PostGE2025 Mgongano wa Kikatiba Wazuka Mahakama Kuu Zanzibar Katika Kesi za Wagombea Ubunge ACT

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Kikwazo cha kwanza, sijui Jamhuri ya Muungano ina kadi za turufu ngapi kuchelewesha Haki ya Kesi kuanza kusikilizwa haraka.

Michezo ya kiufudi ya kisheria ya AG Hamza Johari na wanasheria wake wa serikali

AG Jamhuri :
"Kutokana na hoja hiyo, Sekimanga aliomba Mahakama ikubali pingamizi lililowasilishwa na upande wa Serikali, akisisitiza kuwa Mahakama Kuu ya Zanzibar haina uwezo wa kikatiba kusikiliza mashauri yanayohusu mambo ya Uchaguzi wa Wabunge wa Jamuhuri".
 
Nikum

Nikumbushe tu kwamba hapa Tanzania hapana Mahakama Kuu ya JMT. Mahakama pekee ya JMT ni mahakama ya rufaa.
 
Mambo yanazidi kuwa mazito
Tutatambuana huko mbele. Kama kuna wanaolichukulia poa hili, wacha tuone. Kwa mbali naiona mahakama ya katiba ikiundwa, kwani najua hili wakuu watalififiliza lakini ACT iko makini na natarajia imejitayarisha
 
Haya matatizo aliyatengeneza J.Kikwete na Aman Karume 2010
Mawakili wa ACT Wazalendo wapo sahihi kwa kesi kusikilizwa Zanzibar kwa shauri la Wabunge wa Muungano

Katiba ya Zanzibar (1984) ina ukuu wa kimamlaka dhidi ya ile ya JMT(1977). Sheria zinazotungwa na Bunge la JMT lazima ziidhinishwe na Baraza la Wawakilishi kabla ya kutumika Zanzibar kwa mujibu wa Katiba ya Zbar. Maana yake ni kwamba Katiba ya SMZ ina ukuu dhidi ya ile ya JMT.

Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar 2010 ndiyo iliyonyang'anya Mahakama kuu ya JMT baadhi ya mamlaka. Kuna mashauri hayawezi kuletwa JMT. Ni yale yale ya Amir Jeshi Mkuu wa JMT na Amir Jeshi Mkuu wa SMZ. Yaani tuna Maamir Jeshi wakuu 2 katika Nchi moja

Mkanganyiko ni pale shauri hilo litamalizwa iwe Mahakama kuu au Mahakama kuu Zanzibar.
Wabunge wa Zanzibar wanapovuka Bahari, gharama zao ni za JMT a.k.a Tanganyika hata kama shauri lao limemalizwa Kizanzibar. SMZ haihusiki na mzigo wa gharama

Ni vurugu tupu! Tanganyika , halafu kama Wazanzibar wakitaka kuwe na serikali ya Muungano! ndogo.
Ni kama watataka kwasababu Watanganyika hawana cha kupoteza

JokaKuu
Huu Muungano una kona kona nyingi, Wakati wa Bunge la Katiba ,Mh Lissu alishawahi shauri, kwa kusema kwamba waungwana hukaa chini na kuzitatua changamoto na sio kuzibumba bumba,tusipofanya hivyo sasa,mbeleni ni KIZA, ....wacha miCCM iendelee kushupaza shingo...MUUNGANO tunaupenda na kuhuhitaji ila sio huu wa UJANJA UJANJA

Ila na ninyi ACT, Mungu anawaona, mmeshiriki kwa namna moja or nyingine kuchelewesha kupatikana kwa DEMOKRASIA ya kweli nchi Tanzania.. Matako yenu
 
Mgongano wa kikatiba umejitokeza katika Mahakama Kuu ya Zanzibar kufuatia kesi zilizofunguliwa na waliokuwa wagombea wa Ubunge kupitia Chama cha ACT-WAZALENDO kwa majimbo 19 ya Unguja

