Mgote physics anakariri vitu, haelewi

Mgote physics anakariri vitu, haelewi

Physics mwamba alikuwa Elias kihombo

Anaelewa madude ya physics nje ndani.. na anameza nje ndanii..

Kwenye kuelewa anashinda na kwenye kumeza anashinda

Nina uhakika Elias pepa ya Advance physics ya popote duniani anapata A
Alipata 100% Physics ya Advance 2003...NECTA wakaogopa wangeonekana wajinga wakasema amepata 98

Kingine utafikiri topic ya Organic Chemistry ametunga yeye na unajua ilivyo ngumu
 
kitu kimoja nimekua nikijiuliza sana hawa walimu wazuri sana wa twisheni za masomo mbali mbali ya sekondari enzi hizo, mbona wengi waliwahi kuondoka na waliondoka wakiwa vijana wadogo?!?

Inawezekana yaliyokua yakisemwa ni kweli kuwa walikua wakipika na kupakua mapishi yao!?!
 
Mgote kanifundisha na nimefanikiwa kupiga nae stories mara kadhaa ila ni mtu mweupe sana kwenye mambo ya nje tofauti na ufundishaji. Simsemi vibaya ila ni mtu ambaye hata application ya kile anachofundisha hajui kabisa kabisa. Nilimshangaa tofauti na walimu wenzake wa masomo mengine ambao angalau wanaweza jadili kitu wanachofundisha nje ya masomo.

Hilo la kukaririsha kila aliyesoma kwake mwenye uelewa na dunia inaendaje anajua, utaamua wewe ukariri au uelewe
Aisee
 
Nilikuwa muumini wa muddy physics, pamoja na kuwa jamaa hakuwa na exercise nyingi na kusolve maswali kama mgote ila jamaa alikuwa na uelewa mkubwa sana na physics...Mgote yeye amekariri tu na anaamini katika ule msuli tembo.
Kinachombeba mgote ni aina ya sylabus ya bongo inataka watu waliokariri maswali na sio wenye uelewa.

So utaishia kukariri na kufaulu mambo usiyoyaelewa na huwezi kuyaapply popote, ndio hawa wanaajiriwa mainjinia na GPA kubwa ila vilaza.
Muddy yeye alikuwa anakupa inspiration ya kuelewa madude..kiukweli sylabus ya bongo wanatakiwa waitwist iendane hivi ili kutengeneza wanafunzi wenye uelewa ambao wanaweza kuapply waliyosoma na kuikwamua jamii.
Sie ambao hatukupita huko kote kwenye ma tuition ila tulisoma vitabu tu alone alo e.. ma chandi.. nelkon... Etc na bado tukapita coet udsm na sasa tuko ughaibun una tuelezaje.. mind u.. tumesoma shule hzo hzo kayumba. Ohooo... Ma genius eeh
 
Nilikuwa muumini wa muddy physics, pamoja na kuwa jamaa hakuwa na exercise nyingi na kusolve maswali kama mgote ila jamaa alikuwa na uelewa mkubwa sana na physics...Mgote yeye amekariri tu na anaamini katika ule msuli tembo.
Kinachombeba mgote ni aina ya sylabus ya bongo inataka watu waliokariri maswali na sio wenye uelewa.

So utaishia kukariri na kufaulu mambo usiyoyaelewa na huwezi kuyaapply popote, ndio hawa wanaajiriwa mainjinia na GPA kubwa ila vilaza.
Muddy yeye alikuwa anakupa inspiration ya kuelewa madude..kiukweli sylabus ya bongo wanatakiwa waitwist iendane hivi ili kutengeneza wanafunzi wenye uelewa ambao wanaweza kuapply waliyosoma na kuikwamua jamii.
Wajanja tulikuwa tunasoma kwa Mudy.. material tunatumia ya mgote hata kwenye kusolve maswali [emoji23]

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Walimu wangepikwa wakaacha kucopy maswali kwenye Vitabu NECTA ,waweze kupika maswali ambayo hayapo kwenye rejea za Vitabu ndo utaona maajabu ya hapa bongo ,vijana watafeli kama kuku.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Kuku hawajawahi kufeli, wanataga mayai, supu yao ni tamu, kinyesi chao mbolea
 
