Mgongano: Serikali Vs. Mwanahalisi - Mipaka ya Maoni?

Mgongano: Serikali Vs. Mwanahalisi - Mipaka ya Maoni?

Upumzike mahali pema kaka kubenea - bado hujaandika na kuwajibu tanzania kuhusu tuhuma zako za kutembea na mke wa mtu , tuko na wewe bado -- wengine ni wanaharakati wa ukimwi na haki za wanawake

Shy what is this rubbish? mbona siku kukiwa na matatizo wewe huwa mshangiliaji? lol. Hivi unamaanisha nini kumwambia apumzike mahali pema? Shy please!
 
Upumzike mahali pema kaka kubenea - bado hujaandika na kuwajibu tanzania kuhusu tuhuma zako za kutembea na mke wa mtu , tuko na wewe bado -- wengine ni wanaharakati wa ukimwi na haki za wanawake

wapi huko?
 
Huko alipo kwa nyumba ndogo au popote alipojificha -- nimeshasema katika kesi yake ya kwanza anatakiwa ajibu na awaeleze wasomaji wa gazeti lake kuhusu tuhuma za kutembea na mke wa mtu wakati yeye yuko katika ndoa ??? , mwenye mke nae anataka amani anataka kuelewana na mke wake kubenea asitake kuvunja familia za watu kwa makusudi tunataka atueleze ukweli watanzania tumechoka
 
Shy what is this rubbish? mbona siku kukiwa na matatizo wewe huwa mshangiliaji? lol. Hivi unamaanisha nini kumwambia apumzike mahali pema? Shy please!

Kuna post ilikuwa inasema Shy ni shoga iko wapi jamani?
 
Mwanakijiji,
Mkuu kulingana na habari hii inaonyesha kulikuwepo na mawasiliano ya awali kati yake na kituoi cha Polisi kiasi kwamba aliomba muda kujisalimisha...Sasa ikiwa muda huo umepita hakutokea inakuwa swala jingine...

Kitu kimoja tu ambacho mimi kimenishangaza ktk swala ni nguvu ya Polisi ktk kutoa hukumu mara moja ktk swala linalohusu watu. Katika taarifa ya Kubenea kawataja kundi la watu kuwa lina mipango ya kumwondoa Kikwete madarakani..Hata kama kuna ukweli hili sio jambo baya ama hatari kwa nchi kwani wanatumia demokrasia ndani ya chama kupanga viongozi wengine kumrithi Kikwete...Hili tukio iweje liwe swala la kitaifa mbona hapa Canada huyu kiongozi wetu Harper alikwisha fanya hayo haya kumwondoa kiongozi aliokuwepo zamani. Na kabla yake chama cha Conserative walifanya mageuzi kama haya mara mbili tatu...

Hakuna kati yetu sisi na Polisi wenye ushahidi dhidi ya madai ya Kubenea..sisi tunadai ushahidi wake wakati sisi wenyewe hatuna ushahidi unaopingana naye!.. ndivyo tulivyo mkuu only in Tanzania.

Na sidhani kama kuna mtu kapeleka mashtaka hayo Polisi kisheria, sasa iweje atafutwe na vyombo vya usalama!. Ni kwa kiasi gani serikali wanafahamu kuhusiana na maelezo ya Kubenea kuwa ni uongo na uchochezi kuhatarisha usalama wa taifa..

Je, hao kina Rostam, Lowassa na kundi la wabunge waliotajwa majina yao wamefungua mashtaka against Kubenea na gazeti la Mwanahalisi au ndio kinachotumika hapa ni kwamba Kubenea anahatarisha usalama wa Taifa hata kama kuna ukweli ktk maneno yake.

Amini maneno yangu mkuu hapa kuna ukweli zaidi ktk maneno ya Kubenea kama ilivyokuwa kwa kina Mrema na Mtikila na wengine ambao madai yao yalikwisha siku tu walipofikishwa ktk vyombo vya Usalama. Hawakuchukuliwa hatua kwa sababu ilikuwa kweli na ndio ulikuwa mwisho wa habari na makali ya hawa jamaa...
 
Huko alipo kwa nyumba ndogo au popote alipojificha -- nimeshasema katika kesi yake ya kwanza anatakiwa ajibu na awaeleze wasomaji wa gazeti lake kuhusu tuhuma za kutembea na mke wa mtu wakati yeye yuko katika ndoa ??? , mwenye mke nae anataka amani anataka kuelewana na mke wake kubenea asitake kuvunja familia za watu kwa makusudi tunataka atueleze ukweli watanzania tumechoka

Shy, kwanini unamuuliza yeye badala ya kumuuliza huyo mke wa mtu? Kamtafute huyo mke wa mtu akueleze kuhusu tuhuma hizo ilikuwaje (kama ni kweli) aende nje ya ndoa yake.
 
