Mgunda amenishangaza leo Mapinduzi Cup

Mgunda amenishangaza leo Mapinduzi Cup

Angalau ombi langu limesikilizwa.
Hili kombe halifai
 
Kombe la mbuzi hili halina thamani...
 
Akihojiwa na mtangazaji wa Azam TV baada ya kupoteza mechi dhidi ya Mlandege 0-1 amesema bado ana matumaini ya kushinda mechi 2 zilizobaki katika kundi lao C na kutinga hatua ya nusu fainali kutetea ubingwa wao.

Tangu ratiba inatolewa kundi C lilikuwa na timu 3 tu yaani;

1. Simba
2. Mlandege
3. KVZ

Mechi ya kwanza kwenye kundi hili ilikuwa baina ya Mlandege na KVZ iliyomalizika kwa sare ya 1-1 na Leo mechi ya pili Simba vs Mlandege.

Kwa maana nyingine Kundi limebakiza mechi moja tu Simba vs KVZ ambayo hata Simba akishinda anapata point 3 ambazo hazitamsaidia kuongoza kundi maana tayari Mlandege ana pwenti 4 na anahtajika mshindi mmoja tu.

Labda uelewa wangu kuhusu kanuni za mashindano haya siyo mzuri kiasi kwamba Simba kweli bado ana mechi 2?
Alipochemshia ni pale aliposema wana mechi mbili zilizobaki.
 
Timu ya simba haijielewi hata kidogo! Yaani wana mechi 2 tu za kucheza ili kuingia nusu fainali. Na wakati huo huo walitambua fika wapinzani wao wameshacheza mechi na kutoa sare!

Badala ya kuingiza kikosi chake imara ili kupata ushindi, halafu mechi ya pili ndiyo wangefanya mabadiliko! (Maana hawana kikosi kipana! No Chama, no goal! No assist) Wenyewe wakachagua kuanza na kikosi dhaifu. Mwisho wa siku, wameishia tu kufedheheka.
 
Swala la Mgunda kunyang'anywa majukumu kwa kupitia tweet ya Mo limemfedhehesha sana na mechi ya Leo ilikuwa lazima apoteze ili ionekane ni sahihi kuwa na kocha mpya
Point yako naiona, umeongea ukweli Mkuu. Yaani Mwalimu Mkuu wa shule analetewa Mkuu wake yeye anabaki Mwalimu wa kawaida? Lazima vitu vipotee kichwani.
 
Akihojiwa na mtangazaji wa Azam TV baada ya kupoteza mechi dhidi ya Mlandege 0-1 amesema bado ana matumaini ya kushinda mechi 2 zilizobaki katika kundi lao C na kutinga hatua ya nusu fainali kutetea ubingwa wao.

Tangu ratiba inatolewa kundi C lilikuwa na timu 3 tu yaani;

1. Simba
2. Mlandege
3. KVZ

Mechi ya kwanza kwenye kundi hili ilikuwa baina ya Mlandege na KVZ iliyomalizika kwa sare ya 1-1 na Leo mechi ya pili Simba vs Mlandege.

Kwa maana nyingine Kundi limebakiza mechi moja tu Simba vs KVZ ambayo hata Simba akishinda anapata point 3 ambazo hazitamsaidia kuongoza kundi maana tayari Mlandege ana pwenti 4 na anahtajika mshindi mmoja tu.

Labda uelewa wangu kuhusu kanuni za mashindano haya siyo mzuri kiasi kwamba Simba kweli bado ana mechi 2?
Watarudiana na Mlasimba kwa heshima ya zile goli 7 na kumuenzi PELE.
 
Kukosea ni kawaida hata kipindi tunacheza mashindano ya CAF na Agosto aliwahi kusema Agosto ndio mabingwa wa ligi yao kitu ambacho hakikuwa sahihi
Kuna errors na blunder. Ile kauli dhidi ya Agosto ni error, ila hii ya Jana ni blunder. Unajua kwann? Inaonesha, ameenda Zenji akiwa hajui kundi lake Lina timu ngapi, ni mechi ngapi timu yake inahitajika kucheza hatua ya makundi, si ajabu hata opponents wake hakuwa akiwajua wote.
 
Kukosea ni kawaida hata kipindi tunacheza mashindano ya CAF na Agosto aliwahi kusema Agosto ndio mabingwa wa ligi yao kitu ambacho hakikuwa sahihi
Hata Nabi alipowasili nchini alisema anafurahi kuja kufanya kazi katika klabu kubwa ya Simba
 
Wote hamjui mnachoongea. Simba bado ana mechi moja na akishinda hiyo, halafu Mlandege akifungwa mechi yake ya pili, timu zote zitakuwa na point 3 na mshindi wa group atapatikana kwa tofauti ya magoli.

Simba wasiliachie kombe hili. Wanaolidhihaki wanaogopa kufungwa ndiyo maana wanajidai kutolitilia mkazo ila trust me nao wanalitaka sana tu.
We jamaa ,Nina wasi wasi na wewe.
 
Hakuna maana yoyote kuwepo huko Zanzibar kwa sasa.
 
Kawaida tuu kupitiwa ambae hajawahi kukosea na amkosoe
 
Wote hamjui mnachoongea. Simba bado ana mechi moja na akishinda hiyo, halafu Mlandege akifungwa mechi yake ya pili, timu zote zitakuwa na point 3 na mshindi wa group atapatikana kwa tofauti ya magoli.

Simba wasiliachie kombe hili. Wanaolidhihaki wanaogopa kufungwa ndiyo maana wanajidai kutolitilia mkazo ila trust me nao wanalitaka sana tu.
Mlandege anacheza na nani hiyo mechi ya pili!!?? Na Simba anacheza na nani mechi ya pili !!?? Ila Rage Kwa kweli ajengewe sanamu Kwa kuwaita MBUX3
 
Sikufuatilia. Ndiyo nimejua sasa kuwa Mlandege alishacheza game moja akatoka sare. Haya mashindano ya kupotezeana muda tu.
 
Akihojiwa na mtangazaji wa Azam TV baada ya kupoteza mechi dhidi ya Mlandege 0-1 amesema bado ana matumaini ya kushinda mechi 2 zilizobaki katika kundi lao C na kutinga hatua ya nusu fainali kutetea ubingwa wao.

Tangu ratiba inatolewa kundi C lilikuwa na timu 3 tu yaani;

1. Simba
2. Mlandege
3. KVZ

Mechi ya kwanza kwenye kundi hili ilikuwa baina ya Mlandege na KVZ iliyomalizika kwa sare ya 1-1 na Leo mechi ya pili Simba vs Mlandege.

Kwa maana nyingine Kundi limebakiza mechi moja tu Simba vs KVZ ambayo hata Simba akishinda anapata point 3 ambazo hazitamsaidia kuongoza kundi maana tayari Mlandege ana pwenti 4 na anahtajika mshindi mmoja tu.

Labda uelewa wangu kuhusu kanuni za mashindano haya siyo mzuri kiasi kwamba Simba kweli bado ana mechi 2?
sio hivyo tu uliona kofia aliyovaa,ni kocha wa simba kavaa kofia ya bin slum
 
Back
Top Bottom