Nakumbuka siku moja kwny chumba cha mtihani form five shule flani PCM nilizinguana nae huyu jamaa alikua anatabia ya kutaka kusahihisha mtihani kabla ya muda kuisha ndani ya chumba cha mtihani, yaani ndio mnaanza tu mtihani hata kama ni swali moja anataka asahihishe akanikuta nimeamka na wendawazimu wangu hiyo siku kilichotokea mpaka leo hata hyo physics sihitaji kuisikia, jamaa nimekutana nae shule mbili tofauti olevel form 3 shule nyingine na nikaja kutana nae alevel form5 shule nyingine kuna aliyo yahifadhi rohoni mwake kwa muda ila Mungu c Mjomba wake na hiyo physics yake ya kukariri ilikua inanipotezea muda na kuniletea headech japo nilikua naipenda sana na nilikua muumini wa presentation za physics asubuhi kama akina pendulum bob wazee wa oscillation ila siku hiyo hata hiyo PCM sikutaka tena kuisikia pu*#**vu kabisa
Unaona sasa
 
We umefanya nini remarkable kwenye iyo physics uliyoelewa au unakuja tu kwenye jukwaa kulalama?
We need changes kwenye edu system. Nyie mnavyokariri haiwasaidii chochote.
Mimi sijafanya kitu remarkable kwenye physics, lakin kupitia phylosophy ya kuelewa kuliko kukariri nmefanya vitu remarkable kazini
 
Ko unaona mfumo uwaangusha watu wote ila umekubeba wewe tu huko kazini kwako? Unaweza kueleza jambo ambalo umelifanya kazini liwe limemake difference kutokana na kuelewa kwako shuleni?

Licha ya mfumo wa elimu kuwa mbovu kuna watu wengi wamefanya vitu vingi vizuri na remarkable na wamepitia mfumo wetu huu wa elimu lakini jitihada zao zikawabeba.

Kuna watu waliotoka hapa wakapata nafasi vyuo vya nje na wakafanya vizuri vyuoni na kazini kwa msingi wa elimu yetu ya hapahapa.

Kabla ya kuja hapa kulamimika kuwa watu walifaulu kwa kukariri na wewe ulielewa tuelezee wewe ulieelewa umefanya nini cha tofauti sio kuleta blah blah.
 
Physics mwamba alikuwa Elias kihombo

Anaelewa madude ya physics nje ndani.. na anameza nje ndanii..

Kwenye kuelewa anashinda na kwenye kumeza anashinda

Nina uhakika Elias pepa ya Advance physics ya popote duniani anapata A

Hahaaaaa umenikumbusha mbaali sana
Mwamba Kihombo a.k.a kimangara

Mungu amtunze sana jamaa bila yeye sijui physics ingeniua kifo gani asee..somo gumu sana alafu muda hautoshi kumaliza syllabus ebwaana noma kwelii..!

Kihombo alikunja physics yote ndani ya miezi miwili
Tulikuwa tunaanza pindi saa 10 alfajiri mpk usiku saa4
Jumlisha baridi la kule Iringa enzi hizo ilikuwa mpk -2 C

Ilikuwa kipindi kigumu sana kene maisha ya shule
Lkn nashukuru Mungu,Hard work pays leo naenjoy tu kene viyoyozi si haba. Elimu imetukomboa
 
Na hii ni sababu kubwa kwanini tokea 61 mpaka leo kuna vijiji hakuna maji, hospitali, shule, umeme, barabara wala vyoo
Hata haviusiani kbsa kukarii na kukosekana na vyooo na maji kijini ndio sababu hzo za kukarii

Let me tell you kuwa kila kitu wenzetu white wameshafanya na ndio maana tunatumia vitabu vyao kusoma na kutafafuta kuelewaaa
Hapa tuliko elimu inapimwa siyo kwa uelewa Ni kwa ufaulu tu sas wee tafuta kuuelewaa na mwezako ameze afaulu mtiani ndio utaona tafauti
 
Ko unaona mfumo uwaangusha watu wote ila umekubeba wewe tu huko kazini kwako? Unaweza kueleza jambo ambalo umelifanya kazini liwe limemake difference kutokana na kuelewa kwako shuleni?