Upumzike mahali pema kaka kubenea - bado hujaandika na kuwajibu tanzania kuhusu tuhuma zako za kutembea na mke wa mtu , tuko na wewe bado -- wengine ni wanaharakati wa ukimwi na haki za wanawake
shy,

unajua wewe ni mtu mzima mkuu? Ya nini kuchulia mwenzako Uchuro? Yaani unaamua kusimama upande wa shetani?

Hebu kuwa serious bwana na si lazima sana uchangie huu mjadala.Acha kuharibu thread mkuu.
 
Kuna post ilikuwa inasema Shy ni shoga iko wapi jamani?

Whaaaat? JF bwana!

Wakuu heshima mbele sana, so far bado hatuna habari za uhakika sana kuhusu Kubenea, either mahali alipo au kama ni mzima, lakini kama kawaida tuko on top of this ishu na soon tutakua na something on it,

Sasa hivi na toka jana tumekwua tunapekua kila mahali na tumeshawaarifu wote wanaohusika na amani nchini kuwa tunawa-hold responsible kwa 100% na this, kwa sababu tayari tunajua nani aliyeonekana naye dakika za mwisho kabla hajapotea, na jina tunalo.

Na ushaidi upo wa wazi, wa nini aliambiwa na Rostam, na pia alichoambiwa na Lowassa aliyedai kuwa ametumwa na muungwana kumfikishia huo ujumbe, yes kama hakuonekana ina maana kuna uhusiano wa hayo maneno na kupotea kwake, kwa sababu tunazo records.

Ninaamini kuwa Shujaaa Kubenea, ni mzima na yupo salama tena kwa 100%.

Ahsante Wakuu
 
shy,

unajua wewe ni mtu mzima mkuu? Ya nini kuchulia mwenzako Uchuro? Yaani unaamua kusimama upande wa shetani?

Hebu kuwa serious bwana na si lazima sana uchangie huu mjadala.Acha kuharibu thread mkuu.

Shy ni serengeti boys akikua ataacha!nyie endeleeni kukata nyanga!achaneni na shy!
Na yeye anadare kutalk waziwazi au sio?
 
Inaonyesha wale wote wanaotafutwa na polisi ni wapinzani wa serikali kwa namna moja au nyingine na wanaowatetea ni wapinzani tena wako vyama vya upinzani unaona tindu lissu mtetezi wa kubenea yeye si chadema ? Marando nae vile vile

sasa hawa ndio mwaka 2010 tuwape nchi ? Sasa waruhusu watu kudurufu account za watu katika mabenki wahifadhi katika makomputa yao kama kubenea ? Watu waibe wake za watu na kufanya kufuru zingine ? Nahisi bongo watu wataanza kwenda makazini na helcopter zao

watanzania jiandaeni hawa kina kubenea ndio watakuja kuomba kura mwaka 2010 na sasa hivi wanajiandalia mazingira hayo pamoja na kupanga watu wao vizuri
 
Mwanakijiji,
Mkuu kulingana na habari hii inaonyesha kulikuwepo na mawasiliano ya awali kati yake na kituoi cha Polisi kiasi kwamba aliomba muda kujisalimisha...Sasa ikiwa muda huo umepita hakutokea inakuwa swala jingine...

Mkandara, kulikuwa na mawasiliano;

a. Polisi (unknown person) alimpigia simu jana ya kumtaka aende makao makuu ya Polisi (siyo kujisalimisha). Alikuwa aende tu kuzungumza nao. Yeye akawaambia kwanza hamjui ni nani aliyepiga simu na akasema labda IGP au DCI ampigie ndio atakakwenda. Lakini baadaye baada ya kushauriwa aliamua kuwaambia kuwa hawezi kwenda bila Wakili wake.

b. Polisii wao wakang'ania aende tu na yeye akaenda kuzungumza na Wakili wake na Wakili wake akasema kuwa watakuwa tayari kwenda Jumatatu kwani yuko msibani. Hivyo muda ni wao (kwa kadiri ninavyojua) kina Kubenea waliopendekeza. Tatizo ni kuwa Jumatatu inaonekana ni mbali sana kwa Polisi (kumbuka gazeti linatarajiwa kufungiwa kesho).

c. NI kwa sababu Polisi hawataki kusubiri Jumatatu wanamtaka kwa nguvu leo hii. Hawatoa amri ya mahakama kuwa anatafutwa, ana mashtaka au ana kesi yeyote ile. Sasa hata POlisi wakija kuniambia mimi hapa "njoo Polisi" naweza kwenda nikijisikia au kubakia nakunywa togwa yangu. Ila wakija na warranti toka mahakama halali, nitawafuata au wakija na kusema wananikamaat kwa tuhuma ya kosa x,y then nitawafuata. Lakini hili la Polisi kuamua kumualika raia na kumsaka kwa nguvu ni la kupinga.

