Nipo hapa Hospitali ya Taifa Muhimbili ya Upanga Kitengo cha Mifupa (MOI) nina mgonjwa ambaye tayari anaingia wiki ya pili tangu alazwe. Changamoto kubwa ni kuwa mgonjwa ana tatizo la mshipa uliovimba kichwani, ameshauriwa kufanyiwa upasuaji (operation) haraka.
Hata hivyo, hadi sasa hatujapewa tarehe maalum ya kufanyiwa upasuaji huo. Kila tunapouliza, tunaambiwa kuna changamoto ya vifaa kutokuwa tayari au havijaingizwa kwenye mfumo.
Hali hii inatupa wasiwasi mkubwa, kwa sababu muda unaendelea kwenda huku mgonjwa akiwa hajapatiwa matibabu anayohitaji.
Mbali na hilo, mgonjwa amewekwa kwenye chumba ambacho gharama yake ni kubwa sana zaidi ya shilingi laki moja kwa siku. Kadri siku zinavyosonga mbele, gharama zinaendelea kuongezeka, huku bado hatujui ni lini atapata huduma ya upasuaji.
Ufafanuzi wa Taasisi ~ MOI: Huduma za upasuaji zinaendelea kama kawaida, mwenye changamoto afike ofisini tumsaidie
Mpaka sasa tumeshatakiwa kulipia Shilingi 1,750,000/= hiyo ni gharama ya matibabu yanayoendelea, hapo bado hatujaletewa bili ya Kitanda, na pia hatujajua gharama ya upasuaji itakuwaje.
Kwa kweli hali hii inatupa mzigo mkubwa kifedha na kisaikolojia. Tunaomba uongozi wa hospitali pamoja na mamlaka husika kulifanyia kazi suala hili haraka, ili mgonjwa aweze kupata matibabu kwa wakati na kuepuka madhara zaidi.