited letters exist in the given context and Mr. Kubenea faces an onslaught of the brunt of governmental wrath in full regalia, I am sadenned to officially recognize Tanzania as a "Police State".

There is a thin line between incendiary remarks or malicious news coverage and genuine political analysis.

Mr Kubenea was reporting the analysis of a celebrated political analyst in the name of Professor Baregu.If the government takes issue with the political views and analysis of the good Professor, it should act against the Professor, not the agent of information that carried his views to the public.

The government, (such a stiff upper lipped one at that) in coming down with full force against a mere newspaper, carrying political analysis, gives the crucial credibility to the story in a Shakesperean twist of "The lady doth protest too much".If you see too much protest where none or little is warranted, recognize it is not as unwarranted as it would like to appear.

Muungwana anaogopa kibarua kuota majani vibaya sana.
 
Hii isije ikawa ndio wanapanga kum-suprise Friday jioni ya kesho na warranty kama walivyomfanyie Friday ingine ile ya kumpekua na kuchukua computer! Just speculating though!
 
Nimemsikia Salva hivi punde akilaani taarifa ya Kubenea na kusema kuwa ina lengo la kuleta uchochezzi. Kama kawaida, amemsifia sana Kikwete na kusema kuwa hakuna mtu atakuwa na nia ya kumwondoa rais ambaye amefanya kazi nzuri kama JK!!!

pamoja na kubenea kuwaamsha lakini yeye bado yupo usingizini............kalaghabao!!!!!!!!!! alie lala usi mwamshe.........
 
Habari hii iliyokuwa Ukurasa wa mbele wa gazeti la Mwanahalisi siku ya Jumatano Octoba 8, 2008 ndiyo iliyozua kasheshe. Pamoja nayo (hapo chini) ni mahojiano tuliyofanya na Bw. Kubenea baada ya kupokea barua kadhaa kumtaka atoe maelezo juu ya makala hii ambayo inaonekana ni ya kichochezi napia kichonganishi. Isome, msikilize na amua mwenyewe kama Gazeti la Mwanahalisi limevumka mpaka na linastahili kufungiwa au kupatiwa adhabu yeyote kwa mujibu wa sheria ya magazeti ya 1976.

Njama kumng’oa Kikwete zafichuka
• Mwanae Ridhiwani ashiriki njama
• Watuhumiwa ufisadi wajipanga

KUNDI la watuhumiwa wa ufisadi limejipanga kumng’oa Rais Jakaya Kikwete ili asigombee urais mwaka 2010, MwanaHALISI limegundua.

Taarifa zinasema tayari baadhi ya marafiki wa Kikwete wameunda kile kinachoitwa, “One-term President (OP),” ikimaanisha “Kikwete rais wa kipindi kimoja.”

Suala la Kikwete kuwa rais wa kipindi kimoja lilikuwa mkakati wa baadhi ya washirika wa Kikwete katika kundi la mtandao wakati wa kampeni za urais za 2005.

Taarifa zinawataja Edward Lowassa na Rostam Aziz kuwa viongozi waandamizi wa mtandao waliokuwa wanaendesha mkakati huo. Aliyekuwa anaandaliwa kumwondoa Kikwete alikuwa Edward Lowassa.

Hivi karibuni mkakati wa kushika chama ndiyo ulifanikisha Jacob Zuma kumuondoa Thabo Mbeki kwenye urais nchini Afrika Kusini.

Zuma aliweka mkakati wa kushika chama mara baada ya kuondolewa katika nafasi ya makamu wa rais kwa kashfa za ufisadi na rushwa.

Mara baada ya kuondolewa katika nafasi yake, Zuma alijipanga kushika uongozi wa chama cha ANC ambapo alifanikiwa kumshinda Mbeki na baadaye kumfukuza urais.

Katika CCM, taarifa zinasema, kundi lililopanga kugombea urais mwaka 2010, limekuwa likipigania kuwepo “watu wake” katika nafasi za juu za uongozi katika Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Kamati Kuu (CC).
Baadhi ya wanaotajwa kuandaliwa ni wenyeviti wa mikoa: Deo Sanga (Jaa People- Iringa), Ernest Mabina (Mwanza) na Khamis Mgeja (Shinyanga).

Wengine ni John Guninita (Dar es Salaam), Nawab Mulla (Mbeya), Onesmo Ngole (Arusha), William Kusila (Dodoma) na Hypolitus Matete (Sumbawanga).

Haijafahamika kwa sasa nani ameandaliwa kumrithi Kikwete baada ya Lowassa kujiuzulu wadhifa wake wa waziri mkuu kutokana na kashifa ya Richmond.