Kama wanajua Kubenea kafanya jambo fulani wanaweza kutangaza kwenye website yao Tanzania Police Force Website - Mwanzo(Home) kama wanavyowatangaza watu wengine waliotoweka kama WANATAFUTWA NA POLISI.

Kama Polisi watafuata utaratibu wa mahakama na sisi tutawaunga mkono ili sheria kweli ifuate mkondo.
 
mwanakijiji wewe unataka tufuate kama nyerere alivyosema mwaka ule anaachia ngazi alisema hivi

tumetawala zaidi ya miaka 20 bwana tumefanya mengi mabaya na mazuri lakini tuache mabaya tufuate mazuri na tuendeleze hayo hayo basi tufanye hivi
 
Huko alipo kwa nyumba ndogo au popote alipojificha -- nimeshasema katika kesi yake ya kwanza anatakiwa ajibu na awaeleze wasomaji wa gazeti lake kuhusu tuhuma za kutembea na mke wa mtu wakati yeye yuko katika ndoa ??? , mwenye mke nae anataka amani anataka kuelewana na mke wake kubenea asitake kuvunja familia za watu kwa makusudi tunataka atueleze ukweli watanzania tumechoka

Sasa wewe Shy tabia zako kama hizi unazoonesha hapa ndizo zinazosababisha watu wengine wakuanzishie thread kama hii:

https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/18756-yona-maro-ni-shoga.html
.

Hata kama ni kweli huyo Kubenea katembea na mke wa mtu, wewe ni mwanaume na mke si wako, wivu wa nini? Sisi tunajadili ishu tofauti kabisa hapa, bado wewe unalia wivu kisa Kubenea kachukua mwanamke mwingine. Hebu wanaoweza kumsaidia huyu Shy wamsaidie naona ana shida nyingine kabisa!
 
c. NI kwa sababu Polisi hawataki kusubiri Jumatatu wanamtaka kwa nguvu leo hii. Hawatoa amri ya mahakama kuwa anatafutwa, ana mashtaka au ana kesi yeyote ile. Sasa hata POlisi wakija kuniambia mimi hapa "njoo Polisi" naweza kwenda nikijisikia au kubakia nakunywa togwa yangu. Ila wakija na warranti toka mahakama halali, nitawafuata au wakija na kusema wananikamaat kwa tuhuma ya kosa x,y then nitawafuata. Lakini hili la Polisi kuamua kumualika raia na kumsaka kwa nguvu ni la kupinga.

Mzee Mwanakijiji,

Unaweza kufafanua hilo? Polisi wanahitaji amri ya mahakama kumkamata mtu?

Najua wakitaka kumpekua mtu ndio wanahitaji seach warrant lakini hivi hata kukamata mtu au kumwita mtu kwa ajili ya kumhoji wanahitaji kibali cha mahakama?

Polisi kikawaida wakikupa muda shukuru, tafuta wakili wako na nenda kawaone, vinginevyo wanakutoa ndani uchi.
 
mwanakijiji wewe unataka tufuate kama nyerere alivyosema mwaka ule anaachia ngazi alisema hivi

tumetawala zaidi ya miaka 20 bwana tumefanya mengi mabaya na mazuri lakini tuache mabaya tufuate mazuri na tuendeleze hayo hayo basi tufanye hivi

I'm sorry, hakusema hivyo.
 
Mwanakijiji,

Mkuu navyofahamu mimi Polisi wanaweza kukuita Kituoni kwa ajili ya kuchukua maelezo yako kuhusiana na swala fulani bila warrant kwa sababu haupo chini ya usalama (under arrest). Na unaposhindwa kufika ndipo wao huchukua warrant na kuja ofisini ama nyumbani kukutafuta, hivyo hapa tulipo hakuna kati yetu anayefahamu kama sasa hivi wanayo hiyo warrant ama hawana. Kumbuka tu Bongo warrant inaweza kutolewa kama cheti cha ndoa halmashauri ya jiji...

Mimi kinachonikosha zaidi ni jinsi swala hili lilivyochukuliwa kuwa kubwa kiasi hicho... kwani kuna sheria inayokataza viongozi wa ndani wa CCM kutojenga kundi jingine dhidi kiongozi aliyepo ili uchaguzi ujao waweze kumweka mtu wao?..

Hadi hapa sioni kama Kina Lowassa walikuwa na mbinu ya KUPINDUA serikali ya Kikwete isipokuwa kumwondoa kama mgombea wa kiti cha CCM ktk uchaguzi ujao.. of which sio kuvunja sheria.

