Mgote physics anakariri vitu, haelewi

Mgote physics anakariri vitu, haelewi

Necta yetu tulikutana na swali moja lipo kwenye kitini chake la Projectile motion ila nililikimbia maana sio mchezooo[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Mgote sio wa kusoma mara 100 usome chandy...
Mkuu ukaamua uchimbe,ukafyata mkia mbele ya projectile motion 😂😂,ila Advanced Physics shikamoo
 
Nakumbuka siku moja kwny chumba cha mtihani form five shule flani PCM nilizinguana nae huyu jamaa alikua anatabia ya kutaka kusahihisha mtihani kabla ya muda kuisha ndani ya chumba cha mtihani, yaani ndio mnaanza tu mtihani hata kama ni swali moja anataka asahihishe akanikuta nimeamka na wendawazimu wangu hiyo siku kilichotokea mpaka leo hata hyo physics sihitaji kuisikia, jamaa nimekutana nae shule mbili tofauti olevel form 3 shule nyingine na nikaja kutana nae alevel form5 shule nyingine kuna aliyo yahifadhi rohoni mwake kwa muda ila Mungu c Mjomba wake na hiyo physics yake ya kukariri ilikua inanipotezea muda na kuniletea headech japo nilikua naipenda sana na nilikua muumini wa presentation za physics asubuhi kama akina pendulum bob wazee wa oscillation ila siku hiyo hata hiyo PCM sikutaka tena kuisikia pu*#**vu kabisa
 
Yeah, elimu yetu pia tunatakiwa tuishape iende hivi..
Tukiendelea na hii system ya kukaririshana, tutaendelewa kutawaliwa na wazungu na wachina milele daima
We umefanya nini remarkable kwenye iyo physics uliyoelewa au unakuja tu kwenye jukwaa kulalama?
 
Bro mbona jamaa ni mzuri tu na ametoa T.O za A level phyzo, huenda ni kichwa chako tu bro... Japo anacopy sana chandy

Mengine unapotezea ilimradi mkono unaenda kinywani
 
Samahani napita tu... nimeingia njia siyo leo
 
Mtazamo wangu.

Nilikuwa muumini wa Mgote, nilisoma pale Heat, Wave na Electronics(kutokana na ukata niliweza kumudu hizo topic tu).

Kwa Muddy nilisoma hasa pindi za ofa na kuibia.

Mgote anajua kuandaa notes, kufundisha hapana.

Muddy alikuwa anajua kufundisha, hakuwa anajua kuandaa notes.

Kutokana na Elimu yetu:
Notes za Mgote zilisheni kila kitu(kutoka vitabu mbali mbali) ambapo zinamrahisishia mwanafunzi kupata material mengi tofauti tofauti na kuweza kujisomea.

Notes za Muddy zilikuwa kiduchu sana, alikuwa anafundisha unaelewa lakini concept zilikuwa chache sana kwenye notes, jambo ambalo linamfanya mwanafunzi asiwe na concept kwa kina.

Advance Physics inahitaji bidii ya kusolve mara kwa mara na kusoma concept zake.

Kukariri hakukwepeki hata kama utaelewa, na elimu yetu inahitaji kufaulu ambapo msingi mkuu ni kukariri madude.

Hivyo basi, kwa mimi niliyehitaji kuifaulu Physics kwa mbinu zangu niliamua kusoma notes za Mgote badala za Muddy baada ya kugundua kuwa Notes za Muddy haziwezi kunisaidia kujibu maswali ya Physics ambapo swali lazima lianzie kwenye concept kabla hauijalisolve.

Mgote na Muddy ni Walimu wenye uwezo tofauti na style tofauti ya kufundisha, hawafanani ila wanamchango kwa mwanafunzi kulingana na matakwa ya mwanafunzi mwenyewe.

Juhudi za kusoma Notes za Mgote zilinibeba kwenye Necta maana Biology nilikuwa kibonde, na nisingekomaa na Physics sidhani kama ningefika MUHAS kwa masomo ya Elimu ya Juu
 
Back
Top Bottom