Mgongano huo umeibuka leo mbele ya Jaji Hajji Suleiman Khamis katika Mahakama Kuu ya Zanzibar iliyopo Tunguu, wakati Mwanasheria mwanandamizi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipodai kuwa Mahakama Kuu ya Zanzibar haina mamlaka ya kusikiliza mashauri ya wabunge yanayohusiana na mambo ya Uchaguzi.
View attachment 3529817View attachment 3529818
Mwanasheria wa Serikali, Bi. Nalindwa Sekimanga, akiwa miongoni mwa jopo la wanasheria kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano, alitaja vifungu mbalimbali vya kisheria, ikiwemo Ibara ya 83 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kinachobainisha kuwa mashauri yote ya uchaguzi yanayohusu Wabunge yatasikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kutokana na hoja hiyo, Sekimanga aliomba Mahakama ikubali pingamizi lililowasilishwa na upande wa Serikali, akisisitiza kuwa Mahakama Kuu ya Zanzibar haina uwezo wa kikatiba kusikiliza mashauri yanayohusu mambo ya Uchaguzi wa Wabunge wa Jamuhuri.
View attachment 3529819
Kwa upande wao, mawakili wasomi wanaowawakilisha waliokuwa wagombea Ubunge wa ACT-WAZALENDO, wakiongozwa na Wakili Msomi Omar Said Shaaban, alipinga hoja hiyo akieleza kuwa Mahakama Kuu ya Zanzibar ina mamlaka ya kusikiliza mashauri yanayohusiana na Muungano.

Shaaban alikinukuu kifungu cha 93(1) cha Katiba ya Zanzibar na kifungu cha 3(1)(a) cha sheria Na.2 ya 1985 kuwa ndio kinachoianzisha, na kuipa mamlaka Mahakama Kuu ya Zanzibar na kwamba mamlaka iliyopewa ni bila ya Kikomo (unlimited) kwa mambo yote na sheria zote zinazotumika Zanzibar ikiwemo za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizotungwa na Bunge kama ilivyo sheria ya Uchaguzi. Hivyo Mamlaka ya Mahakama Kuu Zanzibar hayaondolewi wala hayapimiwi na Ibara ya 83 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano katika ngazi ya Mahakama Kuu.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Mahakama imeahirisha kesi hizo hadi tarehe 27 Januari 2026, kwa ajili ya kutoa uamuzi juu ya pingamizi la kikatiba lililowasilishwa na wanasheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

IMETOLEWA NA IDARA HABARI NA UENEZI ACT WAZALENDO
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni use*nge mtupu, nothing more and nothing less.
 
Hakuna jipya hapa, ila mkiambiwa hakuna uchaguzi bila ya mabadiliko, mnadai mtalinda kura! Chaguzi zimekuwepo, na kesi zinafunguliwa, na mtaishia kupiga chini kama kawaida, na bado mtafanya hivi hivi hapo mbeleni. Akili ni nywele!
 
Katika kesi inayoendelea Zanzibar ya kupinga matokeo ya ubunge Zanzibar iliyofunguliwa na chama cha ACT mwanasheria mkuu wa serikali ameweka pingamizi akidai mahakama ilipofunguliwa kesi haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

ACT imefungua kesi kwenye mahakama kuu ya Zanzibar ambayo haitambuliki kwenye katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania wakati kimsingi kesi zote za kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge Tanzania zinatakiwa kufunguliwa mahakama kuu ya Tanzania.

Huu ni mwendelezo wa vitendo vya Zanzibar kufanya mabadiliko ya Tanzania bila kujali mamlaka ya serikali ya muungano na pia mgombea wao urais akiwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar alisimamia sheria hizo kikamilifu lakini ndio zinaweza kuwa anguko lao.
 
Katiba ya jamhuri ya muungano ndio sheria mama, je kwenye katiba ya muungano kuna mahakama kuu ya Zanzibar? jibu hakuna.
Ni kama kesi ya uhaini waliyofunguliwa kina Duni Haji na Maalim Sefu na wenzake ikabainika Zanzibar sio nchi kwa hiyo huwezi kufanya uhaini.
 
Kama mngetaka kufanyia kazi kauli ya Nepi mliingia kwenye uchaguzi kwa nini?
Tuliingia kwenye uchaguzi kutimiza haki yetu ya kikatiba. Kwani nyinyi muliosusia mulisusia kwanini? Na muliingia kwenye maandamano mukaiba, mukaharibu mali za umma na za watu binafsi kwanini? Hivi mkuu sawasawa?
 
Angalia mwingine anayetumia kinyeo kufikiria, kama kulikuwa na mazingira bora kwa uchaguzi huru na haki mnaenda mahakamani kufanya nini?

