DOKEZO Responded Mgonjwa wetu anateseka akisubiri upasuaji wiki ya pili sasa MOI, wanasema “Kuna changamoto ya vifaa”

DOKEZO Responded Mgonjwa wetu anateseka akisubiri upasuaji wiki ya pili sasa MOI, wanasema “Kuna changamoto ya vifaa”

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Majengo na vifaa vinapatikana kwa pesa ya CCM?

Wafanyakazi hulipwa kwa fedha za CCM?

Kama ndivyo, uko sawa maoni Yako

Kama hawalipi CCM ni Kodi za watanzania, hizo za kulipia sijui matibabu sijui gharama za nini huko ni hesabu Gani hizo chief

Matibabu ilitakiwa iwe buuure kabisa, kwa sababu, si vidonge, sijui vifaa, majengo na hata posho za watumishi, Kodi za wananchi hufanya yote hayo
Huwa nawauliza watu kwanini watu walipie hela kwenye hospitali ya serikali,tena malipo makubwa kuliko Aga Khan wakati mishahara,dawa,majengo,vifaa vyote vinalipiwa na kodi ya wanachi?
 
Poleni na mgonjwa
Basi niwaambie, wabongo wengi huwa wanapenda kusema Ulaya matibabu ni bure, ukweli sio bure
Kila mwananchi awe mfanyakazi au kajiajiri lazima alipie kila mwezi kitu inaitwa kama huku NSSF, na hii kwao ni sheria kwa hiyo lazima ifuatwe
Yaani ukikutwa hulipii ni bonge la msala
Sasa huku kwetu haiwezekani, kuna bodaboda, mama ntilie, muuza mifuko, muuza chips, sijui muunga line, na majoblesi kibao, na hawa wote hawachangii chochote, itawezekana vipi matibabu yawe bure au rahisi?
Kama hao bodaboda na nani na nani uliowataja wako visible inawezekana kuchangia kwa lazima ila labda wawe ni invisible !

Watu wengi hawana kazi watashindwaje kufanya kazi hiyo ya kulipisha watu pesa hizo unazo zisema zinalipishwa huko Ulaya ,

Na hata kama hawatalipa watu wooote wa Nchi hii lakini wale watakaolipa itatosha kufanya kama Ulaya !
Kwa sababu siku zote wanaougua na kwenda kutibiwa hospitali ni wachache sana kulinganisha na Idadi ya Watanzania watakaochangia !
 
Huenda wanaka uwape rushwa maana nyakati hizi rushwa ni mmmm
 
Hii nchi bila waziri kutoa tamko vitu haviendi. Bila kurefusha mkono hutoboi hata kwenye matibabu.
 
Poleni sana mkuu,
Huduma ya kwanza kupunguza maumivu kusanya mimea ya gotukola na voacanga Africana mumuandalie chai. Tuwasiliane kwa 0713 039 875
 
Back
Top Bottom