Mimi hapo sielewi kidogo
Hao polisi wametumwa na kundi la LOWASA ama JK?
Tuko wengi ndugu, naona sijui tukae kimya au tuulize wajuao watujuvye?
Kulifungia hawawezi kwa sababu baba yao Lowassa, alijaribu kila njia akiwa Waziri Mkuu, ikiwa ni pamoja na hata kumtisha Kubenea uso kwa uso, lakini hakuweza kulifungia kama alivyotishia kuwa ametumwa na muungwana,
Itakua hawa polisi waliotumwa na Makamba, ambaye binafsi anajua fika kuwa mfupa ulimoshinda fisi Lowassa, yeye atauweza wapi?
Makamba anawatuma polisi kama nani jamani? ni kweli hii taarifa? awa polisi zezeta? ,Na kwa nini Lowassa alishindwa kulifungia akiwa waziri mkuu?,
Sasa huyu Lowasa wanamuogopa nini? au ni tikitaka za kutaka kutuzingua .
Hapohapo who is Lowassa now? at that time alikuwa PM sasa yeye ni nani? ana nguvu kumshinda RAIS?
Mkuu
sasa kwanini jk asimpige chini Makamba? hapo inakua je mkuu? Na jk kwanini asitumie wasaa huo kumning'iniza Lowasa ktk swala zima la Richmonduli?
Mbona mimi naona Rais wa TZ ana nguvu sana anaweza fanya lolote na mafisadi wasifanye lolote, wakijifanya kukupindua bungeni unageuka kuwa dikiteta mstaarabu.
Unajua ni bora kuwa dikiteta mstaarabu kuliko kufanya uchaguzi unatumia fedha nyingi kufanya njama za kuiba kura na kutembeza kipigo kwa raia ama kuhatarisha maisha yao.
Maswali unayouliza , kila wengi tunajiuliza hivyo hivyo, pengine hakuna wa kutujibu, au wajuao ukweli hawajataka kutueleza, au mambo siyo kama tunavyoona.
Tusaidieni jamani maswali yenyewe ni haya yafuatayo, pengine tutarudi nyuma, lakini kwenda mbele ni lazima utoke ulipo, na tumekuwa hapa kwa sababu tumetoka nyuma
1. Taarifa ya kuwa mafisadi wanapanga njama ya kumg'oa rais, naona kama inalenga kutaka tuone kuwa JK anapingana sana na mafisadi wakati siyo hivyo!, hii taarifa bado haijakaa sawa imejaa fully of tetesi ambazo ukweli anaujua Kubenea na hao watu. kuna mtu anawezaa kufanya analyisi ya taarifa hii? tukaielewa?
2.Hivi kama inteligency ya nchi hii haijajua kuwa kuna watu wanaconspire against Kikwete basi hatuna , secret agency nchi hii! nijuavyo mimi kama kubenea aliweza kupata taarifa hizo, he is far more than usalama wa taifa, la kama usalama wa taifa walikuwa na taarifa hizi na hawakufikisha kwa Rais basi, maisha ya rais yako hatarini, hana pa kuegamia.Usalam wa taifa wako wapi? kweli hawajui ukweli?
3. Je kitu gani kinachomfanya Kikwete achelewe kuwapeleka jela hawa mafisadi? even kuwakolimba ana kila kitu cha kufanya hivyo! je ana urafiki na mafisadi? au ana uadui nao? kwa kuwapeleka jela kwanza, atalinda katiba na wajibu wake kwetu, atajiongezea credibility ambayo iko zero ground kwa sasa.
4. Hivi mtu anayeandika habari kama ile inabidi atafutwe kwa ubaya au kwa wema? I hope, polisi wanaweza kutofautisha kati ya taarifa ya kuwasaidia wao. Kama taarifa hii ya kubenea wanamtafuta kwa ubaya; basi polisi yetu imeoza na hakuna watu wa kufikiri starting from bosi wao mwema, au kuna jambo wanalomtafutia SK lingine amabalo haliusiani na taarifa ya Kikwete.
Kuna wanaosema Lowassa amekasirika kwani alitolewa uwaziri mkuu na Kikwete , ni kweli? Taarifa ya Mwakyembe ilisema waziri mkuu awajibike, he had everything to make him stay in his position, akahanaki kama mtoto, akazira, akaondoka, Kikwete alaumiwe kwa lipi hapo? mtu anasema barua ya kujiuzulu nimeshampa Kikwete, Kikwete lazima acheze kama Pele, wengi na magazeti megni yaliripoti kuwa Kikwete amevunja baraza kla mawaziri si Kweli, simply ni kwa sababu Lowassa alijiuzulu, Kikwete akasifika kila kona duniani, kumbe hakufanya lolote.
5. Reaction ya Kikwete kuhusu hii taarifa ya SK, lazima itakuwa nzuri tu-kwanza inamwongezea credibility, sympathy, popularity locally an internationally.Hivyo naamini mamlaka za polisi zingefanya mambo haya kwa upendo towards SK, awaeleze black and out, NA KUBENEA HAKUWA NA SABABU YA KUJIFICHA NA KUTAFUTA WANASHERIA KWA TAARIFA NZURI ALOYOITOA, ndio maana tunasema kuna nini kimejificha?
6.SK alikuwa na haraka gani kuandika ile taarifa? kama hakumalizia uchunguzi angesubiri , kama alikuwa amemaliza ucngunzi kwa nini asikweke complete scene, au rpofessiona za uhandishi wa nahabri zinaruhusu hivyo? au alitaka aandike nusunusu tununue gazeti? angalia sasa haya matatizo..Tumezoea kuona uthibitisho wa taarifa zake nyingi kwenye previous posts
7. Tetesi hazizuiliki, ya kuwa mwanahalisi ni la JK , amelenga kuwaua marafiki zake wa karibu might be true or wrong, lakini mambo yanavyokuwa mixed up kama sasa still watu wanajiuliza , mafisadi wamng'oe kikwete kwa lipi?, wakati mshikaji wao, wengine ni mashemeji,family friend n.k.
maswali hapo juu pengine mengine ya kitoto sana, naomba mnieleweshe, .Kama mambo ni kweli kuwa SK anatafutwa na polisi basi kuna kitu kibaya kinaendelea
SUSPECT:
Kwa sababu hawa jamaa walikuwa marafiki , na kama kweli wanahitilafiana, na kama kweli taarifa ya kubenea ni ya kweli; basi
KUNA UWEZEKANO MKUBWA POLISI, JESHI, USALAMA WA TAIFA, MAJAJI WABUNGE,WAMEGAWANYIKA KUNA WA UPANDE WA KIKWETE NA KUNA WA UPANDE WA LOWASSA, hii ni hatari na mbaya sana kwa taifa letu , anything may happen at any time! IN OTHER WORDS LOWASSA NAYE NI RAIS WA NCHI HII!
AMEACHIWA KWA DHAMANA, BADO SWALI LINGINE, KAMA NI UKWELI UTHIBITISHO HUPO, WHY TWENDE MAHAKAMANI? YAANI UKWELI LAZIMA TUSUBIRI KUUSEMA MAHAKAMANI TU?
wenu kwenye lindi la maswali, niko gizani niwashieni mshumaa kidogo angalau nione mlango nitoke nje!
waberoya