Pili hili ni swala la ndani ya chama, ndani ya Chadema wanaweza kabisa kuunda kundi la kumwondoa Mbowe ktk Uenyekiti na pengine kusimama kwa tiketi ya chama uchaguzi wa 2010. Hawavunji sheria yoyote isipokuwa sisi sote tunatazama ni kina nani wanaotaka kufanya hivyo kutoa hukumu zetu..jambo la muhimu ni wanachama wa CCM kujihadhali na kundi hili litakalo wawakilisha..Kikwete mwenyewe alijiandaa hivyo hivyo kwa miaka kibao kupingana na wana CCM wengine watakao simama kugombea Urais, Nyerere aliweza kuwatangaza kina Mwinyi na Mkapa ktk mbinu kama hizi kuhakikisha mtu fulani (kikwete na Lowassa) hawachukui kiti cha Ikulu.

Iweje hili swala liwe la kitaifa la lenye kuhitaji nguvu ya kituo cha Usalama hali ni mambo ya ndani ya chama!.. Magazeti yetu yaliandika mengi kuhusiana na mbinu hizi hasa wakati wa uchaguzi wa mwaka 1995 - Kikwete vs Mkapa, mbona sikuona mtu akitafutwa!
 
1. Kubenea alipoitwa na Rostam na Lowassa, kwa nyakati mbali mbali hwakumuuliza maswali kuhusu kutembea na mke wa mtu yoyote,

- Mshahara wa ukuwadi wa mafisadi, unatakiwa kuwa kifo when the times come.

2. - Mafisadi wameshikwa pabaya, interpol kwa kushikirkiana na UN, wamempa rais majina matano ya viongozi wazito wa Tanzania, ambao wengine wapo na wengine wawili wameshatoka, kuwa ni wala rushwa na wanaotakwia kuchukuliwa hatua za kisheria kama vile Tanzania tulivyokubali tulipojiunga na hilo shirika la kutokomeza rushwa dunaini, na pia huwa tunapewa hela na hayo mashirka kwa ajili ya kupigana na corruption nchini, Sasa Kikwete amemomba muda kwanza, mawili either Tanzania tutanganze kujitoa huko au awachukulie hatua za kisheria hao mafisadi, hana jinsi!

3. - Wabunge wameshapeleka azimio kwa Spika, kwamba next bunge wanataka kuanzisha sheria itayoiondoa Takukuru under rais, na kuwa resonsible kwa bunge moja kwa moja, mara tu baada ya hiyo sheria kupitishwa.

4. - Sasa hivi almost kila siku wahusika wa ufisadi huitwa kwenye vyombo vya sheria kuhusiana na ufisadi wao, mashitaka yalishatayarishwa na lists nzima, kinachusbiriwa ni uamuzi wa rais tu kazi ianze.

5. - Kiwira kufikishwa mahakamani kama kampuni, kutokana na mapendekezo ya kamati ya Bomani, nako huko tayari mashitaka yameshatengenezwa, ambako Mkapa atabanwa kama Mjasiriamali kwa sababu ndicho kilichoandikwa kwenye sheria wakati wa kulianzisha shirika hilo na walitumia anuani ya Breda.

6.- Accounts zote za Chenge zilishazuiwa siku nyingi sana, anaruhusiwa kutumia moja tu ambayo iko monitored na uwt kila wakati.

Sasa nilitaka tu kuwakumbusha wananchi wenzangu kuwa ndio maana sasa rais sasa ukimuona amechoka sana, na according to the dataz ni kwamba sasa ameamua kuanza kampeni za urais wa 2010 ndio hiyo ameanzia Mbeya, kama ni mafisadi uamuzi wa mwisho ni wake lakini kila kitu kipo ready watu wanasubiri umauzi wake tu!

Ahsante Wakuu.
 
Habari za uhakika ni kwamba Kubenea sasa hivi yuko Polisi Makao Makuu alikoenda dakika chache zilizopita akiwa na Mwanasheria, Mabere Marando, akisindikizwa na Mwandishi Ndimara Tengambwage.

Awali taarifa za kutatanisha zilieleza kwamba Polisi wamekanusha kumtafuta, baada ya Abdalah Msika, msemaji wa polisi kuwaambia waandishi wa habari kwamba hawamtafuti ni uzushi, lakini Msika baadaye akasema alikuwa nje ya mji na hajakanusha. Tusubiri tujue anaitiwa nini, na sasa waandishi kibao wako nje ya polisi wanamsubiri.
 
Hapo pazuri. Natumaini miongoni mwa wanaosubiri nje wapo wanaJF watupenyezee za fastafasta.
 
Back
Top Bottom