Hata hivyo, mpango wa kumg’oa Kikwete bado uko palapale, ingawa waaandaji wanaweza kubadilisha mbinu na mkakati ikiwamo hata kushirikisha watu wengine na kwa malengo tofauti.

Tayari wajumbe wa kundi hilo wamekutana katika miji ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Arusha kuweka mkakati wa kutekeleza azma hiyo. Wajumbe kadhaa wakiwamo baadhi ya mawaziri na wajumbe wa NEC walihudhuria mikutano hiyo.

Taarifa za kuaminika zinasema kikao cha karibuni kimefanyika siku chache baada ya kumalizika kwa kikao cha NEC mwezi uliopita.

Inaelezwa kwamba kwa sasa mkakati wa kundi hilo ni kusimika viongozi katika uchaguzi unaoendelea ndani ya jumuiya za CCM.

Uchaguzi huo unaendelea nchi mzima na unatarajiwa kufikia kilele chake mwishoni mwa mwaka huu.

Gazeti hili liliwasiliana na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba na kumueleza kuwa kuna kundi linotaka kumdhoofisha Kikwete kwa mtindo wa Mbeki wa Afrika ya kusini na kwamba jina lake limetajwa.

Makamba aling’aka, “Sijui kitu. Nasema sijui kitu.” Alipong’ang’anizwa kwamba itakuwaje hajui wakati yeye ni katibu mkuu wa chama, Makamba alijibu kwa sauti kali, “Nakwambia sijui kitu.”

Mjumbe mmoja wa NEC ambaye hakupenda jina lake kutajwa gazetini alipotakiwa maoni yake na gazeti hili alisema, “Inawezekana hata yeye (Makamba) haufahamu kwa undani mpango huu, lakini kwa hatua yake ya kutetea watuhumiwa, hasa Edward Lowassa na Andrew Chenge, anaonyesha anaufahamu.”

Taarifa zinasema naye mtoto wa Kikwete, Ridhiwani Kikwete anahusika kumdhoofisha baba yake. Zinasema Ridhiwani anatumiwa na baadhi ya wajumbe wa kundi hilo kufanikisha mpango huo.

MwanaHALISI limeshindwa kuthibitisha mara moja kama Ridhiwani anaufahamu kwa undani mpango wa kumuondoa baba yake ikulu, ijapokuwa kuna ushahidi wa kutosha kwamba anatumiwa.

Juhudi za kumtafuta Ridhiwani ziliambulia taarifa kwamba aliondoka Jumamosi kwenda nchi za nje.

Haikujulikana mara moja amekwenda nchi gani.

Katika kufanikisha mkakati huo, Ridhiwani amepewa kazi ya kusimika viongozi wa jumuiya za chama hasa UV-CCM.

Mgombea anayetajwa kusimikwa na Ridhiwani ni Beno Malisa ambapo katika kuhakikisha anashinda, Ridhiwani anahaha kusimika viongozi katika ngazi za chini.

“Wanataka kuhakikisha kwamba wenyeviti wote watatu (UWT, UV-CCM na Wazazi) wanakuwa wafuasi wao ili kurahisisha utekezaji wa mpango huo,” anasema kada mmoja wa CCM ambaye anaufahamu mpango huo.

Alisema, “Hii itawasaidia kupata wajumbe wengi wa CC, ili muda wa kuasi ukifika, iwe rahisi kutekeleza ajenda ya kumuondoa Kikwete na kumwacha bila wafuasi.”

“Hawa jamaa wana mkakati mkubwa bwana. Wameamua kumpeleka Ridhiwani mbele ili isionekane kwamba Beno atakuja kutumika vibaya dhidi ya Kikwete huko mbele,” alisema mjumbe mtoa taarifa.

Beno Malisa anatajwa kuwa ni mfuasi mkubwa wa Lowassa akihusishwa na mkataba wa kinyonyaji wa kitegauchumi cha UV-CCM.

Lowassa ni mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la UV-CCM ambaye alipitisha mkataba na mwekezaji bila kushirikisha wenzake katika chama, huku Malisa akitajwa kuwa ni mshirika mkubwa wa mradi huo.

Madai makuu kutoka kambi ya Lowassa katika kundi hilo ni kwamba Kikwete hakufanya jitihada za kumtetea Lowassa katika sakata la Richmond.

“Wanaamini kwamba Kikwete alikuwa na uwezo wa kumuokoa Lowassa, lakini hakumtetea. Sasa tutamuonyesha kama tunaweza kumsulubu,” taarifa zinaeleza.

Katika sakata la Richmond, MwanaHALISI liliripoti kwamba Kikwete aliamua kumtosa Lowassa akisema “waachwe wabunge wenyewe waamue.”

Tayari orodha ndefu ya wajumbe wa NEC imeandaliwa ambapo muda ukifika itatumika kufanikisha lengo hilo.