Licha ya mfumo wa elimu kuwa mbovu kuna watu wengi wamefanya vitu vingi vizuri na remarkable na wamepitia mfumo wetu huu wa elimu lakini jitihada zao zikawabeba.

Kuna watu waliotoka hapa wakapata nafasi vyuo vya nje na wakafanya vizuri vyuoni na kazini kwa msingi wa elimu yetu ya hapahapa.

Kabla ya kuja hapa kulamimika kuwa watu walifaulu kwa kukariri na wewe ulielewa tuelezee wewe ulieelewa umefanya nini cha tofauti sio kuleta blah blah.

Kweli jamaa anajifanya deep sana
Unataka uelewe physics yenyewe unafundishwa theory tena kaikuta kuanzia o-level .aache janja ukikomaa kutaka kuelewa physics kama akina Eistern humalizi hata mechanics tu kwa miaka miwili na Necta ikija lazima ikuone.Physics kariri inahitajika ikibidi na zile practical foji la sivyo kibongo bongo hutoboi[emoji28]
 
Nilikuwa muumini wa muddy physics, pamoja na kuwa jamaa hakuwa na exercise nyingi na kusolve maswali kama mgote ila jamaa alikuwa na uelewa mkubwa sana na physics...Mgote yeye amekariri tu na anaamini katika ule msuli tembo.
Kinachombeba mgote ni aina ya sylabus ya bongo inataka watu waliokariri maswali na sio wenye uelewa.

So utaishia kukariri na kufaulu mambo usiyoyaelewa na huwezi kuyaapply popote, ndio hawa wanaajiriwa mainjinia na GPA kubwa ila vilaza.
Muddy yeye alikuwa anakupa inspiration ya kuelewa madude..kiukweli sylabus ya bongo wanatakiwa waitwist iendane hivi ili kutengeneza wanafunzi wenye uelewa ambao wanaweza kuapply waliyosoma na kuikwamua jamii.
Kuna jamaa mmoja (Kiaumbi kama sijakosea)ila alijulikana kwa jina la "NELKON" alikua na centre yake pale St. Joseph Moshi Mjini. Hakuna swali lolote asilolijua kutoka versions zote za Nelkon.
 
Huko Arusha kuna jamaa angu nae anaitwa doctor jamaa alikuwa vzr kwenye solving ila jamaa six kapiga 3 ya mwisho kaenda St Joseph kapiga kadisco Kisha kurud katk siasa za CDM Kisha akacha siasa sas amerudi na tuition mkp sas
 
Ko unaona mfumo uwaangusha watu wote ila umekubeba wewe tu huko kazini kwako? Unaweza kueleza jambo ambalo umelifanya kazini liwe limemake difference kutokana na kuelewa kwako shuleni?

Licha ya mfumo wa elimu kuwa mbovu kuna watu wengi wamefanya vitu vingi vizuri na remarkable na wamepitia mfumo wetu huu wa elimu lakini jitihada zao zikawabeba.

Kuna watu waliotoka hapa wakapata nafasi vyuo vya nje na wakafanya vizuri vyuoni na kazini kwa msingi wa elimu yetu ya hapahapa.

Kabla ya kuja hapa kulamimika kuwa watu walifaulu kwa kukariri na wewe ulielewa tuelezee wewe ulieelewa umefanya nini cha tofauti sio kuleta blah blah.
Sijasema mimi tu ndio nimebebwa...wapo wengi sana wanafanya makubwa tena kuliko mimi mara 1000.
ila hao wanaofanya makubwa hawakufanya kwa kukariri bali walijiongeza na kuelewa mambo.
Nachosema ni kuwa wengi zaidi na asilimia kubwa ya watu hawajiongezi na hawafanyi makubwa kwasababu ya mfumo wa kukaririshwa.
Mfumo ukibadilika, Tutaona makubwa zaidi yakifanywa na wengi zaidi.
Hebu jaribu kuelewa basi.
 
Back
Top Bottom