Mgunda amenishangaza leo Mapinduzi Cup

Angalau ombi langu limesikilizwa.
Hili kombe halifai
 
Kombe la mbuzi hili halina thamani...
 
Alipochemshia ni pale aliposema wana mechi mbili zilizobaki.
 
Timu ya simba haijielewi hata kidogo! Yaani wana mechi 2 tu za kucheza ili kuingia nusu fainali. Na wakati huo huo walitambua fika wapinzani wao wameshacheza mechi na kutoa sare!

Badala ya kuingiza kikosi chake imara ili kupata ushindi, halafu mechi ya pili ndiyo wangefanya mabadiliko! (Maana hawana kikosi kipana! No Chama, no goal! No assist) Wenyewe wakachagua kuanza na kikosi dhaifu. Mwisho wa siku, wameishia tu kufedheheka.
 
Hata mtangazaji sijajua kwanini hakumrekebisha au naye sijui hakujua?
Watangazaji wetu wanapoongea na viongozi wa Simba au Yanga weledi huwa unakufa kabisa. Yaani ni Sawa na wanapoongea na Viongozi wa CCM.
 
Swala la Mgunda kunyang'anywa majukumu kwa kupitia tweet ya Mo limemfedhehesha sana na mechi ya Leo ilikuwa lazima apoteze ili ionekane ni sahihi kuwa na kocha mpya
Point yako naiona, umeongea ukweli Mkuu. Yaani Mwalimu Mkuu wa shule analetewa Mkuu wake yeye anabaki Mwalimu wa kawaida? Lazima vitu vipotee kichwani.
 
Watarudiana na Mlasimba kwa heshima ya zile goli 7 na kumuenzi PELE.
 
Kukosea ni kawaida hata kipindi tunacheza mashindano ya CAF na Agosto aliwahi kusema Agosto ndio mabingwa wa ligi yao kitu ambacho hakikuwa sahihi
Kuna errors na blunder. Ile kauli dhidi ya Agosto ni error, ila hii ya Jana ni blunder. Unajua kwann? Inaonesha, ameenda Zenji akiwa hajui kundi lake Lina timu ngapi, ni mechi ngapi timu yake inahitajika kucheza hatua ya makundi, si ajabu hata opponents wake hakuwa akiwajua wote.
 
Kukosea ni kawaida hata kipindi tunacheza mashindano ya CAF na Agosto aliwahi kusema Agosto ndio mabingwa wa ligi yao kitu ambacho hakikuwa sahihi
Hata Nabi alipowasili nchini alisema anafurahi kuja kufanya kazi katika klabu kubwa ya Simba
 
We jamaa ,Nina wasi wasi na wewe.
 
Hakuna maana yoyote kuwepo huko Zanzibar kwa sasa.
 
Kawaida tuu kupitiwa ambae hajawahi kukosea na amkosoe
 
Mlandege anacheza na nani hiyo mechi ya pili!!?? Na Simba anacheza na nani mechi ya pili !!?? Ila Rage Kwa kweli ajengewe sanamu Kwa kuwaita MBUX3
 
Mlandege anacheza na nani hiyo mechi ya pili!!?? Na Simba anacheza na nani mechi ya pili !!?? Ila Rage Kwa kweli ajengewe sanamu Kwa kuwaita MBUX3
Sikufuatilia. Ndiyo nimejua sasa kuwa Mlandege alishacheza game moja akatoka sare. Haya mashindano ya kupotezeana muda tu.
 
sio hivyo tu uliona kofia aliyovaa,ni kocha wa simba kavaa kofia ya bin slum
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…