Watu hawataamini kuhusu uwezo wa Mgunda kuifundisha Simba. Simba haiwezi kufundishwa na mgunda na Matola bhana.
Ushindi mfululizo wa Mgunda tuliokuwa tunauona ulitokana na saikolojia ya wachezaji mbele ya kocha mpya tu. Kila mchezaji alikuwa anacheza kwa kiwango kikubwa kuliko afya, kipato na mafundisho yao ili kutafuta namba kwa kocha mpya (mgunda).
Baada ya wachezaji wa Simba kuanza kupokea mafundisho halisi ya mgunda na matola na kupata namba za kudumu watarudi kuliko mashabiki wasikokutaka (kupoteza mechi).
Unajua kwanini? makocha wa kitanzania/waafrika wanafeli kwenye saikolojia ya wachezaji na mbinu za kufundishia, na hii ni kutokana na aina ya malezi na mafundisho yetu.
Mchezaji akikosana na kocha kama Kibadeni, Mkwasa, Mgunda, Minziro, Mwambusi na wengine wa aina hii kutatokea bifu la kufa mtu kati ya kocha na mchezaji, kocha na benchi la ufundi, nk.
Mgunda hana mafunzo ya ukocha ya hali ya juu bali anatumia kipaji, uzoefu na uchezaji mpira wake tu baasi. Kufungwa na Azam huu utakuwa ndio mwanzo mbaya kwa Simba na Mgunga mwenyewe.
Pumba tupu