Guninita anatajwa kwamba mjenga mkakati akitumiwa na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wenye ushawishi mkubwa ndani ya CCM.

Ni Guninita aliyemtetea rais mstaafu, Benjamín Mkapa na kumkemea mbunge wa Vunjo (CCM) Aloyce Kimaro aliyedai kuwa Mkapa alifanya kazi binafsi akiwa ikulu na hivyo kukiuka maadili.

Guninita alitoa utetezi katika kikao cha NEC na wabunge mjini Dodoma.

Mwingine anayetajwa ni mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba ambaye
alimmwagia sifa Rostam Aziz kwa kile alichoita “kunusuru” kampeni za uchaguzi mdogo wa Kiteto.

Rostam alifanikisha upatikanaji wa helikopta ili kupambana na Chama cha Democrasia na Maendeleo (Chadema) kilichoasisi mtindo wa kutumia helikopta katika kampeni za uchaguzi.

Aidha, Komba anatuhumiwa kutafuna mamilioni ya shilingi za CCM, kughushi nyaraka na kubadilisha magari ya chama hicho kuwa yake binafasi. Lakini hajachukuliwa hatua kutokana na kile kinachoitwa, “kutetewa na mafisadi.”

Naye mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba aliyekuwa mtetezi mkubwa wa Lowassa naye anatajwa kutumika katika kufanikisha mpango huo.

Serukamba alirejea kilio chake kuwa Lowassa “hakupewa nafasi ya kujitetea na kwamba bunge lilimhukumu bila kupitisha hoja kwenye chama.” Alisema katika uchaguzi mkuu ujao, wananchi hawatauliza juu ya Richmond, bali utekelezaji wa sera za CCM.

Wajumbe wengine wanaotajwa ni mawaziri wa zamani Andrew Chenge na Nazir Karamagi. Wengine ni Lawrence Masha (Mambo ya Ndani ya Nchi), Dk. Emannuel Nchimbi (Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na Adam Malima (Nishati na Madini).

MAHOJIANO NA KUBENEA:

[media]http://www.klhnews.com/images/podcasts/kubenea.mp3[/media]
 
Ni vigumu kuhudhunika au kufurahia habari hii kwani kwa upande mmoja Muungwana has to go,ikiwezekana hata kesho maana 2010 ni mbali mno.Lakini kwa upande mwingine,hao mafisadi wako worse than Muungwana,na kibaya zaidi hawapangi kumuondoa Muungwana kwa sababu ameshindwa ku-deliver bali kulipa kisasi na kudumisha ufisadi wao.Siasa za Tanzania zinapitia kipindi kigumu sana.

Na hapo tumetajiwa wanasiasa tu,hatujui positions za wakuu wa vyombo vya dola (wa sasa na wastaafu) katika mkakati huo.Ikitokea mkakati huo mufilisi ukafanikiwa,God forbid,basi Muungwana hatakuwa na wa kumlaumu zaidi ya uzembe na uoga wake yeye mwenyewe.He has every ways and means at his disposal kuwashughulikia mafisadi but he chose to protect them.Alichosahau ni kwamba ushirika wa wachawi (au maharamia) haudumu.

Nimekuwa muumini mkubwa wa theory kwamba Lowassa na mafisadi wenzie could hardly wait till 2015,hasa kwa vile wanafahamu fika kuwa by then mambo kadhaa yanaweza kubadili political landscape ya Tanzania na hivyo nyota yake na wenzake kuwa imefifia.He also knows kwamba kwa vile Muungwana will have nothing to lose kama hatamsapoti Lowassa katika presidential bid yake ya 2015,anaweza kabisa kuacha kudhibiti any dirty that could be unleashed against him,especially kutokana na kushamiri kwa siasa za majitaka huko home.

Wanaoujua mtandao wanasema kwamba ni vigumu sana kwa Muungwana kuwageuka baadhi ya watu walimwingiza madarakani hasa kwa vile wanajua mengi machafu kuhusu yeye.However,mie naendelea kumwona kuwa ni dhaifu kwani urais katika nchi za dunia ya tatu ni u-mungu mtu,akiamua lolote dhidi ya yeyote linawezekana.

Tutashuhudia mengi sana kati ya sasa na 2010.Bad news is mengi hayo hayatakuwa na manufaa yoyote kwa wanyonge.At last sasa naona relevancy ya mstari "Mungu Ibariki Tanzania" kwenye our national anthem
 
UONGO: Haya ninayoyasoma bado hayaniingii akilini kwa sababu zifuatazo.

