Mtazamo wangu.
Nilikuwa muumini wa Mgote, nilisoma pale Heat, Wave na Electronics(kutokana na ukata niliweza kumudu hizo topic tu).
Kwa Muddy nilisoma hasa pindi za ofa na kuibia.
Mgote anajua kuandaa notes, kufundisha hapana.
Muddy alikuwa anajua kufundisha, hakuwa anajua kuandaa notes.
Kutokana na Elimu yetu:
Notes za Mgote zilisheni kila kitu(kutoka vitabu mbali mbali) ambapo zinamrahisishia mwanafunzi kupata material mengi tofauti tofauti na kuweza kujisomea.
Notes za Muddy zilikuwa kiduchu sana, alikuwa anafundisha unaelewa lakini concept zilikuwa chache sana kwenye notes, jambo ambalo linamfanya mwanafunzi asiwe na concept kwa kina.
Advance Physics inahitaji bidii ya kusolve mara kwa mara na kusoma concept zake.
Kukariri hakukwepeki hata kama utaelewa, na elimu yetu inahitaji kufaulu ambapo msingi mkuu ni kukariri madude.
Hivyo basi, kwa mimi niliyehitaji kuifaulu Physics kwa mbinu zangu niliamua kusoma notes za Mgote badala za Muddy baada ya kugundua kuwa Notes za Muddy haziwezi kunisaidia kujibu maswali ya Physics ambapo swali lazima lianzie kwenye concept kabla hauijalisolve.
Mgote na Muddy ni Walimu wenye uwezo tofauti na style tofauti ya kufundisha, hawafanani ila wanamchango kwa mwanafunzi kulingana na matakwa ya mwanafunzi mwenyewe.
Juhudi za kusoma Notes za Mgote zilinibeba kwenye Necta maana Biology nilikuwa kibonde, na nisingekomaa na Physics sidhani kama ningefika MUHAS kwa masomo ya Elimu ya Juu