Tumia akili hata ya kuazima basi utatambua kulikuwa na tamko kuwa bila reforms hakuna uchaguzi. Nyie kwa kusumbuliwa na matumbo yenu mkatimiza haki yenu ya kikatiba ondokeni mahakamani.

Kupinga uchafuzi, wizi wa kura hadi mchakato wa uchaguzi kwa mwenye akili atafahamu inamaanisha nini, Iran wanaoandamana kupinga serikali dhulma. Ila nyie kwa sababu aliyeongoza mauaji ni mzanzibari mwenzenu mnakenua macho mkifurahia, wazanzibari ni masnitch.
 
kama kulikuwa na mazingira bora kwa uchaguzi huru na haki mnaenda mahakamani kufanya nini?
Kati yangu na wewe ni nani anatumia kinyeo kufikiri? Ni wapi nimekuambia kulikuwa na mazingira bora kwa uchaguzi huru na haki? Sasa tumia akili timamu kusoma na kuelewa kilichoandikwa. Nasikia pande hizo mumesoma!!
Kupinga uchafuzi, wizi wa kura hadi mchakato wa uchaguzi kwa mwenye akili atafahamu inamaanisha nini, Iran wanaoandamana kupinga serikali dhulma.
Iran wanaandamana kupinga serikali dhulma ila mulioandamana hapa muliandamana kuiba, na kuharibu mali za umma na za watu binafsi. Je munalingana?
Ila nyie kwa sababu aliyeongoza mauaji ni mzanzibari mwenzenu mnakenua macho mkifurahia, wazanzibari ni masnitch.
Haya yalitokea wakati huyo unayemuita mwenzetu akiwa ndo mkuu wa nchi. Hivi kwa mnasaba huu wakati Mkapa alipoua kule Zanzibar nanyi mulifurahia kwasababu ni Mtanganyika mwenzenu? Nikuambie tu kwamba hatujafurahi ila hatufurahishwi kunasibishwa na yaliyotokea kwasababu ya Uzanzibari au aina yoyote iwayo ya ubaguzi.
 
Kati yangu na wewe ni nani anatumia kinyeo kufikiri? Ni wapi nimekuambia kulikuwa na mazingira bora kwa uchaguzi huru na haki? Sasa tumia akili timamu kusoma na kuelewa kilichoandikwa. Nasikia pande hizo mumesoma!!

Iran wanaandamana kupinga serikali dhulma ila mulioandamana hapa muliandamana kuiba, na kuharibu mali za umma na za watu binafsi. Je munalingana?

Haya yalitokea wakati huyo unayemuita mwenzetu akiwa ndo mkuu wa nchi. Hivi kwa mnasaba huu wakati Mkapa alipoua kule Zanzibar nanyi mulifurahia kwasababu ni Mtanganyika mwenzenu? Nikuambie tu kwamba hatujafurahi ila hatufurahishwi kunasibishwa na yaliyotokea kwasababu ya Uzanzibari au aina yoyote iwayo ya ubaguzi.
Anayetumia kinyeo kufikiria bila wasi ni wewe na wazanzibari wapumbavu wenye akili kama zako sababu:

Kupinga uchafuzi na wizi ambao hata taasisi za kimataifa zikiwemo za Africa kama AU na SADC wamesema uchaguzi haukuwa huru na haki ni kawaida. Hata Iran mali zimeharibiwa na kama unafuatilia habari utaona waandamanaji wenye silaha wakishambulia askari.
Wakati wa maandamano USA kupinga kuuliwa kwa Floyd Mayweather na askari mweupe mali ziliharibiwa kama ulikuwa unatumia akili utakumbuka kama ulikuwa hujaanza kutumia kinyeo kufikiria.

Kuna chama kilisema NO reforms no election. Kwa sababu waliona kwa mazingira haya hakuna uchaguzi huru, ila kwa sababu ya ubinafsi na kutokuwa na akili na hekima mkaingia kuhalalisha huu uchafuzi.

Hakuna yeyote mwenye akili timamu aliyefurahia mauaji ya 2001 labda kama mnataka kuhalalisha haya mauaji ya Samia mzanzibari. Nchi imegawanyika kwa sababu ya Samia, nepotism, utekaji , mauaji na kupotezwa kwa wapinzani wa Samia na ufisadi mkubwa anaofanya na mwanae na watu wake wa karibu umesababisha chuki kubwa. Na maumivu ya mauaji ya Samia mzanzibari nionyeshe wazanzibari waliopinga zaidi ya kukaa kimya.