1.Sijaona lolote la maana alilolifanya Kikwete kiasi kuwa ipelekee achukiwe na mafisadi
2 .Sijaona lolote analofanya Kikwete juu ya nchi yake so OP strategy ingefanywa na wasio mafisadi ndani ya CCM na wanaharakati basi ingeingia akilini.

Ridhiwani yuko smart, lakini pia sio mtu wa kutisha au kuwa eti ni fala kiasi hicho. Ridhwani ni mmoja wa watu waliotaka kupindua serikali ya DARUSO chini ya president Kayombo, nikiwa waziri, nilimsoma sana na kumuelewa, sio mjinga! Japo si wa kuwa ana nguvu mno,ushabiki wa nani awe kiongozi wa UVCCM inawezekana ni utashi wake na it has nothing to do na hilo mnalolisema.

Hivyo basi gazeti la Mwanahalisi chini ya Kubenea, japo mmeshafanya mambo mengi makubwa nahuzunika kuwa inawezekana mmetugeuka. kwa sababu zifuatazo.

1. Mnataka mtuaminishe kuwa Kikwete anapigana na na mafisadi hivyo basi wako tayari kumng'oa .Kwa sababu gazeti lenu limeshaaminika, hivyo atakayesoma ataamini.

2. Kuelekea uchaguzi , ndio mnaleta taarifa kama hii.Hili hii taarifa iwe ya kuaminika , kindly provide us proof, kama ilivyo desturi yenu.

I submit

waberoya
 
Mwanzo bwana mdogo Kubene alimshika kende Simba.
Safari hii kaamua kumdandia mgongoni na kumvuta mkia pamoja na Afro yake.
Ni hatari.
Hata hivyo mageuzi ya kweli siku zote huletwa na wale wenye kuthubu tu.
Chukua 5 Kubenea.
 
UONGO: Haya ninayoyasoma bado hayaniingii akilini kwa sababu zifuatazo.

1.Sijaona lolote la maana alilolifanya Kikwete kiasi kuwa ipelekee achukiwe na mafisadi
2 .Sijaona lolote analofanya Kikwete juu ya nchi yake so OP strategy ingefanywa na wasio mafisadi ndani ya CCM na wanaharakati basi ingeingia akilini......Hivyo basi gazeti la Mwanahalisi chini ya Kubenea, japo mmeshafanya mambo mengi makubwa nahuzunika kuwa inawezekana mmetugeuka. kwa sababu zifuatazo.

1. Mnataka mtuaminishe kuwa Kikwete anapigana na na mafisadi hivyo basi wako tayari kumng'oa .Kwa sababu gazeti lenu limeshaaminika, hivyo atakayesoma ataamini.

2. Kuelekea uchaguzi , ndio mnaleta taarifa kama hii.Hili hii taarifa iwe ya kuaminika , kindly provide us proof, kama ilivyo desturi yenu.

I submit

waberoya

Unless nimekuelewa vibaya,sijaona mahala popote katika habari hiyo ambapo Mwanahalisi inataka kutumia kuaminika kwake kumfanya Kikwete naye aaminike machoni mwa Watanzania.Had that been the case,Salva Rweyemamu asingelishutumu na kudai habari hiyo ni uzushi.

Kikwete hachukiwi na mafisadi kwa vile kuna la maana alilowafanyia Watanzania bali mafisadi wanamchukia kwa sababu zao binafsi.Kama huzijui,moja ni imani ya Lowassa kuwa JK hakumtetea kwenye ishu ya Richmond,na nyingine ni tamaa ya madaraka.Kuhusu proof,ushaambiwa kwamba Mwanahalisi wako radhi kupelekwa mahakamani kuthibitisha walichoandika.Hawa watu sio wapumbavu kama unavyofikiri kwani wanafahamu fika madhara ya "kuzua" ishu nzito kama hiyo.
 
UONGO: Haya ninayoyasoma bado hayaniingii akilini kwa sababu zifuatazo.

1.Sijaona lolote la maana alilolifanya Kikwete kiasi kuwa ipelekee achukiwe na mafisadi
2 .Sijaona lolote analofanya Kikwete juu ya nchi yake so OP strategy ingefanywa na wasio mafisadi ndani ya CCM na wanaharakati basi ingeingia akilini.

Ridhiwani yuko smart, lakini pia sio mtu wa kutisha au kuwa eti ni fala kiasi hicho. Ridhwani ni mmoja wa watu waliotaka kupindua serikali ya DARUSO chini ya president Kayombo, nikiwa waziri, nilimsoma sana na kumuelewa, sio mjinga! Japo si wa kuwa ana nguvu mno,ushabiki wa nani awe kiongozi wa UVCCM inawezekana ni utashi wake na it has nothing to do na hilo mnalolisema.

