Vawulence
JF-Expert Member
- Jan 4, 2009
- 1,930
- 2,118
Leo 27.10.2022 Simba watakuwa uwanjani wakiwakabili Azam FC. Timu zote zinakutana zikiwa hazina makocha wakuu bali zikiwa na makocha wa muda.
Simba leo watakosa huduma ya Sadio Kanoute (Putin) na Mzamiru Yasin (kiungo punda) kwenye mafasi ya kiungo. Kanoute ni mgonjwa wakati Mzamiru akiwa na kadi 3 za njano hivyo kanuni kumtaka akose mchezo mmoja wa Ligi Kuu.
Juma Mgunda atalazimika kuwatumia Nelson Okwa na Nasoro Kapama kwa pamoja au kwa wakati tofauti.
Hii inaweza kuwa nafasi adimu sana kwa wachezaji hao kuonesha uwezo wao ili waaminike kuingia kikosi cha kwanza cha Simba FC.
Lakini pia Peter Banda na Enock Hinonga wana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya kiungo kwa ufanisi mkubwa, hivyo haitashangaza kama Kocha ataamua kumtumia mmoja wao katikati.
Okwa na Kapama wanaweza kupata nafasi moja ya kuthibitisha ubora wao leo.