Kwa hili limesababisha mapungufu ya muungano yamulikwe, na hata ukisemaje bado mauaji yamefanywa na SAMIA mzanzibari. Ya 2001 yaliyofanywa na Mkapa mmakonde ni mauaji atakayekataa ni chizi
 
Hata Iran mali zimeharibiwa na kama unafuatilia habari utaona waandamanaji wenye silaha wakishambulia askari.
Kwa hivyo kama Iran waandamanaji wenye silaha walishambulia askari hii inahalalisha waandamanaji kushambulia askari hapa kwetu!! Mkuu umesoma sana kupitiliza. Huku kwetu tunasema "mno dhara"
Kuna chama kilisema NO reforms no election. Kwa sababu waliona kwa mazingira haya hakuna uchaguzi huru, ila kwa sababu ya ubinafsi na kutokuwa na akili na hekima mkaingia kuhalalisha huu uchafuzi.
Ni kweli na tulifanya hivyo kutumia haki yetu kikatiba. Jee mulioiba na kuharibu mulitumia akili na kufikiri kwa kinyeleo?
Hakuna yeyote mwenye akili timamu aliyefurahia mauaji ya 2001 labda kama mnataka kuhalalisha haya mauaji ya Samia mzanzibari.
Kwahivyo nyinyi muliofurahia hamuna akili timamu? Sijahalalisha mauaji. Ninachokisemea ni kuzuia mauaji yaliyofanywa na waandamanaji, kuzuia wizi, na uharibifu wa mali.
Nchi imegawanyika kwa sababu ya Samia, nepotism, utekaji , mauaji na kupotezwa kwa wapinzani wa Samia na ufisadi mkubwa anaofanya na mwanae na watu wake
Haya unayoyazungumza yamekuwa ndio sababu ya mgawanyiko awamu hii? Vipi ile iliyoitangulia hii? Hakukuwa na nepotism? Biteko na Polepole pamoja na wengine walikuwa ni Wazaramo? Bensaanane, Azori nk walipotea/walipotezwa na utawala huu? Siku zote kusema uongo kunahitaji mtu asiwe msahaulifu.
Kwa hili limesababisha mapungufu ya muungano yamulikwe
Haya ndo unayaona leo? Sisi tulishasema zamani. Nadhani pamoja na akili zako changa unajua au utakuwa umesikia yaliyotokea kwa Seif Sharif Hamadi. Huenda pia umesikia ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Nakushauri kasome kwanza kabla ya kujisifia ovyo, utaonekana kichekesho mbele za watu.
 
Kwa hivyo kama Iran waandamanaji wenye silaha walishambulia askari hii inahalalisha waandamanaji kushambulia askari hapa kwetu!! Mkuu umesoma sana kupitiliza. Huku kwetu tunasema "mno dhara"

Ni kweli na tulifanya hivyo kutumia haki yetu kikatiba. Jee mulioiba na kuharibu mulitumia akili na kufikiri kwa kinyeleo?

Kwahivyo nyinyi muliofurahia hamuna akili timamu? Sijahalalisha mauaji. Ninachokisemea ni kuzuia mauaji yaliyofanywa na waandamanaji, kuzuia wizi, na uharibifu wa mali.

Haya unayoyazungumza yamekuwa ndio sababu ya mgawanyiko awamu hii? Vipi ile iliyoitangulia hii? Hakukuwa na nepotism? Biteko na Polepole pamoja na wengine walikuwa ni Wazaramo? Bensaanane, Azori nk walipotea/walipotezwa na utawala huu? Siku zote kusema uongo kunahitaji mtu asiwe msahaulifu.

Haya ndo unayaona leo? Sisi tulishasema zamani. Nadhani pamoja na akili zako changa unajua au utakuwa umesikia yaliyotokea kwa Seif Sharif Hamadi. Huenda pia umesikia ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Nakushauri kasome kwanza kabla ya kujisifia ovyo, utaonekana kichekesho mbele za watu.
Kinyeo kinareason badala ya akili, tuonyeshe hapa nchini muandamanaji gani aliyemshambulia askari?
Punguza bangi mpumbavu wewe

Kinyeo kinaendelea kujenga hoja, mtanganyika gani aliyefurahia mauaji ya 2001 wakati wanaharakati na watetezi wa haki za wananchi walilipigia kelele tena wakiongozwa na mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu?