Hivyo basi gazeti la Mwanahalisi chini ya Kubenea, japo mmeshafanya mambo mengi makubwa nahuzunika kuwa inawezekana mmetugeuka. kwa sababu zifuatazo.

1. Mnataka mtuaminishe kuwa Kikwete anapigana na na mafisadi hivyo basi wako tayari kumng'oa .Kwa sababu gazeti lenu limeshaaminika, hivyo atakayesoma ataamini.

2. Kuelekea uchaguzi , ndio mnaleta taarifa kama hii.Hili hii taarifa iwe ya kuaminika , kindly provide us proof, kama ilivyo desturi yenu.

I submit

waberoya

Simply idiotic!
 
Well binafsi wla sishangai kitu. Mume yeyote anayetumia muda mwingi nje kuliko nyumbani mara nyingi hupokewa na wataalam kuitunza nyumba...

Kikwete hana muda na mkewe mama yetu Tanzania...kila siku huja na visingizio asipokwenda nje kufanya kazi tutakula nini?....

Kosa kubwa!... ni muhimu kwa mwanaume kufahamu jinsi mwanamke anavyofikiria.. na jinsi ya kupanga priorities, kuna muda wa kazi na muda wa kupumzika nyumbani na familia...

Kifupi ni kwamba hata bila taarifa hii nina hakika Kikwete ameanzakuchokwa na Watanzania- hata kama anaifanya kazi nzuri kwa mtazamo wake. Na kuna mabingwa nje wanasubiri tu akosee wapate kudandia, Tanzania sio dada yake Lowassa wala Rostam Aziz hakuna haramu kumzunguka Kikwete.

Kuhusiana na Ridhwan kusema kweli hapo kidogo inanipa shida sana kwa sababu huyu ndiye kipenzi cha Kikwete ktk kutazama mafanikio ya watoto wake. Sidhani kama Ridhwan anaweza kupindua kwa baba yake kwa sababu ya watu kama Lowassa na Rostam ambao hana hata mazoea nao ya karibu.
 
UONGO: Haya ninayoyasoma bado hayaniingii akilini kwa sababu zifuatazo.

1.Sijaona lolote la maana alilolifanya Kikwete kiasi kuwa ipelekee achukiwe na mafisadi
2 .Sijaona lolote analofanya Kikwete juu ya nchi yake so OP strategy ingefanywa na wasio mafisadi ndani ya CCM na wanaharakati basi ingeingia akilini.

Ridhiwani yuko smart, lakini pia sio mtu wa kutisha au kuwa eti ni fala kiasi hicho. Ridhwani ni mmoja wa watu waliotaka kupindua serikali ya DARUSO chini ya president Kayombo, nikiwa waziri, nilimsoma sana na kumuelewa, sio mjinga! Japo si wa kuwa ana nguvu mno,ushabiki wa nani awe kiongozi wa UVCCM inawezekana ni utashi wake na it has nothing to do na hilo mnalolisema.

Hivyo basi gazeti la Mwanahalisi chini ya Kubenea, japo mmeshafanya mambo mengi makubwa nahuzunika kuwa inawezekana mmetugeuka. kwa sababu zifuatazo.

1. Mnataka mtuaminishe kuwa Kikwete anapigana na na mafisadi hivyo basi wako tayari kumng'oa .Kwa sababu gazeti lenu limeshaaminika, hivyo atakayesoma ataamini.

2. Kuelekea uchaguzi , ndio mnaleta taarifa kama hii.Hili hii taarifa iwe ya kuaminika , kindly provide us proof, kama ilivyo desturi yenu.

I submit

waberoya

Hayo Maneno SIYAELEWI KABISA."Kuwa yuko smart,Siyo wa kutisha,halafu wakati huohuo alitaka kupindua seriikali ya kayombo.Sasa wewe bwn msomi wa chuo kikuu,tena waziri unamaanisha nini" Mtu hatishi halafu alitaka kupindua serikali,halafu unakiri ni smart.Kazi kwelikweli
 
Swali ni je makala hiyo ni ya kichochezi? Je inatishia mapinduzi ya kijeshi au namna yoyote ile kuashiria kuondolewa kwa nguvu kwa JK? Je inamchongonisha Kikwete na viongozi wenzake wa CCM au na familia yake? Je inatosha kulifanya gazeti la Mwanahalisi lifungiwe kama inavyotarajiwa?
 
Simply idiotic!

