Mgonjwa aidai TMJ, Hindu Mandal fidia ya shilingi milioni 500

Na hivi vihopsitali vilivyo mtaani wanajiita ma specialist ni vyakuogopa...Kuna hospital moja nzuri tu iko mbezi beach walimpima mtu na mashine ya ECG wakasema anatatizo la moyo anatakiwa aanze clinic muhimbili ..kufika muhimbili kwa daktari bingwa akapimwa Hana tatizo lolote la moyo...kurudia Tena sehemu nyingine hana...
 
Ni
Kweli kaka, uko sahihi katika hili.
 
Duh! Hatari.

Kwenye nchi za dunia ya kwanza kuna wanasheria waliosomea masuala ya Afya, kesi kama hizi ni kawaida.

Laiti huku kwetu kungekuwa na hao watu ili wasaidie wale masikini, mahakama zingejaa kesi hizo.

Kiukweli watumishi kwa kiasi fulani huwa hatuwatendei haki wagonjwa, kwa kusudi au kukosa umahiri.
 
Dah!! So sad!! Na hapo ni kwa kuwa alikuwa na kauwezo kifedha kidogo, je angekuwa kama mimi hapa kajambanani sijui kama angekuwa hai!!
 
Kisheria daktari akikufanyia popfessional negligence abakua liable kukulipa kwaio unaishitaki hospitali na daktari husika lazima ulipwe hela...😀😀😀
Ni sawa, lakini kwa umasikini, ufukara, utahira wa linchi kapuku kama Tanzania sio sawa kuwashitaki.

Kaka kuna madaktari wengi sana nawafahamu wamesoma kwa shida mno wametoka familia za tabu sanaa hadi leo wako hapo ni neema tu siamini sana kama ni uzembe tusiwashitaki
 
Hii inawakuta wengi tu,, mdogo wangu poly clinic moja walimwambia mishipa ya moyo imetanuka..

Mtoto alilia hii siku,, mtu mmoja akanambia tafuteni vipimo vya hosp kama 3.

Nikaenda nae NSK Arusha, wakampima majibu ni hamna shida yoyote kwenye moyo… likizo akaenda Dar akapima tena Rabininsia, hamna kitu.

Sasa sijui wanakwama wapi
 
Kesi kama hizi zinatakiwa kua nyingi sana..umasikini wa mtu au kusoma kwa shida hauna uhusiano wowote ule katika kutoa professional advice na kutekeleza majukumu hayo, ukitoa ushauri wa kitaalamu kimakosa unatakiwa uwajibike..miezi kadhaa nyuma humu ndani kuna jamaa alipoteza mtoto wake kwa uzembe wa hospitali kwaio kesi zikikomaa zikawa nyingi mtu atajikita katika kufanya tafiti kuliko kuanza kubahatisha...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…