Mtoto, mkwe, binamu, mshenga wote wako kwenye Baraza la mawaziri, kwa hiyo Polepole mngoni alikuwa ana undigi wa damu na msukuma Magufuli?
Wewe mjinga wakati wa Magufuli tulikemea, sasa huyu muuaji wa Kizimkazi kaja kuendeleza, kwa hiyo kwa akili za kizenji huyu ana haki ya kuteka na kuua watanganyika kwa sababu yeyote ile? PUMBAVU kama Samia.

Maalim Seif aliteswa na kuuliwa na watanganyika? Mfumo wa wahafidhina wachache ndani ya CCM ndio wanaofaidika, na tatizo lako mfumo wa CCM unaona ni wa Tanganyika. Tanganyika tunaupinga mfumo huo, ila hapa wewe kwa ujinga wako unataka kuhalalisha mauaji ya dikteta Samia.
 
tuonyeshe hapa nchini muandamanaji gani aliyemshambulia askari?
Punguza bangi mpumbavu wewe
Hivi mimi ni mtumwa wa kukuonesha wewe muandamanaji? Hiyo si kazi yangu. Hapa ndo kikomo cha uwezo wako wa kufikiri!!
mtanganyika gani aliyefurahia mauaji ya 2001 wakati wanaharakati na watetezi wa haki za wananchi walilipigia kelele tena wakiongozwa na mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu?
Unaendelea kuonesha uzandiki na ujinga. CHADEMA gani iliyopiga kelele wakati kila mmoja akijifanya hayamhusu kwa vile waliouliwa ni Wazanzibari? Akili yako ya kifala inakudanganya.
Wewe mjinga wakati wa Magufuli tulikemea, sasa huyu muuaji wa Kizimkazi kaja kuendeleza, kwa hiyo kwa akili za kizenji huyu ana haki ya kuteka na kuua watanganyika kwa sababu yeyote ile? PUMBAVU kama Samia.
Unajitia kimasomaso kwamba mulikemea wakati ule. Sasa si ni nyinyi munasema leo alikuwa shujaawa taifa?
Mtoto, mkwe, binamu, mshenga wote wako kwenye Baraza la mawaziri, kwa hiyo Polepole mngoni alikuwa ana undigi wa damu na msukuma Magufuli?
Wakati ukijificha mgongo wazi kwenye tuwa la njugu, sisi tunajua yaliyokuwa yanaendelea. Biteko ni Mndengereko? Hivi unajua kweli?
Kinyeo kinareason badala ya akili, tuonyeshe hapa nchini muandamanaji gani aliyemshambulia askari?
Punguza bangi mpumbavu wewe

Kinyeo kinaendelea kujenga hoja, mtanganyika gani aliyefurahia mauaji ya 2001 wakati wanaharakati na watetezi wa haki za wananchi walilipigia kelele tena wakiongozwa na mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu?

Mtoto, mkwe, binamu, mshenga wote wako kwenye Baraza la mawaziri, kwa hiyo Polepole mngoni alikuwa ana undigi wa damu na msukuma Magufuli?
Wewe mjinga wakati wa Magufuli tulikemea, sasa huyu muuaji wa Kizimkazi kaja kuendeleza, kwa hiyo kwa akili za kizenji huyu ana haki ya kuteka na kuua watanganyika kwa sababu yeyote ile? PUMBAVU kama Samia.

Maalim Seif aliteswa na kuuliwa na watanganyika? Mfumo wa wahafidhina wachache ndani ya CCM ndio wanaofaidika, na tatizo lako mfumo wa CCM unaona ni wa Tanganyika. Tanganyika tunaupinga mfumo huo, ila hapa wewe kwa ujinga wako unataka kuhalalisha mauaji ya dikteta Samia.
Unauliza jibu? Maalim Seif aliuliwa na Watanganyika huko Tanganyika. Na hili eti hulijui!!! Mimi nazungumza mauaji na mateso aliyofanyiwa huko Tanganyika na sizungumzii CCM kama akili yako ndogo inavyokuambia.
 
Back
Top Bottom