Hewala baba, asante ila sijatukana nimeweka mawazo yangu wewe premium member mawazo yako siyo idiotic.Nimejenga hoja kutokana na habari, niliposoma. Thanks again, hoja yako nzuri!
,Salva Rweyemamu asingelishutumu na kudai habari hiyo ni uzushi.
Kikwete hachukiwi na mafisadi kwa vile kuna la maana alilowafanyia Watanzania bali mafisadi wanamchukia kwa sababu zao binafsi.Kama huzijui,moja ni imani ya Lowassa kuwa JK hakumtetea kwenye ishu ya Richmond,na nyingine ni tamaa ya madaraka.Kuhusu proof,ushaambiwa kwamba Mwanahalisi wako radhi kupelekwa mahakamani kuthibitisha walichoandika.Hawa watu sio wapumbavu kama unavyofikiri kwani wanafahamu fika madhara ya "kuzua" ishu nzito kama hiyo.

Asante kaka, sikuwa na taarifa kuwa Rweyemamu amezipinga hizo habari, sikuwa na taarifa hiyo.Kwa maneno yako simply naweza nikondoa commenta yangu.Thanks kunifumbua macho.

Hayo Maneno SIYAELEWI KABISA."Kuwa yuko smart,Siyo wa kutisha,halafu wakati huohuo alitaka kupindua seriikali ya kayombo.Sasa wewe bwn msomi wa chuo kikuu,tena waziri unamaanisha nini" Mtu hatishi halafu alitaka kupindua serikali,halafu unakiri ni smart.Kazi kwelikweli

Pengine smart nilivyotumia hapo siyo unavyotaka wewe litumike.wala haimaanishi kama mtu hatishi siyo smart! read again friend, next time nitakuwa more clear.

waberoya
 
Njama kumng’oa
Kikwete zafichuka
• Mwanae Ridhiwani ashiriki njama
• Watuhumiwa ufisadi wajipanga

KUNDI la watuhumiwa wa ufisadi limejipanga kumng’oa Rais Jakaya Kikwete ili asigombee urais mwaka 2010, MwanaHALISI limegundua.

Taarifa zinasema tayari baadhi ya marafiki wa Kikwete wameunda kile kinachoitwa, “One-term President (OP),” ikimaanisha “Kikwete rais wa kipindi kimoja.”

Suala la Kikwete kuwa rais wa kipindi kimoja lilikuwa mkakati wa baadhi ya washirika wa Kikwete katika kundi la mtandao wakati wa kampeni za urais za 2005.

Taarifa zinawataja Edward Lowassa na Rostam Aziz kuwa viongozi waandamizi wa mtandao waliokuwa wanaendesha mkakati huo. Aliyekuwa anaandaliwa kumwondoa Kikwete alikuwa Edward Lowassa.

Hivi karibuni mkakati wa kushika chama ndiyo ulifanikisha Jacob Zuma kumuondoa Thabo Mbeki kwenye urais nchini Afrika Kusini.

Zuma aliweka mkakati wa kushika chama mara baada ya kuondolewa katika nafasi ya makamu wa rais kwa kashfa za ufisadi na rushwa.

Mara baada ya kuondolewa katika nafasi yake, Zuma alijipanga kushika uongozi wa chama cha ANC ambapo alifanikiwa kumshinda Mbeki na baadaye kumfukuza urais.

Katika CCM, taarifa zinasema, kundi lililopanga kugombea urais mwaka 2010, limekuwa likipigania kuwepo “watu wake” katika nafasi za juu za uongozi katika Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Kamati Kuu (CC).
Baadhi ya wanaotajwa kuandaliwa ni wenyeviti wa mikoa: Deo Sanga (Jaa People- Iringa), Ernest Mabina (Mwanza) na Khamis Mgeja (Shinyanga).

Wengine ni John Guninita (Dar es Salaam), Nawab Mulla (Mbeya), Onesmo Ngole (Arusha), William Kusila (Dodoma) na Hypolitus Matete (Sumbawanga).

Haijafahamika kwa sasa nani ameandaliwa kumrithi Kikwete baada ya Lowassa kujiuzulu wadhifa wake wa waziri mkuu kutokana na kashifa ya Richmond.

Hata hivyo, mpango wa kumg’oa Kikwete bado uko palapale, ingawa waaandaji wanaweza kubadilisha mbinu na mkakati ikiwamo hata kushirikisha watu wengine na kwa malengo tofauti.

Tayari wajumbe wa kundi hilo wamekutana katika miji ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Arusha kuweka mkakati wa kutekeleza azma hiyo. Wajumbe kadhaa wakiwamo baadhi ya mawaziri na wajumbe wa NEC walihudhuria mikutano hiyo.

Taarifa za kuaminika zinasema kikao cha karibuni kimefanyika siku chache baada ya kumalizika kwa kikao cha NEC mwezi uliopita.

Inaelezwa kwamba kwa sasa mkakati wa kundi hilo ni kusimika viongozi katika uchaguzi unaoendelea ndani ya jumuiya za CCM.

Uchaguzi huo unaendelea nchi mzima na unatarajiwa kufikia kilele chake mwishoni mwa mwaka huu.

Gazeti hili liliwasiliana na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba na kumueleza kuwa kuna kundi linotaka kumdhoofisha Kikwete kwa mtindo wa Mbeki wa Afrika ya kusini na kwamba jina lake limetajwa.

Makamba aling’aka, “Sijui kitu. Nasema sijui kitu.” Alipong’ang’anizwa kwamba itakuwaje hajui wakati yeye ni katibu mkuu wa chama, Makamba alijibu kwa sauti kali, “Nakwambia sijui kitu.”

Mjumbe mmoja wa NEC ambaye hakupenda jina lake kutajwa gazetini alipotakiwa maoni yake na gazeti hili alisema, “Inawezekana hata yeye (Makamba) haufahamu kwa undani mpango huu, lakini kwa hatua yake ya kutetea watuhumiwa, hasa Edward Lowassa na Andrew Chenge, anaonyesha anaufahamu.”

Taarifa zinasema naye mtoto wa Kikwete, Ridhiwani Kikwete anahusika kumdhoofisha baba yake. Zinasema Ridhiwani anatumiwa na baadhi ya wajumbe wa kundi hilo kufanikisha mpango huo.

MwanaHALISI limeshindwa kuthibitisha mara moja kama Ridhiwani anaufahamu kwa undani mpango wa kumuondoa baba yake ikulu, ijapokuwa kuna ushahidi wa kutosha kwamba anatumiwa.

Juhudi za kumtafuta Ridhiwani ziliambulia taarifa kwamba aliondoka Jumamosi kwenda nchi za nje.

Haikujulikana mara moja amekwenda nchi gani.

Katika kufanikisha mkakati huo, Ridhiwani amepewa kazi ya kusimika viongozi wa jumuiya za chama hasa UV-CCM.

Mgombea anayetajwa kusimikwa na Ridhiwani ni Beno Malisa ambapo katika kuhakikisha anashinda, Ridhiwani anahaha kusimika viongozi katika ngazi za chini.

“Wanataka kuhakikisha kwamba wenyeviti wote watatu (UWT, UV-CCM na Wazazi) wanakuwa wafuasi wao ili kurahisisha utekezaji wa mpango huo,” anasema kada mmoja wa CCM ambaye anaufahamu mpango huo.

Alisema, “Hii itawasaidia kupata wajumbe wengi wa CC, ili muda wa kuasi ukifika, iwe rahisi kutekeleza ajenda ya kumuondoa Kikwete na kumwacha bila wafuasi.”

“Hawa jamaa wana mkakati mkubwa bwana. Wameamua kumpeleka Ridhiwani mbele ili isionekane kwamba Beno atakuja kutumika vibaya dhidi ya Kikwete huko mbele,” alisema mjumbe mtoa taarifa.

Beno Malisa anatajwa kuwa ni mfuasi mkubwa wa Lowassa akihusishwa na mkataba wa kinyonyaji wa kitegauchumi cha UV-CCM.

Lowassa ni mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la UV-CCM ambaye alipitisha mkataba na mwekezaji bila kushirikisha wenzake katika chama, huku Malisa akitajwa kuwa ni mshirika mkubwa wa mradi huo.

Madai makuu kutoka kambi ya Lowassa katika kundi hilo ni kwamba Kikwete hakufanya jitihada za kumtetea Lowassa katika sakata la Richmond.

“Wanaamini kwamba Kikwete alikuwa na uwezo wa kumuokoa Lowassa, lakini hakumtetea. Sasa tutamuonyesha kama tunaweza kumsulubu,” taarifa zinaeleza.

Katika sakata la Richmond, MwanaHALISI liliripoti kwamba Kikwete aliamua kumtosa Lowassa akisema “waachwe wabunge wenyewe waamue.”

Tayari orodha ndefu ya wajumbe wa NEC imeandaliwa ambapo muda ukifika itatumika kufanikisha lengo hilo.

Guninita anatajwa kwamba mjenga mkakati akitumiwa na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wenye ushawishi mkubwa ndani ya CCM.

Ni Guninita aliyemtetea rais mstaafu, Benjamín Mkapa na kumkemea mbunge wa Vunjo (CCM) Aloyce Kimaro aliyedai kuwa Mkapa alifanya kazi binafsi akiwa ikulu na hivyo kukiuka maadili.

Guninita alitoa utetezi katika kikao cha NEC na wabunge mjini Dodoma.

Mwingine anayetajwa ni mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba ambaye
alimmwagia sifa Rostam Aziz kwa kile alichoita “kunusuru” kampeni za uchaguzi mdogo wa Kiteto.

Rostam alifanikisha upatikanaji wa helikopta ili kupambana na Chama cha Democrasia na Maendeleo (Chadema) kilichoasisi mtindo wa kutumia helikopta katika kampeni za uchaguzi.

Aidha, Komba anatuhumiwa kutafuna mamilioni ya shilingi za CCM, kughushi nyaraka na kubadilisha magari ya chama hicho kuwa yake binafasi. Lakini hajachukuliwa hatua kutokana na kile kinachoitwa, “kutetewa na mafisadi.”

Naye mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba aliyekuwa mtetezi mkubwa wa Lowassa naye anatajwa kutumika katika kufanikisha mpango huo.

Serukamba alirejea kilio chake kuwa Lowassa “hakupewa nafasi ya kujitetea na kwamba bunge lilimhukumu bila kupitisha hoja kwenye chama.” Alisema katika uchaguzi mkuu ujao, wananchi hawatauliza juu ya Richmond, bali utekelezaji wa sera za CCM.

Wajumbe wengine wanaotajwa ni mawaziri wa zamani Andrew Chenge na Nazir Karamagi. Wengine ni Lawrence Masha (Mambo ya Ndani ya Nchi), Dk. Emannuel Nchimbi (Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na Adam Malima (Nishati na Madini).

........i would love to see this game........bring on the movie........!!
 
Mkuu TZnjema,

Between wewe na Kubenea, ninamuamini Kubenea kwa 100%, na hizi notes za mkutano wa Morogoro, ambazo hata Kubenea hana lakini tutampa, hazikuandikwa na Kubenea,

Kama una tatizo lako lingine na Kubenea, uliweke hapa lakini usichanganye mambo mkuu, wewe unajua kua hivi majuzi at one point Lowassa na Ridhiwani walikuwa pamoja US walikuwa wanafanya nini? Kwa maneno yako ninakuelewa wazi kuwa una something to do na huyo Beno au Lowassa, lakini sisi tumeamua kulikomboa taifa letu hatuogopi mtu wala maneno makali ambayo ni hewa tupu!

Punguza jazba bro! Kubali ukweli kuwa haya either huyajui au unataka kudanganya umma hapa JF kuwa-cover mafisadi, hii habari unayoililia iliandikwa Nipashe last week, Kubenea ame-etxend tu!

Hivi kaka unajua maana ya neno jazba? Maana maandishi yako siku zote ni SI Unit ya jazba sasa unapowaambia wale wasiokubali kuburuzwa na umahiri wako na so called the truth kutoka kwa kubenea tunayemjua sisi na haswa afanyavyo kazi zake kama sio jazba yenyewe ni nini. Kaka kama unalilia demokrasia lazima wewe binafsi ujenge utamaduni wa kidemokrasia na uendeshaji wako wa mijadala ni mfano wa wazi kuwa kwako wewe demokrasia ni haki tu na sio jukumu pia.

Unapofikia kuninasabisha na manyang'au kama LOWASSA eti kwa kuwa namtetea BENO huko ni kuishiwa na uvumilivu na mfano halisi wa siasa chafu ambazo wewe binafsi huzipigia kelele humu. Mimi namjua BENO...anaweza akafanya mengine lakini hili la LOWASA na mafisadi wengine katu sikubaliani nalo. Na sio kuwa nategemea habari za magazetini bali ninahakikisha kuwa kijana hafanyi kosa kama hilo hata siku moja.

Tatizo ndugu yangu unashindwa kutofautisha masilahi yako kisiasa katika hili (NAPE-MALECELA connection) na ukweli wa siasa za uchaguzi UVCCM. Mimi si muumini wa CCM lakini nakuhakikishia kuwa nafuatilia kwa karibu sana siasa za nchi yangu nikiwa nchini mwangu na sio kwa remote control kama ufanyavyo wewe.

Kaka demokrasia ni utamaduni na sio nyenzo tu ya kuhalalisha matakwa ama maoni yako.....

Tanzanianjema
 
Hihi FMES umeshawahi kuonana na KUBENEA? Ni muhimu kumuunga mkono lakini ni muhimu pia kutambua mapungufu yake......

Tanzanianjema
 
Muda umefika tunda limeivaaaaaaa sasa linataka kupasuka.

Kama serikali itang'ang'ania kushughulikia mambo haya kisiasa basi isubiri hao "Wayahudi" waje wamsulubu Muungwana ndipo watakapo amini kwamba Tanzania ina "Manabii". Lakini wakitaka kuweka mambo sawa basi wabuni mbinu ya kudhoofisha mpango huo. Ninachokiona mimi ni kwamba viongozi waandamizi serikalini ni wavivu wa kutoamini kwamba kumekucha bado wanang'ang'ania mashuka. Kalaga baaaaaaaaaahoooooooooo!!!!!
 
Back
Top Bottom